2 Samweli 9 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 9:1-13

Daudi Na Mefiboshethi

19:1 1Sam 20:14-17, 42; 23:18; 18:3; Mit 27:10Daudi akauliza, “Je, hakuna mtu hata mmoja wa nyumba ya Sauli aliyebaki ambaye naweza kumtendea wema kwa ajili ya Yonathani?”

29:2 2Sam 16:1-4; 19:17, 26-29Basi palikuwepo mtumishi wa nyumba ya Sauli aliyeitwa Siba. Wakamwita aje mbele ya Daudi, naye mfalme akamwambia, “Wewe ndiwe Siba?”

Akamjibu, “Naam, mimi ndiye mtumishi wako.”

39:3 1Nya 8:34; Law 21:18; 1Sam 20:14; 2Sam 4:4; Kum 19:15; Mt 5:44; Lk 6:36; Tit 3:3-4Mfalme akauliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonyesha wema wa Mungu?”

Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani, yeye ni kiwete miguu yote.”

49:4 2Sam 17:27-29Mfalme akauliza, “Yuko wapi?”

Siba akajibu, “Yuko nyumbani kwa Makiri mwana wa Amieli huko Lo-Debari.”

5Basi Mfalme Daudi akamtaka aletwe kutoka Lo-Debari, kutoka nyumbani kwa Makiri mwana wa Amieli.

69:6 Mwa 37:7; 2Sam 16:4Mefiboshethi mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, alipofika kwa Daudi, akainama kumpa mfalme heshima.

Daudi akamwita, “Mefiboshethi!”

Mefiboshethi akajibu, “Ndimi mtumishi wako.”

79:7 1Sam 20:14-15; 2Sam 19:28; 21:7; 1Fal 2:7; 2Fal 25:29; Yer 52:33; Mwa 43:18; 50:21; 1Sam 12:19-24; Yer 52:33Daudi akamwambia, “Usiogope, kwa maana hakika nitakutendea wema kwa ajili ya baba yako Yonathani. Nitakurudishia ardhi yote iliyokuwa mali ya Sauli baba yako, nawe daima utakula chakula mezani pangu.”

89:8 2Sam 4:4; 3:8; 1Sam 24:14; 2Sam 16:9Mefiboshethi akasujudu akasema, “Mimi mtumishi wako ni nini hata uangalie mbwa mfu kama mimi?”

99:9 Isa 32:8Ndipo mfalme akamwita Siba mtumishi wa Sauli na kumwambia, “Nimempa mwana wa bwana wako kila kitu kilichokuwa mali ya Sauli na jamaa yake. 109:10 2Sam 16:3; 19:28Wewe, wanao na watumishi wako mtamlimia mashamba Mefiboshethi na kumletea mavuno, ili kwamba mwana wa bwana wako apate mahitaji yake. Naye Mefiboshethi mwana wa bwana wako atakula chakula mezani pangu daima.” (Siba alikuwa na wana kumi na watano, na watumishi ishirini.)

119:11 Ay 36:7; Za 113:8; 1Sam 16:1-4; Mit 12:17Ndipo Siba akamwambia mfalme, “Mtumishi wako atafanya chochote bwana wangu mfalme atakachoagiza mtumishi wake kufanya.” Basi Mefiboshethi akala chakula mezani pa Daudi kama mmoja wa wana wa mfalme.

129:12 2Sam 4:4; 1Nya 8:34Mefiboshethi alikuwa na mwanawe mdogo aliyeitwa Mika, nao watu wote wa nyumba ya Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi. 139:13 2Sam 19:33-36; 2Fal 25:29; Yer 52:33-34Naye Mefiboshethi akaishi huko Yerusalemu, kwa sababu daima alikula mezani pa mfalme, naye alikuwa kiwete miguu yote.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 9:1-13

大卫恩待米非波设

1大卫问:“扫罗一家还有什么人吗?我要因为和约拿单的情义而恩待他。” 2有人就去叫扫罗家一个名叫洗巴的仆人来见大卫,王问他:“你就是洗巴吗?”他说:“仆人正是洗巴。” 3王说:“扫罗家中还有什么人?我要以上帝的慈爱来待他。”洗巴答道:“约拿单还有一个儿子,是双脚残废的。” 4王说:“他在哪里?”洗巴答道:“他住在罗·底巴,在亚米利的儿子玛吉家里。” 5于是,大卫王派人去罗·底巴把他从亚米利的儿子玛吉家里接来。 6扫罗的孙子、约拿单的儿子米非波设来到大卫面前,向他俯伏叩拜。大卫说:“米非波设!”米非波设答道:“仆人在这里。” 7大卫说:“你不用害怕,我要因为和你父亲约拿单的情义而恩待你。我要把你祖父扫罗所有的田地归还给你,你要常与我同席吃饭。” 8米非波设再次叩拜,说:“仆人算什么?不过像一条死狗罢了,你竟这样眷顾我!”

9王又把扫罗的仆人洗巴召来,对他说:“我已把扫罗全家的产业都赐给了你主人的孙子米非波设10你和你的儿子及仆人要为米非波设种田,把出产拿来供养他。他还要常常与我同席吃饭。”洗巴有十五个儿子,二十个仆人。 11洗巴对王说:“仆人必遵行我主我王的一切吩咐。”于是,米非波设像王子一样常与大卫同席吃饭。 12米非波设有一个小儿子名叫米迦洗巴家中的人都做了米非波设的仆人。 13从此,双脚残废的米非波设就住在耶路撒冷,常常与王同席吃饭。