2 Wakorintho 3 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wakorintho 3:1-18

Wahudumu Wa Agano Jipya

13:1 Rum 16:1; 2Kor 5:12; 10:12-18; 12:11; Mdo 18:17; Rum 16:1; 1Kor 3:16Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine? 23:2 1Kor 9:2Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu. 33:3 Mt 16:16; Kut 24:12; 31:18; 32:15-16; Mit 3:3; 7:3; Yer 31:33; Eze 36:26Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.

43:4 Efe 3:12Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 53:5 2Kor 2:16; 1Kor 15:10Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu. 63:6 Lk 22:20; Rum 2:29; 7:6; Yn 6:63Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.

Utukufu Wa Agano Jipya

73:7 Rum 4:15; Kut 34:29-35; Isa 42:21Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu, hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake ingawa ulikuwa ni wa kufifia, 83:8 Gal 3; 5; 3:2je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? 93:9 Kum 27:26; Rum 1:17; 3:21-22Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi? 103:10 Kut 34:29Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Agano Jipya. 11Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu?

123:12 Rum 5:4-5; 8:24-25; Mdo 4:29Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. 133:13 Kut 34:33; 2Kor 3:7; Kut 34:35; Rum 10:4Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. 143:14 Rum 11:7-8; 2Kor 4:4; Mdo 13:15; 15:21Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa. 153:15 Rum 11:23; Kut 34:35; Isa 25:7Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. 163:16 Rum 11:23; Kut 34:34; Isa 25:7Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa. 17Basi Bwana ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru. 183:18 1Kor 13:12; Yn 17:22-24; 2Kor 4:4-6; Rum 8:29Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.

New International Version

2 Corinthians 3:1-18

1Are we beginning to commend ourselves again? Or do we need, like some people, letters of recommendation to you or from you? 2You yourselves are our letter, written on our hearts, known and read by everyone. 3You show that you are a letter from Christ, the result of our ministry, written not with ink but with the Spirit of the living God, not on tablets of stone but on tablets of human hearts.

4Such confidence we have through Christ before God. 5Not that we are competent in ourselves to claim anything for ourselves, but our competence comes from God. 6He has made us competent as ministers of a new covenant—not of the letter but of the Spirit; for the letter kills, but the Spirit gives life.

The Greater Glory of the New Covenant

7Now if the ministry that brought death, which was engraved in letters on stone, came with glory, so that the Israelites could not look steadily at the face of Moses because of its glory, transitory though it was, 8will not the ministry of the Spirit be even more glorious? 9If the ministry that brought condemnation was glorious, how much more glorious is the ministry that brings righteousness! 10For what was glorious has no glory now in comparison with the surpassing glory. 11And if what was transitory came with glory, how much greater is the glory of that which lasts!

12Therefore, since we have such a hope, we are very bold. 13We are not like Moses, who would put a veil over his face to prevent the Israelites from seeing the end of what was passing away. 14But their minds were made dull, for to this day the same veil remains when the old covenant is read. It has not been removed, because only in Christ is it taken away. 15Even to this day when Moses is read, a veil covers their hearts. 16But whenever anyone turns to the Lord, the veil is taken away. 17Now the Lord is the Spirit, and where the Spirit of the Lord is, there is freedom. 18And we all, who with unveiled faces contemplate3:18 Or reflect the Lord’s glory, are being transformed into his image with ever-increasing glory, which comes from the Lord, who is the Spirit.