Ayubu 3 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 3:1-26

Sehemu Ya Pili: Mazungumzo Ya Ayubu Na Rafiki Zake Watatu

(Ayubu 3–31)

Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu

Ayubu Anazungumza

13:1 Yer 15:10; 20:14Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

2Kisha akasema:

33:3 Mhu 6:3; Ay 10:18-19; Yer 15:10; Ay 3:11, 16; Mit 26:24“Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali,

nao usiku ule iliposemekana,

‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

4Siku ile na iwe giza;

Mungu juu na asiiangalie;

nayo nuru isiiangazie.

53:5 Za 44:19; Yer 13:16; Ay 16:16; Isa 9:2; Za 23:4; Mt 4:16; Lk 1:79; Mhu 4:2Giza na kivuli kikuu kiikalie tena;

wingu na likae juu yake;

weusi na uifunike nuru yake.

63:6 Ay 23:17; 30:26; Za 20:5; 33:3; 65:13; Isa 26:19Usiku ule na ushikwe na giza kuu;

usihesabiwe katika siku za mwaka,

wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote.

73:7 Za 20:5; 33:3; Isa 26:19; Yer 51:48Usiku ule na uwe tasa;

sauti ya furaha na isisikike ndani yake.

83:8 Yer 9:17Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku,

wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.3:8 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.

93:9 Ay 41:18; Hab 3:4Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;

nao ungojee mwanga bila mafanikio,

wala usiuone mwonzi wa kwanza

wa mapambazuko,

10kwa sababu huo usiku haukunifungia

mlango wa tumbo la mama yangu,

ili kuyaficha macho yangu

kutokana na taabu.

113:11 Ay 3:3“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa?

Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

123:12 Mwa 30:3; 48:12; Isa 66:12Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea

na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

133:13 Ay 17:13; 30:23; 3:17; 7:8-10, 21; 3:19; 14:10-12; Za 139:11; Isa 8:22Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani.

Ningekuwa nimelala na kupumzika

143:14 Isa 14:9; Eze 32:28-32; Yer 51:37; Nah 3:7; Ay 9:24; 12:17; 15:28pamoja na wafalme na washauri wa dunia,

waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,

153:15 Ay 12:21; 15:29; 20:10; 27:17; Mit 13:22; Sef 1:11; Isa 45:1; Za 49:16-17; 45:1; Mit 13:22pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu,

waliozijaza nyumba zao kwa fedha.

163:16 Mhu 6:3; 4:3; Za 58:8; 71:6Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu,

kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?

173:17 Ay 3:26; 30:26; 17:16; Mhu 4:2; Isa 14:3Huko waovu huacha kusumbua

na huko waliochoka hupumzika.

183:18 Ay 38:7; 39:7; Isa 51:14; Mwa 15:13Wafungwa nao hufurahia utulivu wao,

hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.

193:19 Ay 9:22; 17:16; 21:33; 24:24; 30:23; Mhu 12:5Wadogo na wakubwa wamo humo,

na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.

203:20 Yer 20:18; Eze 27:30-31; 1Sam 1:10“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni,

na hao wenye uchungu kupewa uhai,

213:21 Ufu 9:6; Mit 2:4; Za 119:127wale wanaotamani kifo ambacho hakiji,

wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,

223:22 Ay 7:16; Mhu 4:3; Yer 8:3ambao hujawa na furaha,

na hushangilia wafikapo kaburini?

233:23 Mao 2:4; 3:7; Hos 2:6; Mt 4:19; Isa 59:10; Yer 13:16; 23:12; Ay 6:4; 16:13; Za 88:8Kwa nini uhai hupewa mtu

ambaye njia yake imefichika,

ambaye Mungu amemzungushia boma?

243:24 Ay 33:20; Mao 2:12; 1Sam 1:15; Isa 35:10; 53:12; Za 6:6; 22:1; 32:3; 107:18Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula;

kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.

253:25 Hos 13:3; Ay 7:9; 30:15; 9:28; Mwa 42:36Lile nililokuwa naliogopa limenijia;

lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

263:26 Dan 4:5; Mt 11:28; Isa 48:22; Yn 14:27Sina amani, wala utulivu;

sina pumziko, bali taabu tu.”

New International Version

Job 3:1-26

Job Speaks

1After this, Job opened his mouth and cursed the day of his birth. 2He said:

3“May the day of my birth perish,

and the night that said, ‘A boy is conceived!’

4That day—may it turn to darkness;

may God above not care about it;

may no light shine on it.

5May gloom and utter darkness claim it once more;

may a cloud settle over it;

may blackness overwhelm it.

6That night—may thick darkness seize it;

may it not be included among the days of the year

nor be entered in any of the months.

7May that night be barren;

may no shout of joy be heard in it.

8May those who curse days3:8 Or curse the sea curse that day,

those who are ready to rouse Leviathan.

9May its morning stars become dark;

may it wait for daylight in vain

and not see the first rays of dawn,

10for it did not shut the doors of the womb on me

to hide trouble from my eyes.

11“Why did I not perish at birth,

and die as I came from the womb?

12Why were there knees to receive me

and breasts that I might be nursed?

13For now I would be lying down in peace;

I would be asleep and at rest

14with kings and rulers of the earth,

who built for themselves places now lying in ruins,

15with princes who had gold,

who filled their houses with silver.

16Or why was I not hidden away in the ground like a stillborn child,

like an infant who never saw the light of day?

17There the wicked cease from turmoil,

and there the weary are at rest.

18Captives also enjoy their ease;

they no longer hear the slave driver’s shout.

19The small and the great are there,

and the slaves are freed from their owners.

20“Why is light given to those in misery,

and life to the bitter of soul,

21to those who long for death that does not come,

who search for it more than for hidden treasure,

22who are filled with gladness

and rejoice when they reach the grave?

23Why is life given to a man

whose way is hidden,

whom God has hedged in?

24For sighing has become my daily food;

my groans pour out like water.

25What I feared has come upon me;

what I dreaded has happened to me.

26I have no peace, no quietness;

I have no rest, but only turmoil.”