Ayubu 14 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 14:1-22

114:1 Mhu 2:23; Mwa 3:17; Ay 15:14; 10:20; Mt 11:11; Za 51:5“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke

siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.

214:2 Za 103:15; Yak 1:10; 1Pet 1:24; Isa 40:6-8; Mhu 6:12Huchanua kama ua kisha hunyauka;

huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.

314:3 Za 144:3; 8:4; 143:2; Ay 7:18Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo?

Je, utamleta mbele yako katika hukumu?

414:4 Mwa 5:3; Ay 4:17; Za 51:10; Rum 5:12; Efe 2:1-3; Yn 3:6Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi?

Hakuna awezaye!

514:5 Ay 24:1; 21:21; Za 31:15; 139:16; 39:4; 90:12; Mdo 17:26Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka;

umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake

na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.

614:6 Ay 7:19; 7:1, 2; Za 39:13; Isa 16:14; 21:16Hivyo angalia mbali umwache,

hadi awe amekamilisha muda wake

kama mtu aliyeajiriwa.

714:7 Ay 19:10; 24:20; Za 52:5; Isa 11:1; 53:2; 60:21; 6:13“Kwa maana lipo tumaini kwa mti;

kama ukikatwa utachipuka tena,

nayo machipukizi yake mapya hayatakoma.

814:8 Isa 6:13; 11:1; 53:2Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini

na kisiki chake kufa udongoni,

914:9 Ay 29:9; Zek 10:1; Za 1:3; Yer 17:8; Eze 31:7; Law 26:4; Eze 34:27lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua

na kutoa machipukizi kama mche.

1014:10 Ay 14:12; 10:21; 13:19Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake;

hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena!

1114:11 2Sam 14:14; Isa 19:5Kama vile maji yatowekavyo katika bahari,

au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu,

1214:12 Za 102:26; Ufu 21:1; Mdo 3:21; Ay 14:10; Ufu 20:11ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke;

hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena,

wanadamu hawataamka au kuamshwa

kutoka kwenye usingizi wao.

1314:13 Za 30:5; Isa 54:7; Ay 6:8; 7:9; Isa 26:20; 54:7; Mwa 8:1“Laiti kama ungenificha kaburini,14:13 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

na kunisitiri hadi hasira yako ipite!

Laiti ungeniwekea wakati,

na kisha ukanikumbuka!

1414:14 Ay 7:1; 2Fal 6:33; Za 16:10; 1Kor 15:42-58; Flp 3:21Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena?

Siku zote za kazi zangu ngumu

nitangojea kufanywa upya kwangu.

1514:15 Ay 13:22; Yn 5:28; 1The 4:16; Za 50:4Utaniita nami nitakuitika;

utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.

1614:16 Mit 5:21; Yer 16:17; 32:19; Hos 13:12; 1Kor 13:5Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu,

lakini hutazifuatia dhambi zangu.

1714:17 Kum 32:34; Ay 13:23; 9:30; Yer 32:10Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko,

nawe utazifunika dhambi zangu.

1814:18 Eze 38:20; Ay 18:4“Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika

na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake,

1914:19 Eze 13:13; Mwa 7:23; Ay 7:8kama maji yamalizavyo mawe,

na mafuriko yachukuavyo udongo,

ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu.

2014:20 Ay 4:20; 7:10; 8:18; 12:19; 27:19; Yak 1:10Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka;

waibadilisha sura yake na kumwondoa.

2114:21 Mhu 9:5; Isa 63:16; 1Sam 4:20Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu;

kama wakidharauliwa, yeye haoni.

2214:22 Za 38:7; Isa 21:3; Yer 4:19; Ay 21:21Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe,

naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约伯记 14:1-22

1“人为妇人所生,

一生短暂,充满患难。

2他如花盛开,转眼凋谢;

如影消逝,无法久留。

3你还察看这样的世人吗?

还要把我召来受审吗?

4谁能使污秽产生洁净呢?

没有人能。

5人的年日已被限定,

你掌管他的岁月,

设定他无法逾越的界限。

6求你转身,别去管他,

好让他如雇工度完他的日子。

7树木若被砍下,还有希望,

它仍可重新萌芽,

嫩枝生长不息。

8虽然树根在土里衰老,

树干在地里死去,

9但一有水气,

它就会像新栽的树一样发芽长枝。

10但人一死,就失去力量;

人一咽气,就不知去向。

11湖水会枯竭,

江河会干涸,

12人躺下便不再起来,

到诸天不复存在,

他仍不会醒来,

不会从长眠中被唤醒。

13但愿你把我藏在阴间,

把我藏起来直到你息怒,

定下眷顾我的日期。

14人若死了,还能复生吗?

我要在劳苦的岁月中等待,

直到我得释放的日子来临。

15那时你呼唤,我便回应,

你必惦念你亲手所造之物。

16那时你必鉴察我的脚步,

但不会追究我的罪恶。

17我的过犯会被封在袋中,

你会遮盖我的罪愆。

18“高山崩塌,

磐石挪移;

19流水磨损石头,

急流冲走泥土;

你也这样粉碎人的希望。

20你永远击败他,使他消逝;

你改变他的容颜,让他离世。

21他的后人得尊荣,他无从知晓;

他们遭贬抑,他也无法察觉。

22他只能感受自身的痛苦,

为自己哀哭。”