Ayubu 30 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 30:1-31

130:1 Ay 12:4; Za 119:21“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki,

watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau

kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.

2Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu,

kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?

330:3 Isa 8:21; Ay 24:5; Yer 17:6Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa,

walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.

430:4 Ay 39:6; 1Fal 19:4Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi,

nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.

5Walifukuzwa mbali na watu wao,

wakipigiwa kelele kama wevi.

630:6 Isa 2:19; Hos 10:8Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka,

kwenye majabali na mahandaki.

730:7 Ay 6:5; 39:5-6Kwenye vichaka walilia kama punda,

na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka.

830:8 Amu 9:4; Ay 18:18Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya,

waliofukuzwa watoke katika nchi.

930:9 Ay 16:10; 12:4; Za 69:11; Mao 3:14; Ay 16:10; Za 69:11; Ay 12:4; Mao 3:14, 63; Ay 17:6“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo;

nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.

1030:10 Hes 12:14; Mt 26:67Wananichukia sana na kujitenga nami,

wala hawasiti kunitemea mate usoni.

1130:11 Mwa 12:17; Rut 1:21; Ay 41:13; Za 32:9Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa,

wamekuwa huru kunitendea waonavyo.

1230:12 Za 109:6; Zek 3:1; Za 140:4-5; Ay 16:10Kuume kwangu kundi linashambulia;

wao huitegea miguu yangu tanzi,

na kunizingira.

1330:13 Isa 3:12; Za 69:26Huizuia njia yangu,

nao hufanikiwa katika kuniletea maafa,

nami sina yeyote wa kunisaidia.

14Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana;

katikati ya magofu huja na kunishambulia.

1530:15 Kut 3:6; Za 55:4-5; Hos 13:3; Ay 3:25Vitisho vimenifunika;

heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo,

salama yangu imetoweka kama wingu.

1630:16 Za 22:14; Isa 53:12“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho;

siku za mateso zimenikamata.

17Usiku mifupa yangu inachoma;

maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.

18Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo;

hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.

1930:19 Za 40:2; Yer 38:6, 22Yeye amenitupa kwenye matope,

nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.

2030:20 Ay 19:7; Mao 3:8; Mt 15:23“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu;

ninasimama, nawe unanitazama tu.

2130:21 Ay 19:6; Yer 6:23; Isa 9:12; Eze 6:14; Ay 10:3Wewe unanigeukia bila huruma;

unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.

2230:22 Ay 27:21; 9:17; Yud 12Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo;

umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.

2330:23 2Sam 14:14; Ay 3:19; 10:8Ninajua utanileta mpaka kifoni,

mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.

24“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji,

anapoomba msaada katika shida yake.

2530:25 Za 35:13-14; Rum 12:15; Yn 11:35Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu?

Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?

2630:26 Za 82:5; Yer 8:15Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia;

nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.

2730:27 Za 38:8; Mao 2:11Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii;

siku za mateso zinanikabili.

2830:28 Mao 4:8; Za 38:6; Ay 19:7; 24:12Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua;

ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.

2930:29 Isa 34:13; Yer 9:11; Za 102:6; Mik 1:8Nimekuwa ndugu wa mbweha,

rafiki wa mabundi.

3030:30 Mao 3:4; 4:8; 5:10; Kum 28:35Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika;

mifupa yangu inaungua kwa homa.

3130:31 Mwa 8:8; Za 137:2Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo,

nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

約伯記 30:1-31

哀歎今日的痛苦

1「但如今,比我年少的人竟嘲笑我,

他們的父親曾被我鄙視,

連我的牧羊犬都不如。

2他們精力衰竭,

對我有何益處?

3他們貧窮饑餓,瘦弱不堪,

夜間在乾旱荒涼之地啃食。

4他們在草叢中拔鹹草充饑,

以羅騰樹根為食。

5他們被趕離人群,

像賊一樣被喝斥。

6他們只好住在荒谷,

在地洞和岩穴棲身;

7在雜草間嚎叫如獸,

在樹叢中蜷縮一團。

8他們是愚昧無名之輩,

被人用鞭子趕出境外。

9「如今,他們竟唱歌諷刺我,

我成了他們的笑柄。

10他們厭惡我,不願靠近我,

任意朝我臉上吐唾沫。

11因為上帝苦待我,使我毫無力量,

他們才在我面前肆無忌憚。

12這些無賴從右邊攻擊我,

迫使我逃亡,

他們展開攻勢要毀滅我。

13他們截斷我的路,

想方設法害我,無人相助。

14他們衝破防線,

從廢墟中向我襲來。

15恐懼籠罩著我,

我的尊榮隨風而去,

我的榮華如雲消散。

16「如今我的生命將盡,

痛苦的日子抓住我。

17夜間我的骨頭刺痛,

如被啃噬,無休無止。

18上帝猛力抓住我的衣服,

緊緊地揪住我的衣領。

19祂把我扔進淤泥,

使我如塵埃灰燼。

20「上帝啊!我向你呼求,你不回應;

我站起來,你也不理睬。

21你變得對我殘酷無情,

用你大能的手迫害我,

22把我提到風中,讓我被風吹走,

被暴風拋來拋去。

23我知道你要帶我去死亡之地,

那是你為眾生所定的歸宿。

24「誠然,不幸的人在困境中呼救,

無人會伸手加害他。

25難道我不曾為受苦的人哭泣,

我的心不曾為窮困者悲傷嗎?

26我盼望幸福,來的卻是災禍;

我期待光明,來的卻是黑暗。

27我心裡一直煩亂不安,

苦難的日子迎面襲來。

28我皮膚發黑,不是因為日曬,

我在會眾中站起來呼救。

29我成了豺狼的兄弟,

駝鳥的夥伴。

30我的皮膚發黑、脫落,

我的骨頭如被烤焦。

31我的琴唱出哀樂,

我的簫奏出悲鳴。