2 Wathesalonike 1 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wathesalonike 1:1-12

11:1 Mdo 16:1; 1The 1:1Paulo, Silvano1:1 Yaani Sila. na Timotheo:

Kwa kanisa la Wathesalonike mlio katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo:

21:2 Rum 1:7; 1Kor 1:3Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

Shukrani Na Maombi

31:3 1The 3:12; 1:2, 3; 2The 2:13Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. 41:4 2Kor 7:14; 1The 1:3; 1:6Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

51:5 Flp 1:28Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake. 61:6 Rum 12:19; Ufu 6:10Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi 71:7 1The 4:16; Yud 14na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 81:8 Gal 4:8; Rum 2:8Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. 91:9 1The 5:3; 2Pet 3:7; 2The 2:8Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, 101:10 1Kor 3:13; Yn 17:10; 1Kor 1:6siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.

111:11 1The 1:3; 2The 1:5Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu. 121:12 Flp 2:9, 11; 1Pet 1:7; 4:14Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Yesu lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.

New International Version – UK

2 Thessalonians 1:1-12

1Paul, Silas1:1 Greek Silvanus, a variant of Silas and Timothy,

To the church of the Thessalonians in God our Father and the Lord Jesus Christ:

2Grace and peace to you from God the Father and the Lord Jesus Christ.

Thanksgiving and prayer

3We ought always to thank God for you, brothers and sisters,1:3 The Greek word for brothers and sisters (adelphoi) refers here to believers, both men and women, as part of God’s family; also in 2:1, 13, 15; 3:1, 6, 13. and rightly so, because your faith is growing more and more, and the love all of you have for one another is increasing. 4Therefore, among God’s churches we boast about your perseverance and faith in all the persecutions and trials you are enduring.

5All this is evidence that God’s judgment is right, and as a result you will be counted worthy of the kingdom of God, for which you are suffering. 6God is just: he will pay back trouble to those who trouble you 7and give relief to you who are troubled, and to us as well. This will happen when the Lord Jesus is revealed from heaven in blazing fire with his powerful angels. 8He will punish those who do not know God and do not obey the gospel of our Lord Jesus. 9They will be punished with everlasting destruction and shut out from the presence of the Lord and from the glory of his might 10on the day he comes to be glorified in his holy people and to be marvelled at among all those who have believed. This includes you, because you believed our testimony to you.

11With this in mind, we constantly pray for you, that our God may make you worthy of his calling, and that by his power he may bring to fruition your every desire for goodness and your every deed prompted by faith. 12We pray this so that the name of our Lord Jesus may be glorified in you, and you in him, according to the grace of our God and the Lord Jesus Christ.1:12 Or God and Lord, Jesus Christ