Ayubu 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 2:1-13

Jaribu La Pili La Ayubu

12:1 Ay 1:6; Mwa 6:2Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. 22:2 Mwa 3:1Bwana akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibu Bwana “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

32:3 Kut 20:20; Ay 6:29; 9:17; 13:18; Yak 1:12; Za 44:17; Ay 13:18; 27:5, 6; 1Pet 1:7; Mt 7:11; Yn 9:2Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

42:4 Ay 1:10Shetani akamjibu Bwana, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake. 52:5 Za 102:5; Ay 19:20; Mao 4:8; Za 32:3, 4; Ay 16:8; 1:11Lakini nyoosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

62:6 Ay 1:12; 2Kor 12:7Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umwachie uhai wake.”

72:7 Kum 28:35; Ay 7:5; 16:16Basi Shetani akatoka mbele za Bwana naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. 82:8 2Sam 13:19; Za 7:5; Mt 11:21; Mwa 18:27; Es 4:3; Ay 16:15; 19:9; 42:6; Isa 5:8; 6:13; Yer 6:26; Mao 3:29; Eze 26:16; Yon 3:5-8Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

92:9 Ay 1:21; 13:15; 27:5; 33:9; 35:2; 1The 5:8; Kut 20:7; 2Fal 6:33Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

102:10 Mhu 2:24; Mao 3:38-41; Yak 5:11; Za 39:1Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu2:10 Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili. yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

112:11 Mwa 25:2; 36:11; 37:35; Yer 49:7; Rum 12:15; Ay 11:1; 20:1; Yn 11:19Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. 122:12 2Sam 1:2; Neh 9:1; Eze 27:30; Ay 17:7; Isa 52:14; Mwa 37:29; Mk 14:63; Yos 7:6Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. 132:13 Mwa 50:10-12; Eze 3:15; Isa 3:26; 47:1; Eze 26:16; Yn 3:6; Hag 2:22; Mit 17:28; Isa 23:2; 47:5Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约伯记 2:1-13

约伯失去健康

1又有一天,众天使来朝见耶和华,撒旦也在他们当中。 2耶和华问撒旦:“你从哪里来?”撒旦答道:“我在地上到处游走。” 3耶和华问道:“你注意到我的仆人约伯了吗?世上没有人像他那样纯全正直,敬畏我,远离罪恶。虽然你鼓动我无缘无故地攻击他、毁灭他,他仍然持守自己的纯正。” 4撒旦回答说:“人会以皮换皮,为了保全生命,情愿舍弃一切。 5倘若你伸手伤害他的骨和肉,他必当面亵渎你。” 6耶和华说:“好吧,他在你手中,但要留他一命。” 7于是,撒旦从耶和华面前退去,开始加害约伯,使他从头到脚长毒疮。 8约伯坐在炉灰中,拿瓦片刮身体。 9他的妻子对他说:“你还要持守自己的纯正吗?不如亵渎上帝,死掉算了!” 10约伯回答说:“你说话像个愚昧的妇人。难道我们只从上帝手里接受祝福,却不接受灾殃吗?”约伯遭此不幸,仍毫无怨言。

约伯的三个朋友

11约伯的三个朋友提幔以利法书亚比勒达拿玛琐法听到他的不幸遭遇,便各自从家乡动身,相约一起来探望、安慰他。 12他们远远地看见约伯,几乎认不出是他,禁不住放声大哭,各自撕裂外袍,扬起尘土,让土落在头上。 13他们看到约伯极其痛苦,就陪着他在地上坐了七天七夜,没有对他说一句话。