2 Yohana 1 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Yohana 1:1-13

Salamu

11:1 Mdo 11:30; 3Yn 1; Rum 16:13; 1Pet 5:13; Yn 8:32; 1Tim 2:4Mzee:

Kwa bibi mteule na watoto wake, niwapendao katika kweli, wala si mimi tu, bali na wale wote waijuayo kweli: 21:2 2Pet 1:12; Yn 14:17; 1Yn 1:8kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itaendelea kukaa nasi milele:

31:3 Rum 1:7; 1Tim 1:2; 2Yn 1; 1:4; 3Yn 3, 4Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwanawe Baba, itakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

Kweli Na Upendo

4Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza. 51:5 1Yn 2:7; 3:11Sasa, bibi mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake. 61:6 1Yn 2:5; Yn 14:15; 1Yn 2:7Hili ndilo pendo, kwamba tuenende sawasawa na amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.

71:7 1Yn 2:22; 4:2, 3; 4:1; 2:18Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na mpinga Kristo. 81:8 Mt 10:42; Ebr 11:26Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu. 91:9 1Yn 2:23; Yn 8:31Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. 101:10 Rum 16:17; 2The 3:6; 1Fal 13:17; 3Yn 8Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. 111:11 1Tim 5:22Yeyote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.

Salamu Za Mwisho

121:12 3Yn 13, 14; Yn 17:13; 1Yn 1:4Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

131:13 1Pet 5:13; 2Yn 1Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

約翰二書 1:1-13

1我這作長老的寫信給蒙揀選的女士1·1 學者一般認為「蒙揀選的女士」是指教會。和你的兒女,就是我本著真理所愛的。你們不單是我所愛的,也是一切認識真理的人所愛的。 2我們愛你們,因為真理在我們裡面,並且永遠與我們同在。

3從父上帝和祂兒子耶穌基督而來的恩典、憐憫和平安也必在真理和愛中與我們同在!

彼此相愛

4你的兒女當中有人按照我們從父領受的命令遵行真理,我知道後非常欣慰。 5女士啊,我現在勸你,我們大家要彼此相愛。這不是新命令,而是我們從起初就已經領受的命令。 6愛就是遵行上帝的命令,這是你們從起初就聽過又當遵行的命令。

提防騙子

7因為現在世上有許多騙子出來迷惑人,他們否認耶穌基督曾降世為人。這樣的人是騙子,是敵基督者。 8你們要謹慎,好得到完滿的賞賜,免得我們前功盡棄。 9誰偏離基督的教導,誰心中就沒有上帝;誰遵守基督的教導,誰就有父和子與他同在。 10若有人到你們那裡不傳基督的教導,不要請他到家裡,也不要問候他, 11因為問候他就是與他同流合污。

結語

12我還有許多事要告訴你們,但不想藉助紙墨,而是希望有機會到你們那裡與你們當面暢談,使我們充滿喜樂。

13你那蒙揀選之姊妹的兒女問候你。