2 Timotheo 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Timotheo 2:1-26

Askari Mwema Wa Kristo Yesu

12:1 Efe 6:10; 1Tim 1:2; 2Tim 1:18Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu. 2Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile. 3Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4Hakuna askari yeyote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari. 52:5 1Kor 9:25; 2Tim 4:8; 1Kor 9:10Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano. 6Mkulima mwenye bidii ya kazi ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata fungu la mavuno. 7Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo hayo yote.

82:8 Mdo 2:24; Rum 2:16Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, yeye aliye wa uzao wa Daudi. Hii ndiyo Injili yangu, 92:9 Mdo 9:16; 2Tim 1:12ambayo kwayo ninateseka hata kufikia hatua ya kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi. 102:10 Kol 1:24; 2Kor 4:17Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.

112:11 Rum 6:2-11; 1Tim 1:15; 2Kor 4:10Hili ni neno la kuaminiwa:

Kwa maana kama tumekufa pamoja naye,

tutaishi pia pamoja naye.

122:12 Rum 8:17; 1Pet 4:13; Mt 10:33Kama tukistahimili,

pia tutatawala pamoja naye.

Kama tukimkana yeye,

naye atatukana sisi.

132:13 Hes 23:19; 1Kor 1:9Kama tusipoamini,

yeye hudumu kuwa mwaminifu,

kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

Mfanyakazi Aliyekubaliwa Na Mungu

142:14 1Tim 5:21; 6:13; 2Tim 4:1; 1Tim 1:4; 6:4; Tit 3:9, 11Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia. 152:15 Kol 1:5; Yak 1:18Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli. 162:16 Tit 3:9; 1Tim 4:7; 6:20Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu. 172:17 1Tim 1:20Mafundisho yao yataenea kama kidonda kisichopona. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto 182:18 1Tim 6:21; 1Kor 15:12ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kuwako, nao huharibu imani ya baadhi ya watu. 192:19 Isa 28:16; Hes 16:5Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana, na auache uovu.”

202:20 1Tim 3:15; Rum 9:21Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida. 212:21 2Kor 9:8Basi ikiwa mtu amejitakasa na kujitenga na hayo niliyoyataja, atakuwa chombo maalum, kilichotengwa na ambacho kinamfaa mwenye nyumba, kimeandaliwa tayari kwa kila kazi njema.

222:22 1Tim 6:11; 5:14Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 232:23 1Tim 1:4; 4:7; 6:4; 2Tim 2:16; Tit 3:9; 2Tim 2:14Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi. 242:24 1Tim 3:2-9; Tit 3:2; 1:9Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu. 252:25 1Tim 2:4; Gal 6:1; 1Tim 6:11; 1Pet 3:12; Mdo 8:22; 1Tim 2:4Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, 262:26 1Tim 3:7ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

提摩太后书 2:1-26

基督的精兵

1我儿啊!你要靠着基督耶稣的恩典刚强起来。 2以前你在许多见证人面前听过我的教导,你要把这些教导传给忠信可靠、能够教导他人的人。

3你要做基督耶稣的精兵与我同受苦难。 4当兵的若让其他事务缠身,就不能取悦征召他的上司。 5同样,参加比赛的人若不遵守比赛规则,就不可能得奖。 6辛劳的农夫理当先享受收成。 7你要思想我说的话,因为主必赐你悟性明白各样的事。

8你要切记我所传的福音:耶稣基督是大卫的后裔,祂从死里复活了。 9我为这福音受苦,甚至像犯人一样被囚禁,但上帝的道是囚禁不住的。 10我为了上帝所拣选的人忍受一切痛苦,使他们可以获得在基督耶稣里的救恩和永远的荣耀。 11有真实可信的话说:

“我们若与基督同死,

就必与祂同活。

12我们若忍耐到底,

就必与祂一同做王。

我们若不承认祂,

祂也必不承认我们。

13我们纵然会失信,

祂仍然信实可靠,

因为祂不能违背自己。”

做无愧的工人

14你要提醒众人这些事,在主面前嘱咐他们:不要为言词争辩,因为那对听见的人有害无益。 15你应当竭力在上帝面前做经得起考验、问心无愧的工人,正确地阐释真理之道。 16要远避一切世俗的空谈,因为好空谈的人只会越来越不敬虔。 17他们讲的话像毒疮,只会越烂越大,许米乃腓理徒就是例子。 18他们离经背道,说复活的事已成过去,动摇了许多人的信心。 19然而,上帝所立的坚实根基永不动摇,这根基上刻着:“主认识谁是属于祂的人”,“凡自称是属于主的人都要离弃罪恶。”

20大户人家不但有金器银器,也有木器瓦器,这些器皿的用途有贵贱之分。 21人若洁身自爱,远离卑贱的事,就必成为圣洁无瑕的贵重器皿,可以被主用来成就各样的善事。

22你要逃避年轻人的邪情私欲,要跟那些以清洁的心求告主的人一同追求公义、信心、仁爱、和平。 23不要参与愚昧无知的辩论,因为这些事只会引起纷争。 24上帝的奴仆不可与人争执,总要温和待人,善于教导,心存忍耐。 25要温柔地规劝那些反对我们的人,也许上帝会赐给他们悔改的心,使他们明白真理, 26让他们这些被魔鬼掳去、受其摆布的人能够醒悟过来,脱离魔鬼的网罗。