2 Wafalme 18 – NEN & NRT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 18:1-37

Hezekia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 29:1–31:21)

118:1 Hos 1:1; Mik 1:1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi mfalme wa Yuda alianza kutawala. 218:2 Isa 38:5Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 318:3 1Fal 14:8; Isa 38:5Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Daudi baba yake alivyofanya. 418:4 2Nya 31:1; Hes 21:9Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (ilikuwa ikiitwa Nehushtani18:4 Nehushtani maana yake Kipande cha shaba.).

518:5 2Fal 19:10; Mit 3:26Hezekia aliweka tumaini lake kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Hapakuwepo na mfalme mwingine wa kufanana naye miongoni mwa wafalme wa Yuda, kabla yake au baada yake. 618:6 Kum 6:18Alishikamana na Bwana kwa bidii wala hakuacha kumfuata; alishika amri ambazo Bwana alikuwa amempa Mose. 718:7 Mwa 39:3; Ezr 4:19Naye Bwana alikuwa pamoja naye, akafanikiwa katika kila alichokifanya. Aliasi dhidi ya mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia. 818:8 2Fal 17:9Kuanzia mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, aliwashinda Wafilisti, hadi kufikia Gaza na himaya yake yote.

918:9 Isa 1:1Mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela kutawala Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru alikwenda kuishambulia Samaria na kuuzunguka kwa majeshi. 10Baada ya miaka mitatu Waashuru wakautwaa. Kwa hiyo Samaria ulitekwa katika mwaka wa sita wa utawala wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa utawala wa Hoshea mfalme wa Israeli. 1118:11 Isa 37:12; Eze 16:39Mfalme wa Ashuru akawahamishia Waisraeli huko Ashuru na akawaweka Hala, na Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi. 1218:12 Dan 9:6, 10; 1Fal 9:6Hili lilitokea kwa sababu hawakumtii Bwana Mungu wao, lakini walikuwa wamevunja agano lake, yale yote ambayo Mose mtumishi wa Bwana aliwaamuru. Hawakuzisikiliza amri wala kuzitimiza.

13Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka. 1418:14 2Fal 19:8; Isa 24:5Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa chochote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta 30018:14 Talanta 300 za fedha ni sawa na tani 10. za fedha, na talanta thelathini18:14 Talanta 30 za dhahabu ni sawa na tani moja. za dhahabu. 1518:15 1Fal 15:18; Isa 39:2Basi Hezekia akampa fedha yote iliyopatikana ndani ya Hekalu la Bwana na katika hazina ya jumba la mfalme.

16Wakati huu Hezekia mfalme wa Yuda akabandua dhahabu yote iliyokuwa imefunika milango na miimo ya Hekalu la Bwana, akampa mfalme wa Ashuru.

Senakeribu Anaitishia Yerusalemu

(2 Nyakati 32:1-19; Isaya 36:1-22)

1718:17 2Fal 20:20; Isa 20:1Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi, pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja Yerusalemu na kusimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi. 1818:18 2Fal 19:2; Isa 22:20Wakaagiza mfalme aitwe. Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la mfalme, Shebna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakawaendea.

1918:19 Ay 4:6Yule jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia:

“ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi unapoweka hili tumaini lako? 20Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata ukaniasi mimi? 2118:21 Eze 29:6; Isa 30:5, 7Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea. 22Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia Bwana Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya katika Yerusalemu”?

23“ ‘Njooni sasa, fanyeni mapatano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha waendesha farasi juu yao! 2418:24 Isa 10:8Utawezaje kumzuia hata afisa mmoja aliye mdogo kati ya maafisa wa bwana wangu, ijapo unategemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi? 2518:25 2Fal 19:29Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza mahali hapa pasipo neno kutoka kwa Bwana? Bwana mwenyewe ndiye aliniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ”

2618:26 Ezr 4:7Ndipo Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”

27Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?”

28Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, akasema: “Sikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru! 2918:29 2Fal 19:10Hili ndilo asemalo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa mkononi mwangu. 30Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini Bwana kwa kuwaambia, ‘Hakika Bwana atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

3118:31 Hes 13:23; Yer 14:3“Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwa mzabibu wake na mtini wake mwenyewe, na kunywa maji kutoka kisima chake mwenyewe, 3218:32 Kum 30:19mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima, sio mauti!

“Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha asemapo, ‘Bwana atatuokoa.’ 3318:33 2Fal 19:12Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru? 3418:34 2Fal 17:24; Isa 10:9Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena na Iva? Je, imeokoa Samaria kutoka mkononi mwangu? 3518:35 Za 2:1-2Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Bwana aiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?”

36Lakini wale watu wakakaa kimya, wala hawakujibu lolote, kwa kuwa mfalme alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lolote.”

3718:37 Isa 33:7; 2Fal 6:30Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.

New Russian Translation

4 Царств 18:1-37

Езекия – царь Иудеи

(2 Пар. 29:1-2; 31:1, 20-21)

1На третьем году правления царя Израиля Осии, сына Элы, в Иудее начал царствовать Езекия, сын Ахаза. 2Ему было двадцать пять лет, когда он стал царем, и правил он в Иерусалиме двадцать девять лет. Его мать звали Ави18:2 Вариант имени Авия., она была дочерью Захарии. 3Он делал то, что было правильным в глазах Господа, как и его предок Давид. 4Он убрал святилища на возвышенностях, разбил священные камни и срубил столбы Ашеры. Он разломал на куски бронзового змея, которого сделал Моисей, потому что до того самого времени израильтяне возжигали перед ним благовония. Он назывался Нехуштан18:4 По-еврейски это название означает «медный змей». См. Чис. 21:4-9..

5Езекия доверял Господу, Богу Израиля. Не было подобного ему среди всех царей Иудеи ни до него, ни после него. 6Он крепко держался Господа и неотступно следовал за Ним; он исполнял повеления, которые Господь дал через Моисея. 7И Господь был с ним: он преуспевал во всем, за что бы ни брался. Он восстал против царя Ассирии и отказался ему служить. 8Он бил филистимлян до самого города Газы и ее окрестностей, от сторожевой башни до укрепленного города.

Ассирийцы захватывают Самарию

(4 Цар. 17:5-7)

9На четвертом году правления царя Езекии – седьмом году правления Осии, сына Элы, царя Израиля, – Салманассар, царь Ассирии, двинулся на Самарию и осадил ее. 10Через три года ассирийцы взяли ее. Так на шестом году правления Езекии – девятом году правления Осии, царя Израиля, – была взята Самария. 11Царь Ассирии увел Израиль в плен в свою страну и поселил их в Халахе, в Гозане, что на реке Хаворе, и в городах мидян. 12Это произошло потому, что они не слушали Господа, своего Бога, но нарушили Его завет – все, что повелел Моисей, слуга Господа. Они и не слушали, и не исполняли.

Синаххериб угрожает Иерусалиму

(2 Пар. 32:1-19; Ис. 36:1-22)

13На четырнадцатом году правления царя Езекии18:13 В 701 г. до н. э. Синаххериб18:13 Синаххериб был сыном и преемником Саргона II. Он правил с 705 по 681 гг. до н. э., царь Ассирии, напал на все укрепленные города Иудеи и захватил их. 14Езекия, царь Иудеи, послал в город Лахиш сказать царю Ассирии:

– Я виновен. Оставь меня, и я заплачу тебе все, что ты от меня потребуешь.

Царь Ассирии взыскал с Езекии, царя Иудеи, триста талантов18:14 Около 10 т. серебра и тридцать талантов18:14 Около 1 т. золота. 15Езекия отдал ему все серебро, какое нашлось в доме Господа и в сокровищницах царского дворца. 16Тогда же Езекия, царь Иудеи, ободрал все золото, которым покрыл двери и дверные косяки храма Господа, и отдал его царю Ассирии.

17Но, тем не менее, царь Ассирии послал из Лахиша к царю Езекии в Иерусалим верховного военачальника, начальника придворных и главного виночерпия18:17 Главный виночерпий был одним из самых важных лиц при дворе, которому царь доверял свою жизнь. с большим войском. Они подошли к Иерусалиму и остановились у водопровода Верхнего пруда, на дороге к Сукновальному полю. 18Они позвали царя, и к ним вышли распорядитель дворца, Элиаким, сын Хелкии, писарь Шевна и летописец Иоах, сын Асафа.

19Главный виночерпий сказал им:

– Скажите Езекии: «Так говорит великий царь, царь Ассирии: „Откуда у тебя эта уверенность? 20Ты думаешь, что пустые слова – то же самое, что военное искусство и сила? На кого же ты надеешься, что восстал против меня? 21Вот, ты надеешься на Египет, эту надломленную трость, которая пронзит ладонь всякому, кто на нее обопрется! Фараон, царь Египта, таков со всеми, кто на него надеется. 22А если вы скажете мне: «Мы надеемся на Господа, нашего Бога», то не Его ли святилища на возвышенностях и жертвенники убрал Езекия, сказав Иудее и Иерусалиму: «Поклоняйтесь только перед этим жертвенником, что в Иерусалиме»?“

23Итак, заключи сделку с господином моим, царем Ассирии: я дам тебе две тысячи коней, только найдешь ли ты для них всадников? 24Как ты сможешь отразить хотя бы наименьшего начальника из слуг господина моего, даже надеясь на египетские колесницы и всадников?18:24 Или: «колесничих». 25Да и разве не по воле Господа я двинулся на это место, чтобы уничтожить его? Господь Сам сказал мне пойти на эту страну и уничтожить ее».

26Тогда Элиаким, сын Хелкии, Шевна и Иоах сказали главному виночерпию:

– Пожалуйста, говори с твоими слугами по-арамейски, ведь мы понимаем этот язык. Не говори с нами по-еврейски при народе, что на стене.

27Но главный виночерпий ответил:

– Разве мой господин послал меня сказать это только вашему господину и вам, а не людям, находящимся на стене, которые, как и вы сами, будут есть свой кал и пить свою мочу?

28Главный виночерпий встал и громко закричал по-еврейски:

– Слушайте слово великого царя, царя Ассирии! 29Так говорит царь: «Не давайте Езекии обманывать вас. Он не может избавить вас от моей руки. 30Не давайте Езекии убедить вас положиться на Господа, когда он говорит: „Господь непременно спасет нас; этот город не будет отдан в руки царя Ассирии“. 31Не слушайте Езекию».

Так говорит царь Ассирии: «Заключите со мной мир и выходите ко мне. Тогда все вы будете есть со своей лозы и инжирных деревьев и пить воду из своего колодца, 32пока я не приду и не возьму вас в страну, такую же, как ваша, в страну зерна и вина, страну хлеба и виноградников, страну оливковых деревьев и меда. Выберите жизнь, а не смерть! Не слушайте Езекию, потому что он сбивает вас с толку, говоря: „Господь спасет нас“. 33Разве какой-либо бог другого народа избавил свою страну от руки царя Ассирии? 34Где боги Хамата и Арпада? Где боги Сепарваима, Ены и Иввы? Разве кто-нибудь избавил от моей руки Самарию? 35Кто из богов всех этих стран смог избавить от меня свою страну? Как же Господь сможет избавить от моей руки Иерусалим?»

36Но народ молчал и не говорил в ответ ничего, потому что царь приказал: «Не отвечайте ему».

37И распорядитель дворца Элиаким, сын Хелкии, писарь Шевна и летописец Иоах, сын Асафа, пришли к Езекии в разорванных одеждах и передали ему то, что сказал главный виночерпий.