2 Wafalme 23 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 23:1-37

Yosia Analifanya Upya Agano

(2 Nyakati 34:3-7, 29-33)

1Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. 223:2 Kum 31:11; Kut 24:7Akapanda kwenda hekaluni mwa Bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la Bwana. 323:3 1Fal 7:15; Kum 13:4Mfalme akasimama karibu na nguzo, na kufanya upya agano mbele za Bwana: yaani kumfuata Bwana na kuzishika amri zake, maagizo na sheria kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, hivyo kuyathibitisha maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika agano.

423:4 2Fal 25:18; Yer 35:4Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani mkuu, makuhani waliomfuata kwa cheo, na mabawabu kuondoa kutoka kwenye Hekalu la Bwana vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali na Ashera na jeshi lote la mianga ya angani! Akavichoma nje ya Yerusalemu katika mashamba ya Bonde la Kidroni, na kuyachukua hayo majivu mpaka Betheli. 523:5 2Fal 16:4; Yer 8:2Akawafukuza makuhani wa kipagani waliokuwa wameteuliwa na wafalme wa Yuda kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Yuda na ile iliyozunguka Yerusalemu, yaani wale waliofukiza uvumba kwa Baali, kwa jua na mwezi, kwa makundi ya nyota, na jeshi lote la angani. 623:6 Kut 32:20; Yer 26:23Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu la Bwana, na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu, akaiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wa kawaida. 723:7 1Fal 14:24; Eze 16:16Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada za miungu, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Bwana na mahali wanawake walipofuma kwa ajili ya Ashera.

823:8 1Fal 15:22Yosia akawaleta makuhani wote wa Bwana kutoka miji yote ya Yuda, na kunajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la Lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji. 923:9 Eze 44:10-14Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu hawakuhudumu katika madhabahu ya Bwana katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.

1023:10 Law 18:21; Isa 30:33Kisha mfalme akanajisi Tofethi, palipokuwa katika Bonde la Ben-Hinomu, ili mtu yeyote asiweze kupatumia kumtoa kafara mwanawe au binti yake katika moto kwa mungu Moleki. 1123:11 Neh 9:34; Kum 4:19Akaondoa kutoka kwenye ingilio la Hekalu la Bwana wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathan-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa jua.

1223:12 2Nya 33:15; Yer 19:13Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la Bwana. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande, na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni. 1323:13 1Fal 11:7; Kum 27:15Mfalme pia akanajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu chukizo la watu wa Amoni. 1423:14 Kut 23:24; Za 53:5Yosia akapasua yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Ashera. Kisha akafunika hayo maeneo kwa mifupa ya wanadamu.

1523:15 1Fal 12:33; Yos 7:2Hata madhabahu yaliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, alibomoa hata hayo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia miungu. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia miungu na kupasaga hadi pakawa vumbi, na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia. 1623:16 1Fal 13:2Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitokea kulingana na neno la Bwana lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.

17Mfalme akauliza, “Lile kaburi lenye mnara wa ukumbusho ninaloliona ni kwa ajili gani?”

Watu wa mji wakasema, “Hii ni alama ya kaburi la mtu wa Mungu aliyekuja kutoka Yuda, naye akanena dhidi ya hii madhabahu ya Betheli mambo yale yale uliyoifanyia leo.”

1823:18 1Fal 13:31Akasema, “Liacheni, msiliguse. Msimruhusu mtu yeyote kuiondoa mifupa yake.” Basi wakaiacha mifupa yake pamoja na ile ya yule nabii ambaye alikuwa amekuja kutoka Samaria.

19Kama alivyokuwa amefanya huko Betheli, Yosia akabomoa na kunajisi mahali pa kuabudia miungu kwenye mahali pa juu ambapo wafalme wa Israeli walikuwa wamejenga ndani ya miji ya Samaria, ambayo ilikuwa imemghadhibisha Bwana. 2023:20 2Fal 11:18; Kut 22:20Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika madhabahu zao wenyewe, na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.

Yosia Aadhimisha Pasaka

2123:21 Kut 12:11Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwa Bwana Mungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano.” 22Hapakuwahi kuwepo na adhimisho lingine la Pasaka kama hilo tangu nyakati za Waamuzi walioongoza Israeli, wala katika nyakati zote za wafalme wa Israeli na wafalme wa Yuda. 2323:23 Hes 28:16Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia, Pasaka hii iliadhimishwa kwa Bwana huko Yerusalemu.

2423:24 Kum 18:11; Mwa 31:19Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa waaguzi, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa, na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana huko Yuda na Yerusalemu. Aliyafanya haya ili kutimiza matakwa ya sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikipata ndani ya Hekalu la Bwana. 2523:25 1Sam 7:3Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine yeyote ambaye alimpenda Bwana kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Mose.

2623:26 2Fal 21:12Hata hivyo, Bwana hakuacha ghadhabu yake iliyowaka dhidi ya Yuda kwa sababu ya yale yote ambayo Manase alikuwa amefanya kumghadhibisha. 2723:27 Kut 33:15; Yer 27:10Hivyo Bwana akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua, na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Jina langu litakaa humo.’ ”

28Matukio mengine ya utawala wa Yosia na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?

2923:29 Yer 46:2; 2Fal 9:27Yosia alipokuwa mfalme, Farao Neko mfalme wa Misri akapanda mpaka Mto Frati kumsaidia mfalme wa Ashuru. Mfalme Yosia akatoka kwenda kupigana naye, lakini Neko akamkabili na kumuua huko Megido. 3023:30 2Fal 9:28Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.

Yehoahazi Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 36:2-4)

3123:31 1Nya 3:15; Yer 22:11Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna. 3223:32 1Fal 15:26Akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyofanya. 3323:33 Hes 34:11; 1Fal 8:65Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja23:33 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.4. za fedha, na talanta moja ya dhahabu23:33 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. katika Yuda. 3423:34 2Nya 36:5-8; Yer 22:12Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, na kulibadilisha jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua Yehoahazi na kumpeleka Misri, naye akafia huko.

Yehoyakimu Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 36:5-8)

35Yehoyakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoyakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadrio ya mapato yao.

36Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Zebida binti Pedaya kutoka Ruma. 37Naye akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyokuwa wamefanya.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀下 23:1-37

約西亞的改革

1於是,王召集猶大耶路撒冷的所有長老, 2與祭司、先知、猶大人、耶路撒冷的居民等全體民眾,不論貴賤,一同上到耶和華的殿。王把在殿中發現的約書唸給他們聽。 3王站在柱旁,在耶和華面前立約,要全心全意地跟隨耶和華,遵從祂的一切誡命、法度和律例,履行約書上的規定。民眾都答應守約。

4王吩咐大祭司希勒迦及其副手和殿門守衛清除耶和華殿裡用來祭拜巴力亞舍拉及天上萬象的一切器具,將其搬到耶路撒冷城外汲淪溪旁的田野燒掉,又把灰燼帶到伯特利5從前,猶大各王任命祭司在猶大各城和耶路撒冷周圍的邱壇燒香。現在,約西亞除掉那些祭司,又除掉向巴力、日、月、星辰及天上萬象燒香的祭司。 6他將亞舍拉神像從耶和華的殿裡搬到耶路撒冷城外汲淪溪旁燒掉,磨成灰撒在平民的墳墓上。 7他又拆毀耶和華的殿內男廟妓的房屋,就是婦女為亞舍拉編織帳幔的地方。 8他召集猶大各城中的祭司,污瀆從迦巴別示巴的各邱壇,那些祭司曾在那裡燒香。他拆毀耶路撒冷城門左邊、約書亞總督門前的邱壇。 9但在邱壇燒香的祭司不能在耶路撒冷耶和華的祭壇那裡事奉,只可以和其他祭司一起吃無酵餅。 10他污瀆欣嫩子谷中的陀斐特,使人們不能焚燒自己的兒女獻給摩洛11他從耶和華的殿門口除掉猶大各王獻給太陽神的馬匹,這些馬匹在太監拿單·米勒房子旁邊的院子裡。他燒掉了那些獻給太陽神的戰車。 12他推倒猶大各王在亞哈斯樓頂上建造的祭壇,摧毀瑪拿西在耶和華殿的兩個院子裡所築的祭壇,把它們打碎,把灰丟進汲淪溪。 13他污瀆耶路撒冷東面、敗壞山南面的邱壇。這些邱壇都是以色列所羅門西頓人可憎的神明亞斯她錄摩押人可憎的神明基抹亞捫人可憎的神明米勒公建造的。 14他砸碎神柱,砍倒亞舍拉神像,用死人骨頭填滿那些地方。

15他拆掉伯特利高崗上的祭壇,即尼八的兒子耶羅波安誘使以色列人犯罪時建造的祭壇,把祭壇燒毀,搗碎成灰,又焚燒亞舍拉神像。 16約西亞轉身看見山上的墳墓,就派人取出墓中的屍骨,放在那祭壇上焚燒,污瀆了那祭壇,應驗了耶和華藉祂的僕人所說的預言。 17約西亞問:「我看到的那墓碑是誰的?」那城裡的人告訴他:「是上帝僕人的,他曾從猶大來預言你對伯特利祭壇所做的這些事。」 18他說:「不要動他,不要動他的屍骨。」於是,他們沒有動那位先知和撒瑪利亞來的先知的屍骨。 19他拆毀以色列各王從前建在撒瑪利亞各城高崗上、惹耶和華發怒的邱壇,就像他在伯特利所做的一樣。 20他在祭壇上殺死那些邱壇的祭司,又在壇上焚燒死人骨頭。之後,他返回耶路撒冷

約西亞守逾越節

21約西亞王吩咐民眾:「你們應當依照約書的記載慶祝逾越節,以尊崇你們的上帝耶和華。」 22-23約西亞執政第十八年,他們在耶路撒冷慶祝逾越節,以尊崇耶和華。自士師治理以色列起,至以色列猶大列王統治期間,都沒有這樣慶祝過逾越節。

24為了遵守祭司希勒迦在耶和華殿裡找到的律法書上的話,約西亞徹底清除了耶路撒冷猶大境內的靈媒、巫師、家庭神像及其他一切可憎之物。 25約西亞全心、全意、全力歸向耶和華,遵行摩西的一切律法,在猶大列王中空前絕後。

26然而,瑪拿西所行的一切惹怒耶和華,耶和華對猶大仍盛怒未息。 27耶和華說:「我要像驅逐以色列人一樣將猶大人從我面前趕走。我要撇棄我所揀選的耶路撒冷和我名常在的殿。」

28約西亞其他的事及作為都記在猶大的列王史上。 29約西亞執政期間,埃及尼哥前往幼發拉底河援助亞述王,約西亞出兵迎戰尼哥,在米吉多被殺。 30他的臣僕用車把他的屍體從米吉多運回耶路撒冷,安葬在他的墓穴裡。民眾膏立他兒子約哈斯做王。

約哈斯做猶大王

31約哈斯二十三歲登基,在耶路撒冷執政三個月。他母親叫哈慕她,是立拿耶利米的女兒。 32約哈斯像他祖先一樣做耶和華視為惡的事。 33埃及尼哥約哈斯囚禁在哈馬利比拉,不准他在耶路撒冷做王,又罰猶大國三點四噸銀子和三十四公斤金子。

約雅敬做猶大王

34埃及尼哥約西亞的另一個兒子以利亞敬為王,給他改名為約雅敬約哈斯尼哥帶到埃及,並死在那裡。 35為了繳納法老索要的金銀,約雅敬向全國徵稅,按照民眾家產的多少徵收金銀。 36約雅敬二十五歲登基,在耶路撒冷執政十一年。他母親叫西布妲,是魯瑪毗大雅的女兒。 37他像他祖先一樣做耶和華視為惡的事。