2 Wakorintho 9 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wakorintho 9:1-15

Wasaidieni Wakristo Wenzenu

19:1 1The 4:9; Mdo 24; 17; 9:13Hakuna haja yangu kuwaandikia kuhusu huduma hii itolewayo kwa ajili ya watakatifu. 29:2 2Kor 8:11-19; 7:4, 14; 8:10, 24; Mdo 18:12Kwa kuwa ninajua mlivyo na shauku ya kusaidia, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili ya jambo hilo kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana na shauku yenu imewachochea wengi wao katika kutoa. 39:3 2Kor 8:23; 1Kor 16:2Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusiwe maneno matupu, bali mpate kuwa tayari kama nilivyosema mngekuwa tayari. 49:4 Rum 15:26Kwa maana kama nikija na Mmakedonia yeyote na kuwakuta hamjawa tayari, tutaona aibu kusema chochote juu yenu katika matoleo. 59:5 Flp 4:17; 2Kor 12:17-18Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.

Kupanda Kwa Ukarimu

69:6 Mit 11:24-25; 22:9; Gal 6:7-9Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. 79:7 Kut 25:2; 2Kor 8:12; Kum 15:10; Rum 12:8Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. 89:8 Efe 3:20; Flp 4:19Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. 99:9 Mal 3:10; Za 112:9Kama ilivyoandikwa:

“Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu

akawapa maskini;

haki yake hudumu milele.”

109:10 Isa 55:10; Hos 10:12Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 119:11 1Kor 1:5; 2Kor 1:11; 4:15Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

129:12 2Kor 8:12; 1:11Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. 13Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote. 149:14 2Kor 8:1Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. 159:15 2Kor 2:14; Rum 5:15-16Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

King James Version

2 Corinthians 9:1-15

1For as touching the ministering to the saints, it is superfluous for me to write to you: 2For I know the forwardness of your mind, for which I boast of you to them of Macedonia, that Achaia was ready a year ago; and your zeal hath provoked very many. 3Yet have I sent the brethren, lest our boasting of you should be in vain in this behalf; that, as I said, ye may be ready: 4Lest haply if they of Macedonia come with me, and find you unprepared, we (that we say not, ye) should be ashamed in this same confident boasting. 5Therefore I thought it necessary to exhort the brethren, that they would go before unto you, and make up beforehand your bounty, whereof ye had notice before, that the same might be ready, as a matter of bounty, and not as of covetousness. 6But this I say, He which soweth sparingly shall reap also sparingly; and he which soweth bountifully shall reap also bountifully. 7Every man according as he purposeth in his heart, so let him give; not grudgingly, or of necessity: for God loveth a cheerful giver. 8And God is able to make all grace abound toward you; that ye, always having all sufficiency in all things, may abound to every good work: 9(As it is written, He hath dispersed abroad; he hath given to the poor: his righteousness remaineth for ever. 10Now he that ministereth seed to the sower both minister bread for your food, and multiply your seed sown, and increase the fruits of your righteousness;) 11Being enriched in every thing to all bountifulness, which causeth through us thanksgiving to God. 12For the administration of this service not only supplieth the want of the saints, but is abundant also by many thanksgivings unto God; 13Whiles by the experiment of this ministration they glorify God for your professed subjection unto the gospel of Christ, and for your liberal distribution unto them, and unto all men; 14And by their prayer for you, which long after you for the exceeding grace of God in you. 15Thanks be unto God for his unspeakable gift.