Ayubu 37 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 37:1-24

137:1 Za 38:10; Isa 15:5; Yer 4:19; Hab 3:16“Kwa hili moyo wangu unatetemeka,

nao unaruka kutoka mahali pake.

237:2 Za 18:13; 29:3-9Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake,

sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake.

337:3 2Sam 22:13; Za 18:14; Ay 36:32; Mt 24:27; Lk 17:24Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote

na kuupeleka hata miisho ya dunia.

437:4 1Sam 2:10; Kut 20:19Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake;

Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari.

Wakati sauti yake ingurumapo tena,

huuachilia umeme wake wa radi.

537:5 Ay 11:7-9Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu;

yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.

637:6 Kum 28:12; Ay 38:22; Mwa 7:4; Ay 36:27Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’

nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’

737:7 Ay 12:14; Za 111:2; 109:27; 104:19-23Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake,

yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.

837:8 Ay 28:26; 38:40; Za 104:22Wanyama hujificha;

hubakia kwenye mapango yao.

937:9 Za 50:3; 147:17Dhoruba hutoka katika chumba chake,

baridi hutoka katika upepo uendao kasi.

1037:10 Ay 38:29-30; Za 147:17Pumzi ya Mungu hutoa barafu,

eneo kubwa la maji huganda.

1137:11 Ay 26:8; 36:30; 28:26Huyasheheneza mawingu kwa maji,

naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.

1237:12 Za 147:16; 148:8; Ay 37:3Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake,

juu ya uso wa dunia yote,

kufanya lolote ayaamuruyo.

1337:13 Kut 9:22-23; 1Sam 12:17; Kut 9:18; 1Fal 18:45Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu,

au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.

1437:14 Ay 32:10; 5:9“Ayubu, sikiliza hili;

nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu.

1537:15 Ay 36:30, 32Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu,

na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?

1637:16 Ay 36:29; 5:9; 36:4Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia,

hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?

1737:17 Mdo 27:13Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako

wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini,

1837:18 Mwa 1:1, 8; Ay 22:14; Kum 28:23; Za 104:2je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga,

zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa?

1937:19 Rum 8:26; Ay 13:18; 9:3“Tuambieni yatupasayo kumwambia;

hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu.

20Je, aambiwe kwamba nataka kuongea?

Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa?

2137:21 Amu 5:31; Mdo 22:1; 26:13Basi hakuna awezaye kulitazama jua,

jinsi linavyongʼaa angani,

upepo ukishafagia mawingu.

2237:22 Za 19:5; Kut 24:17Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu;

Mungu huja katika utukufu wa kutisha.

2337:23 Ay 5:9; Rum 11:33; Ay 8:3; Yer 25:5; Mao 3:33Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza;

katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.

2437:24 Mik 6:8; Mt 10:28; 11:25; Efe 5:15Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni,

kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约伯记 37:1-24

1“因此我心战栗,

在胸膛跳动。

2请仔细听祂发出的雷声,

听祂口中发出的轰鸣。

3祂使闪电划过整个天空,

亮光直照到地极。

4随后雷声隆隆,

祂发出威严之声。

祂一发声,雷电交加。

5上帝发出奇妙的雷声,

我们无法测度祂伟大的作为。

6祂命雪降在大地,

令雨倾盆倒下,

7使人们停下工作,

以便世人都知道祂的作为。

8野兽躲进窝里,

留在洞中。

9暴风从南天而来,

寒流由北方而至。

10上帝嘘气成冰,

使宽阔的水面凝结。

11祂使密云布满水气,

从云端发出闪电。

12云随祂的指令旋转,

在地面之上完成祂的吩咐,

13或为惩罚大地,

或为彰显慈爱。

14约伯啊,请留心听,

要驻足沉思上帝的奇妙作为。

15你知道上帝如何发出命令,

使云中电光闪烁吗?

16你知道全知者的奇妙作为——

祂如何使云彩飘浮吗?

17南风吹来,大地沉寂时,

你就汗湿衣襟,你知道为何吗?

18你能像祂那样铺展坚如铜镜的穹苍吗?

19我们因愚昧而无法陈诉,

请指教我们如何与祂对话。

20我怎敢与祂对话?

岂有人自取灭亡?

21风吹散天空的云后,

无人能仰视太阳的强光。

22北方出现金色的光芒,

上帝充满可怕的威严。

23我们无法测度全能者,

祂充满能力,无比正直公义,

不恃强凌弱。

24所以,人们都敬畏祂,

祂不看顾自以为有智慧的人。”