2 Wafalme 3 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 3:1-27

Moabu Wanaasi

13:1 2Fal 1:17Yehoramu3:1 Yehoramu wakati mwingine limetajwa kama Yoramu. mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili. 23:2 1Fal 16:30; Kut 23:24Akafanya maovu machoni pa Bwana, lakini sio kama baba yake na mama yake walivyokuwa wamefanya. Akaondoa nguzo ya ibada ya Baali ambayo baba yake alikuwa ameitengeneza. 33:3 1Fal 12:30Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha.

43:4 Mwa 19:37; Isa 16:1Basi Mesha mfalme wa Moabu akafuga kondoo, naye akawa ampatie mfalme wa Israeli wana-kondoo 100,000 pamoja na sufu ya kondoo dume 100,000. 53:5 2Fal 1:1Lakini baada ya Ahabu kufa, mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli. 6Kwa hiyo wakati ule Mfalme Yehoramu akaondoka kutoka Samaria na kukusanya Israeli yote tayari kwenda vitani. 73:7 1Fal 22:4Akapeleka pia ujumbe ufuatao kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda: “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?”

Akajibu, “Nitakwenda pamoja nawe. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”

8Akauliza, “Je, tutashambulia kupitia njia gani?”

Akajibu, “Kupitia Jangwa la Edomu.”

93:9 1Fal 22:47Hivyo mfalme wa Israeli akaondoka akiwa pamoja na mfalme wa Yuda na mfalme wa Edomu. Baada ya kuzunguka kwa siku saba, jeshi likawa limeishiwa maji kwa matumizi yao na kwa ajili ya wanyama waliokuwa nao.

10Mfalme wa Israeli akamaka, “Nini! Je, Bwana ametuita sisi wafalme watatu ili tu kututia mikononi mwa Moabu?”

113:11 Mwa 25:22; 1Fal 19:16Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Bwana hapa, ili tuweze kumuuliza Bwana kupitia kwake?”

Afisa mmoja wa mfalme wa Israeli akajibu, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa. Ndiye alikuwa akimimina maji juu ya mikono ya Eliya.”

123:12 Hes 11:17Yehoshafati akasema, “Neno la Bwana liko pamoja naye.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli na Yehoshafati pamoja na mfalme wa Edomu wakamwendea.

13Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina nini mimi nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.”

Mfalme wa Israeli akajibu, “La hasha, kwa sababu ni Bwana ambaye ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”

14Elisha akasema, “Hakika, kama Bwana Mwenye Nguvu Zote aishivyo ambaye ninamtumikia, kama si kuheshimu Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekutazama wala hata kukutupia jicho. 153:15 1Sam 10:5; Eze 1:3Lakini sasa, nileteeni mpiga kinubi.”

Mpiga kinubi alipokuwa akipiga, mkono wa Bwana ukaja juu ya Elisha, 16naye akasema, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Chimbeni bonde hili lijae mahandaki.’ 17Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana: Hamtaona upepo wala mvua, lakini bonde hili litajaa maji, nanyi pamoja na ngʼombe wenu na wanyama wenu wengine mtakunywa. 183:18 Mwa 18:14; Yer 32:17, 27; Mk 10:27Hili ni jambo rahisi machoni pa Bwana. Pia ataitia Moabu mikononi mwenu. 19Mtaushinda kila mji wenye ngome na kila mji mkubwa. Mtakata kila mti ulio mzuri, mtaziba chemchemi zote, na kuharibu kila shamba zuri kwa mawe.”

203:20 Kut 29:41Kesho yake asubuhi, karibu na wakati wa kutoa dhabihu ya asubuhi, tazama, maji yakawa yanatiririka kutoka upande wa Edomu! Nayo nchi ikajaa maji.

21Basi Wamoabu wote walikuwa wamesikia kuwa wale wafalme wamekuja kupigana dhidi yao. Hivyo kila mtu, kijana na mzee, ambaye angeweza kushika silaha akaitwa na kuwekwa mpakani. 22Walipoamka asubuhi na mapema, jua likawa linamulika juu ya maji. Wamoabu waliokuwa upande wa pili wakaona maji ni mekundu, kama damu. 23Wamoabu wakasema, “Ile ni damu! Lazima hao wafalme wamepigana na kuchinjana wao kwa wao. Sasa Moabu, twendeni tukateke nyara!”

24Lakini Wamoabu walipofika kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakainuka na kuwapiga mpaka wakakimbia. Nao Waisraeli wakaivamia nchi na kuwachinja Wamoabu. 253:25 Isa 16:7; Yer 48:31, 36Wakaiharibu miji, kila mtu akatupa jiwe juu ya kila shamba zuri mpaka likafunikwa. Wakaziba chemchemi zote na kukata kila mti mzuri. Kir-Haresethi peke yake ndio uliobaki na mawe yake yakiwa mahali pake. Lakini hata hivyo watu waliokuwa na makombeo wakauzunguka na kuushambulia vilevile.

26Mfalme wa Moabu alipoona kuwa vita vimekuwa vikali dhidi yake, akachukua watu 700 wenye panga ili kuingia kwa mfalme wa Edomu, lakini wakashindwa. 273:27 Za 106:38; Mik 6:7Ndipo akamchukua mwanawe mzaliwa wake wa kwanza, ambaye angekuwa mfalme baada yake, akamtoa kama dhabihu ya kuteketezwa juu ya ukuta wa mji. Ghadhabu ikawa kubwa dhidi ya Israeli; wakajiondoa kwake na kurudi katika nchi yao wenyewe.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪下 3:1-27

以色列与摩押争战

1犹大约沙法执政第十八年,亚哈的儿子约兰撒玛利亚登基做以色列王,执政十二年。 2他做耶和华视为恶的事,不过没有他父母那么败坏,因为他除掉了他父亲立的巴力神柱。 3可是他沉溺于尼八的儿子耶罗波安所犯的罪恶,使以色列人陷入罪中。

4摩押米沙以牧羊为业,每年向以色列王进贡十万只公绵羊的羊毛和十万只羊羔。 5亚哈死后,米沙背叛了以色列王。 6那时,约兰撒玛利亚出发,召集以色列全军。 7他还派人去对犹大约沙法说:“摩押王背叛了我,你肯和我一起去攻打摩押吗?”约沙法回复说:“我肯去。你我不分彼此,我的军队就是你的军队,我的战马就是你的战马。 8我们从哪一条路进攻呢?”约兰答道:“从以东的旷野。”

9于是,以色列王跟犹大王和以东王联合出兵。他们绕道行了七天,军队和随行的牲畜都没有水喝了。 10以色列王叫道:“唉!怎么办呢?耶和华招聚我们三王,是要把我们交给摩押王!” 11约沙法说:“这里有没有耶和华的先知?我们可以托他求问耶和华。”以色列王的一个臣仆答道:“沙法的儿子以利沙在这里,以前他是以利亚的助手。” 12约沙法说:“耶和华会借他说话。”于是以色列王、犹大王和以东王一起去见以利沙

13以利沙以色列王说:“我与你有什么关系?你去问你父母的先知吧!”以色列王说:“不要这样说,耶和华招聚我们三王,是要把我们交给摩押王!” 14以利沙说:“我事奉的是永活的万军之耶和华,我凭祂起誓,若不是看犹大约沙法的情面,我决不理你,也不会见你。 15现在你们给我找一个琴师来。”琴师弹琴的时候,耶和华的灵降在以利沙身上, 16他说:“耶和华吩咐你们要在这山谷中到处挖沟, 17因为耶和华说,‘你们虽不见风,也不见雨,但这谷中必到处有水,人畜都会有水喝。’ 18这对耶和华来说是微不足道的事,祂还要把摩押人交在你们手中。 19你们必攻陷所有的坚城重镇,砍倒各种佳美的树木,堵塞所有水泉,用石头毁坏一切良田。” 20次日早晨,约在献祭的时候,水从以东流来,遍地都是水。

21摩押人听说三王联军进攻他们,于是把凡能打仗的,不论老少都聚集起来,把守在边界上。 22第二天早晨,日光照在水面上,摩押人起来后,看见对面的水像血一样红, 23便说:“那是血啊!一定是三王内讧,自相残杀。弟兄们,我们去抢财物吧!” 24他们到了以色列营,以色列人奋起迎战,杀得他们转身逃跑。以色列人乘胜追击,杀入摩押境内,击杀摩押人, 25摧毁城邑,人人抛掷石头填满所有良田,堵塞一切水泉,砍倒各种佳美树木。摩押境内仅剩的吉珥·哈列设城也遭到甩石的士兵围攻。 26摩押王见战事不利,就率领七百名刀兵,企图从以东王那边突围,但没有成功。 27于是,他在城上将本应继承自己王位的长子杀掉,献为燔祭。以色列人感到非常恐惧3:27 非常恐惧”希伯来文是“大怒”,含“恶心、恐惧”之意。,便退兵回国了。