2 Wafalme 24 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 24:1-20

124:1 Yer 25:1, 9; 2Fal 18:7Wakati wa utawala wa Yehoyakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoyakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza. 224:2 Yer 5:15; Isa 28:18-19; Eze 23:23Bwana akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la Bwana lililosemwa na watumishi wake manabii. 324:3 2Fal 21:12Hakika mambo haya yalitokea Yuda kulingana na agizo la Bwana, ili kuwaondoa kutoka machoni pake kwa sababu ya dhambi za Manase na yote aliyoyafanya, 424:4 2Fal 21:16; Kut 23:21ikiwa ni pamoja na kumwaga damu isiyo na hatia. Kwa kuwa aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyo na hatia, naye Bwana hakuwa radhi kusamehe.

524:5 Yer 22:18-19Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 624:6 Yer 22:19; Eze 19:1Yehoyakimu akalala pamoja na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake.

724:7 Mwa 15:18; Yer 46:25Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati.

Yehoyakini Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 36:9-10)

824:8 1Nya 3:16; Yer 13:18Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu. 924:9 1Fal 15:26Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.

1024:10 2Fal 24:1Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja ili kuishambulia Yerusalemu, nao wakaizunguka kwa jeshi. 11Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi. 1224:12 Yer 24:1Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza.

Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa. 1324:13 2Fal 20:17; Isa 39:6Kama vile Bwana alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la Bwana na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana. 1424:14 Kum 28:36; Ay 5:16Akawachukua watu wa Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi.

1524:15 2Fal 20:18; Mao 2:9Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi. 1624:16 Ezr 2:1Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli mashujaa elfu saba, wenye nguvu na wanaofaa kupigana vita, na watu wenye ustadi na mafundi elfu moja. 1724:17 2Nya 36:11; Yer 37:1Akamfanya Matania, ndugu wa baba yake Yehoyakini, kuwa mfalme mahali pake, na akalibadilisha jina lake kuwa Sedekia.

Sedekia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 36:11-12; Yeremia 52:1-3)

1824:18 Yer 39:1; 2Fal 23:31Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna. 19Alifanya maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Yehoyakimu. 20Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya Bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake.

Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

New International Version

2 Kings 24:1-20

1During Jehoiakim’s reign, Nebuchadnezzar king of Babylon invaded the land, and Jehoiakim became his vassal for three years. But then he turned against Nebuchadnezzar and rebelled. 2The Lord sent Babylonian,24:2 Or Chaldean Aramean, Moabite and Ammonite raiders against him to destroy Judah, in accordance with the word of the Lord proclaimed by his servants the prophets. 3Surely these things happened to Judah according to the Lord’s command, in order to remove them from his presence because of the sins of Manasseh and all he had done, 4including the shedding of innocent blood. For he had filled Jerusalem with innocent blood, and the Lord was not willing to forgive.

5As for the other events of Jehoiakim’s reign, and all he did, are they not written in the book of the annals of the kings of Judah? 6Jehoiakim rested with his ancestors. And Jehoiachin his son succeeded him as king.

7The king of Egypt did not march out from his own country again, because the king of Babylon had taken all his territory, from the Wadi of Egypt to the Euphrates River.

Jehoiachin King of Judah

8Jehoiachin was eighteen years old when he became king, and he reigned in Jerusalem three months. His mother’s name was Nehushta daughter of Elnathan; she was from Jerusalem. 9He did evil in the eyes of the Lord, just as his father had done.

10At that time the officers of Nebuchadnezzar king of Babylon advanced on Jerusalem and laid siege to it, 11and Nebuchadnezzar himself came up to the city while his officers were besieging it. 12Jehoiachin king of Judah, his mother, his attendants, his nobles and his officials all surrendered to him.

In the eighth year of the reign of the king of Babylon, he took Jehoiachin prisoner. 13As the Lord had declared, Nebuchadnezzar removed the treasures from the temple of the Lord and from the royal palace, and cut up the gold articles that Solomon king of Israel had made for the temple of the Lord. 14He carried all Jerusalem into exile: all the officers and fighting men, and all the skilled workers and artisans—a total of ten thousand. Only the poorest people of the land were left.

15Nebuchadnezzar took Jehoiachin captive to Babylon. He also took from Jerusalem to Babylon the king’s mother, his wives, his officials and the prominent people of the land. 16The king of Babylon also deported to Babylon the entire force of seven thousand fighting men, strong and fit for war, and a thousand skilled workers and artisans. 17He made Mattaniah, Jehoiachin’s uncle, king in his place and changed his name to Zedekiah.

Zedekiah King of Judah

18Zedekiah was twenty-one years old when he became king, and he reigned in Jerusalem eleven years. His mother’s name was Hamutal daughter of Jeremiah; she was from Libnah. 19He did evil in the eyes of the Lord, just as Jehoiakim had done. 20It was because of the Lord’s anger that all this happened to Jerusalem and Judah, and in the end he thrust them from his presence.

The Fall of Jerusalem

Now Zedekiah rebelled against the king of Babylon.