2 Samweli 3 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 3:1-39

13:1 1Fal 14:30; 2Sam 5:12; 2:17; 22:44; Es 9:4; Za 46:9; Isa 2:4; Mik 4:3; Mt 10:35-36; Gal 5:17; Efe 6:12Vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi vilidumu kwa muda mrefu. Daudi akaendelea kuwa imara zaidi na zaidi, wakati nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika zaidi na zaidi.

23:2 2Sam 13:1; 1Sam 25:43; 1Nya 3:1-3Wana walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni:

Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni mwana wa Ahinoamu wa Yezreeli;

33:3 1Sam 25:42; 2Sam 13:1, 28, 37; 14:32; 15:8mzaliwa wake wa pili alikuwa Danieli3:3 Jina lingine lake ni Kileabu. mwana wa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli;

wa tatu, Absalomu mwana wa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

43:4 1Fal 1:5-11; 2:13, 22wa nne, Adoniya mwana wa Hagithi;

wa tano, Shefatia mwana wa Abitali;

5wa sita, Ithreamu mwana wa Egla, mkewe Daudi.

Hawa ndio waliozaliwa kwa Daudi huko Hebroni.

Abneri Anamwendea Daudi

63:6 1Sam 14:50; 2Sam 2:8-9; 2Nya 25:8Wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri alikuwa anajiimarisha katika nafasi yake kwenye nyumba ya Sauli. 73:7 Mwa 22:24; 2Sam 16:21-22; 1Fal 1:3; 2Sam 21:8-11Basi Sauli alikuwa amekuwa na suria, jina lake Rispa binti wa Aiya. Naye Ish-Boshethi akamwambia Abneri, “Kwa nini umekutana kimwili na suria wa baba yangu?”

83:8 1Sam 17:43; 2Sam 9:8; 16:9; 8; 13; 1Sam 24:14; Kut 23:18Abneri akakasirika sana kwa sababu ya kile Ish-Boshethi alichosema, naye akamjibu, “Je, mimi ni kichwa cha mbwa, kwa upande wa Yuda? Siku hii ya leo mimi ni mtiifu kwa nyumba ya baba yako Sauli, kwa jamaa yake na rafiki zake. Sijakukabidhi kwa Daudi, lakini bado unanilaumu kwa kosa la kuhusika na huyu mwanamke! 93:9 1Sam 15:28; Rut 1:17; 1Fal 19:2; 1Sam 16:12; 1Nya 12:23; Za 78:70; 89:19-20; Mdo 13:22Mungu na amshughulikie Abneri, tena kwa ukali, ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile Bwana alichomwahidi kwa kiapo, 103:10 Amu 20:1; 1Sam 25:28-31; 2Sam 24:2; 17:11; 1Fal 4:25na kuuhamisha ufalme kutoka kwenye nyumba ya Sauli na kuimarisha kiti cha ufalme cha Daudi juu ya Israeli na Yuda kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba.” 11Ish-Boshethi hakuthubutu kusema neno jingine kwa Abneri, kwa sababu alimwogopa Abneri.

12Ndipo Abneri akatuma wajumbe kwa niaba yake kwa Daudi, kumwambia, “Nchi hii ni ya nani? Fanya mapatano na mimi, nami nitakusaidia kuiweka Israeli yote juu yako.”

133:13 Mwa 43:5; 1Sam 18:20; Mwa 44:23-26Daudi akasema, “Vyema, nitafanya mapatano nawe. Lakini nahitaji jambo moja kwako: Usije mbele yangu mpaka umemleta Mikali binti Sauli wakati utakapokuja kuniona.” 143:14 1Sam 18:27Kisha Daudi akapeleka wajumbe kwa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, kudai, “Nipe Mikali mke wangu, ambaye nilimposa mwenyewe kwa mahari ya magovi 100 ya Wafilisti.”

153:15 Kum 24:1-4; 1Sam 25:44Kwa hiyo Ish-Boshethi akatoa amri kwamba Mikali achukuliwe kutoka kwa Paltieli mumewe, mwana wa Laishi. 163:16 2Sam 16:5; 17:18; 19:16Hata hivyo, mumewe alikwenda pamoja naye, akilia nyuma ya mkewe njia yote hadi Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani!” Kwa hiyo akarudi.

173:17 Amu 11:11Abneri akafanya shauri pamoja na wazee wa Israeli, akasema, “Muda mrefu mmetaka kumfanya Daudi mfalme wenu. 183:18 1Sam 9:16; 2Sam 8:6; 1Sam 15:28Sasa fanyeni hivyo! Kwa maana Bwana alimwahidi Daudi akisema, ‘Kwa kupitia Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka mikononi mwa Wafilisti na kutoka mikononi mwa adui zako wote.’ ”

193:19 1Nya 12:2, 16, 29; 1Sam 10:20-21Pia Abneri mwenyewe akazungumza na kabila la Benyamini. Kisha akaenda mpaka Hebroni kumwambia Daudi kila kitu ambacho Israeli na nyumba yote ya Benyamini walichotaka kufanya. 203:20 1Nya 12:29Wakati Abneri aliyekuwa na watu ishirini pamoja naye, alipokuja kwa Daudi huko Hebroni, Daudi akamwandalia karamu pamoja na watu wake. 213:21 2Sam 5:3; 1Fal 11:37; Kum 14:26; Za 20:4Ndipo Abneri akamwambia Daudi, “Niache niende mara moja nikakusanye Israeli yote kwa ajili ya mfalme bwana wangu, ili waweze kufanya mapatano na wewe, ili kwamba uweze kutawala juu ya yote yale ambayo moyo wako unaonea shauku.” Basi Daudi akamuaga Abneri, naye akaenda kwa amani.

Yoabu Amuua Abneri

22Wakati huo huo, watu wa Daudi na Yoabu walirudi kutoka kwenye kushambulia, nao wakarudi na nyara nyingi mno. Lakini Abneri hakuwa tena pamoja na Daudi huko Hebroni, kwa sababu Daudi alikuwa amemruhusu aende zake, naye akaenda kwa amani. 23Yoabu na askari wote aliokuwa nao walipowasili, aliambiwa kwamba Abneri mwana wa Neri alikuwa amekuja kwa mfalme na kwamba mfalme alikuwa amemruhusu aende zake, na kwamba alikwisha ondoka kwa amani.

24Basi Yoabu alikwenda kwa mfalme na kumwambia, “Ni nini hiki ulichofanya? Tazama, Abneri alikuja kwako. Kwa nini ukamwacha aende? Sasa amekwenda! 253:25 Hes 27:17; Kum 28:6; 1Sam 29:6; Za 121:8; Isa 37:28Wajua Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kuchunguza nyendo zako na kupata kila kitu unachokifanya.”

26Ndipo Yoabu akamwacha Daudi na kutuma wajumbe wamfuate Abneri, nao wakamrudisha kutoka kisima cha Sira. Lakini Daudi hakufahamu jambo hili. 273:27 2Sam 2:8; 4:1; 1Fal 2:5, 32; Kut 21:14; Amu 3:21; 2Sam 2:22-23; 20:9-10Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Ili kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni palepale, naye akafa.

283:28 Kum 21:9Baadaye, Daudi aliposikia kuhusu jambo hili, akasema, “Mimi na ufalme wangu kamwe hatuna hatia mbele za Bwana kuhusu damu ya Abneri mwana wa Neri. 293:29 Law 20:9; 1Fal 2:31-33; Law 15:2; Amu 9:54-57; Za 7:11-16; Mit 2:22; 5:22Damu yake na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na juu ya nyumba yote ya baba yake! Kamwe asikosekane yeyote katika nyumba ya Yoabu mwenye kidonda chenye usaha, au ukoma au mwenye kuegemea fimbo au aangukaye kwa upanga au kupungukiwa na chakula.”

303:30 2Sam 2:23(Yoabu na Abishai ndugu yake walimuua Abneri kwa sababu alikuwa amemuua Asaheli ndugu yao katika vita huko Gibeoni.)

313:31 Za 30:11; 35:13; 69:11; Isa 20:2; Mwa 37:34; Yos 6:7; Amu 11:35; 2Fal 19:1; Ay 16:15; Yoe 1:8Kisha Daudi akamwambia Yoabu na watu wote aliokuwa pamoja nao, “Rarueni nguo zenu na mvae nguo za gunia na mtembee mkiomboleza mbele ya Abneri.” Mfalme Daudi mwenyewe akatembea nyuma ya jeneza. 323:32 Hes 14:1; Mit 24:17; 1Sam 31:4; 2Sam 18:33Wakamzika Abneri huko Hebroni, naye mfalme akalia kwa sauti kwenye kaburi la Abneri. Pia watu wote wakalia.

333:33 Mwa 50:10; 2Sam 1:19; 13:13; Mhu 2:15-16Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri:

“Je, ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?

343:34 Ay 36:8; Za 2:3; 149:8; Isa 45:14; Nah 3:10Mikono yako haikufungwa,

miguu yako haikufungwa pingu.

Ulianguka kama yeye aangukaye

mbele ya watu waovu.”

Nao watu wote wakamlilia tena.

353:35 Rut 1:17; 1Sam 31:13; 2Sam 12:17; Yer 16:7; 1Sam 3:17Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!”

36Watu wote wakaona hilo nao ikawapendeza; naam, kila kitu mfalme alichofanya kiliwapendeza. 37Kwa hiyo siku ile watu wote na Israeli yote wakajua kwamba mfalme hakushiriki katika mauaji ya Abneri mwana wa Neri.

383:38 2Sam 1:19Kisha mfalme akawaambia watu wake, “Je, hamfahamu kwamba mkuu na mtu mashuhuri ameanguka katika Israeli leo? 393:39 2Sam 2:18; 16:9; 18:11; Amu 18:26; 1Fal 2:32; Za 41:10; 101:8; 2Sam 19:7, 13; Za 28:4; 62:12; 2Tim 4:14Nami leo ingawa ni mfalme mpakwa mafuta, mimi ni dhaifu, nao hawa wana wa Seruya wananizidi nguvu. Bwana na amlipize mtenda maovu sawasawa na matendo yake maovu!”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

撒母耳記下 3:1-39

押尼珥之死

1掃羅大衛兩家長期爭戰,大衛家的勢力越來越強,掃羅家卻日益衰微。

2大衛希伯崙生的兒子有耶斯列亞希暖所生的長子暗嫩3迦密拿八的遺孀亞比該所生的次子基利押基述達買的女兒瑪迦所生的三子押沙龍4哈及所生的四子亞多尼雅亞比她所生的五子示法提雅5大衛的妻子以格拉所生的六子以特念大衛的這些兒子都是在希伯崙生的。

6掃羅大衛兩家爭戰期間,押尼珥掃羅家權勢日增。 7他跟掃羅的一個妃嬪、艾押的女兒利斯巴通姦,伊施波設問他:「你為什麼跟我父親的妃嬪一起睡覺呢?」 8押尼珥聽了非常憤怒,說:「難道我是猶大的走狗嗎?我這樣厚待你父親掃羅家和他的親人朋友,沒有把你交給大衛,今天你竟為了一個女人來責備我! 9-10倘若我不照著耶和華應許大衛的誓言把掃羅的江山奪過來交給大衛,讓他統治全以色列猶大,從別示巴,願耶和華重重地懲罰我!」

11伊施波設一句話也不敢答,因為他害怕押尼珥

12押尼珥派使者送信給大衛,說:「這個國家難道不是你的嗎?如果你與我立約,我必幫助你統一以色列。」 13大衛回答說:「好,但你一定要把掃羅的女兒米甲帶來才能見我。」 14於是,大衛派使者去見掃羅的兒子伊施波設說:「請把我的妻子米甲送回來,因為她是我用一百個非利士人的包皮作聘禮娶來的。」 15伊施波設就派人把米甲從她丈夫——拉億的兒子帕鐵那裡接回來。 16帕鐵一路跟著米甲,邊走邊哭,一直到巴戶琳押尼珥對他說:「你回去吧!」他就回去了。

17押尼珥以色列的長老商量說:「你們以前一直都希望大衛做你們的王, 18現在是時候了,因為耶和華曾說要藉著祂僕人大衛的手,從非利士人和其他敵人手中拯救祂的以色列子民。」 19押尼珥也跟便雅憫人商談,然後到希伯崙以色列人和便雅憫人的願望告訴大衛20當時,他帶了二十個人前往希伯崙大衛大衛就設宴款待他們。 21押尼珥大衛說:「我要為我主我王招聚所有的以色列人,跟你立約,你便可以如願以償,統治全以色列。」於是大衛為他送行,他就平安地回去了。

22大衛押尼珥離開後不久,約押就率領大衛的軍隊帶著許多戰利品凱旋而歸。 23約押率領全軍回來後,有人告訴他:「尼珥的兒子押尼珥剛才來朝見王,王送他平安地離去了。」 24約押聽後,就去見王,說:「你這做的是什麼事?押尼珥來見你,你為什麼放他走呢? 25你要知道,尼珥的兒子押尼珥想來騙你,探聽你的虛實。」

26約押大衛那裡出來,派人去追押尼珥,他們在西拉井追上了他,把他帶了回來。大衛對這件事一無所知。 27押尼珥回到希伯崙的時候,約押就把他帶到城門的甕洞,裝作與他密談,乘機用短劍刺入他的肚子,把他殺死了,為他兄弟亞撒黑報了仇。 28大衛聽到消息就說:「耶和華作證,我和我的人民永遠跟尼珥的兒子押尼珥的死無關。 29約押和他全家要承擔這罪,願他的後代永遠有長瘡的、患皮膚病的、拄拐杖的、被刀劍所殺的或挨餓的。」 30約押和他兄弟亞比篩之所以殺押尼珥,是因為押尼珥基遍殺了他們的兄弟亞撒黑

31大衛約押和部下說:「你們要撕裂衣服,腰束麻布,在押尼珥棺前哭喪!」大衛王也跟在棺後送葬。 32他們就把押尼珥葬在希伯崙大衛王和眾人在墓旁大哭一場。 33大衛王哀悼押尼珥,說:

押尼珥啊!

你怎能死得糊里糊塗3·33 糊里糊塗」希伯來文是「像愚笨人」。呢?

34你的手沒有被捆,

你的腳沒有被鎖,

你是死在陰險小人的手裡啊!」

於是眾人都為押尼珥哀哭。 35大衛整天沒有進食,眾人來勸他吃一點東西,但他起誓說:「我若在日落以前吃任何東西,願上帝重重地懲罰我!」 36眾人聽見了,都很喜悅,王做的每一件事都令他們喜悅。 37那天全國的人都看出尼珥的兒子押尼珥的死與大衛無關。 38大衛王對他的隨從說:「你們難道不知道今天以色列損失了一位偉大的將領嗎? 39今天我雖然是耶和華所膏立的王,但仍勢單力薄,無法對付洗魯雅的兩個兒子,願耶和華報應他們的惡行。」