2 Samweli 17 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 17:1-29

1Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Nipe ruhusa niwachague watu kumi na mbili elfu na waanze safari usiku huu huu kumfuatia Daudi. 217:2 2Sam 16:14; 1Fal 22:31; Zek 13:7; Kut 25:18; Yn 11:50; Mt 21:38Nitamshambulia wakati akiwa amechoka na ni dhaifu. Nitampiga na hofu, na kisha watu wote walio pamoja naye watakimbia. Nitampiga mfalme peke yake 317:3 Yer 6:14na kuwarudisha watu wote kwako. Kifo cha mtu yule unayemtafuta kitamaanisha kurudi kwa wote, hakuna hata mtu mmoja atakayeumizwa.” 4Mpango huu ulionekana mzuri kwa Absalomu na kwa wazee wote wa Israeli.

517:5 2Sam 15:32Lakini Absalomu akasema, “Pia mwiteni Hushai, Mwariki, ili tuweze kusikia anachokisema.” 6Hushai alipokuja, Absalomu akasema, “Ahithofeli ametoa shauri hili. Je, tufanye anavyosema? Kama sivyo, tupe maoni yako.”

7Hushai akamjibu Absalomu, “Shauri la Ahithofeli alilotoa halifai kwa wakati huu. 817:8 Hos 13:8; 1Sam 16:18; Amu 18:25Unamfahamu baba yako na watu wake, ni wapiganaji hodari, nao ni wakali kama dubu mwitu aliyepokonywa watoto wake. Zaidi ya hayo, baba yako ni mpiganaji jasiri, usiku hatalala pamoja na vikosi. 917:9 Yer 41:9Hata sasa, amefichwa ndani ya pango au mahali pengine. Kama atatangulia kushambulia vikosi vyako, yeyote asikiaye habari hii atasema, ‘Kuna machinjo makubwa miongoni mwa vikosi vinavyomfuata Absalomu.’ 1017:10 1Nya 12:8; Yos 2:9-11; Eze 21:15; 2Sam 23:8; 1Nya 11:11Basi hata yule askari hodari kuliko wengine wote, ambaye moyo wake ni kama wa simba, atayeyuka kwa hofu, kwa maana Israeli yote wanajua kwamba baba yako ni mpiganaji na kwamba wale walio pamoja naye ni watu hodari.

1117:11 Amu 20:1; Mwa 12:2; Yos 11:4; Mwa 22:17“Kwa hiyo nakushauri: Israeli wote na wakusanyikie kwako, kuanzia Dani hadi Beer-Sheba, katika wingi wao jinsi walivyo kama mchanga wa ufuoni mwa bahari, wewe mwenyewe ukiwaongoza vitani. 12Ndipo tutakapomshambulia popote atakapoonekana, nasi tutamwangukia kama umande unavyoshuka juu ya ardhi. Yeye mwenyewe wala watu wake hakuna atakayeachwa hai. 1317:13 Mik 1:6Kama atakimbilia katika mji wowote, basi Israeli wote watazungushia mji ule kamba, nasi tutauburuta mji huo mpaka bondeni hadi isionekane hata changarawe ya huo mji.”

1417:14 2Sam 16:23; 15:12; 15:34; Neh 4:15; Za 9:16; 2Nya 10:8Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai, Mwariki, ni jema zaidi kuliko lile la Ahithofeli.” Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kupinga shauri nzuri la Ahithofeli, ili kuleta maafa juu ya Absalomu.

15Hushai akawaambia makuhani Sadoki na Abiathari, “Ahithofeli amemshauri Absalomu na wazee wa Israeli kufanya kadha wa kadha, lakini mimi nimewashauri wao kufanya kadha wa kadha. 1617:16 2Sam 15:28-35Sasa tumeni ujumbe haraka na kumwambia Daudi, ‘Usiku huu usilale kwenye vivuko katika jangwa; vuka bila kukosa, la sivyo, mfalme pamoja na watu wote waliofuatana naye watamezwa.’ ”

1717:17 2Sam 15:27, 36; Ay 15:7; 18:16; 1Fal 1:9; Yos 2:4; 15:7Yonathani na Ahimaasi walikuwa wakingoja huko En-Rogeli, naye mtumishi mmoja wa kike akawa anakwenda kuwapasha habari nao wakawa wanakwenda kumwambia Mfalme Daudi, kwa maana wasingetaka kujihatarisha kuonekana wakiingia mjini. 1817:18 2Sam 3:16; 16:5Lakini kijana mmoja mwanaume akawaona, naye akamwambia Absalomu. Basi wote wawili wakaondoka haraka, wakaenda mpaka kwenye nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu. Mtu huyo alikuwa na kisima katika ua wa nyumba yake, nao Yonathani na Ahimaasi wakateremka ndani ya kisima hicho. 1917:19 Yos 2:9Mkewe akachukua kifuniko, akakiweka kwenye mdomo wa kile kisima na kuanika nafaka juu yake. Hakuna mtu yeyote aliyefahamu chochote kuhusu jambo hilo.

2017:20 Kut 1:19; Yos 2:3-5; 1Sam 19:12-18; 21:2Watu wa Absalomu walipofika kwa huyo mwanamke, wakamuuliza, “Wako wapi Ahimaasi na Yonathani?”

Huyo mwanamke akawajibu, “Walivuka kijito.” Watu wa Absalomu wakapekua lakini hawakuwaona hata mmoja, hivyo wakarudi Yerusalemu.

21Baada ya watu hao kuondoka, wale watu wawili yaani Yonathani na Ahimaasi wakapanda kutoka mle kisimani na kwenda kumpasha Mfalme Daudi habari. Wakamwambia, “Ondoka, uvuke haya maji haraka. Ahithofeli ameshauri kadha wa kadha dhidi yako.” 22Kwa hiyo Daudi na watu wote aliokuwa nao waliondoka na kuvuka Yordani. Kufika wakati wa mapambazuko, hapakuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa hajavuka Mto Yordani.

2317:23 2Sam 16:23; 2Fal 20:1; 2Sam 15:12; Mt 27:5; Za 55:23; Ay 31:3Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani kwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.

2417:24 Mwa 32:2; 2Sam 2:8; Yos 13:26Daudi akaenda Mahanaimu, naye Absalomu akavuka Yordani pamoja na watu wote wa Israeli. 2517:25 2Sam 19:13; 20:4-12; 1Fal 2:5, 32; 1Nya 12:18; 2:13-17Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa mtu mmoja aliyeitwa Yetheri, Mwisraeli, ambaye alikuwa amemwoa Abigaili binti Nahashi, dada yake Seruya mamaye Yoabu. 26Waisraeli na Absalomu wakapiga kambi huko nchi ya Gileadi.

2717:27 1Sam 11:1; Kum 3:11; 2Sam 9:4; 19:31-39; 1Fal 2:7; Ezr 2:61; 2Sam 12:30Daudi alipofika Mahanaimu, Shobi mwana wa Nahashi kutoka Raba ya Waamoni, Makiri mwana wa Amieli kutoka Lo-Debari, na Barzilai Mgileadi kutoka Rogelimu 2817:28 1Sam 25:18; Mit 11:25; Mt 5:7wakaleta matandiko ya kitandani, mabakuli na vyombo vya mfinyanzi. Walileta pia ngano na shayiri, unga na bisi, maharagwe na kunde, 2917:29 1Nya 12:40; 2Sam 16:2; Rum 12:13; Kut 15:7; Amu 8:4-6; Za 34:8-10asali na maziwa yaliyoganda, kondoo na jibini kutoka kwenye maziwa ya ngʼombe kwa ajili ya Daudi na watu wake ili wale. Kwa maana walisema, “Watu wameona njaa, tena wamechoka na wamepata kiu huko jangwani.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 17:1-29

亚希多弗计谋落空

1亚希多弗押沙龙说:“让我挑选一万二千人,今夜启程追赶大卫2趁他疲惫无力的时候袭击他,使他惊慌失措,他的部下必逃命。我只把王一个人杀掉, 3把他的部下全都带来归顺你。你寻索的人既然死了,跟随他的人必然会归顺你。这样,大家就平安无事了。” 4押沙龙以色列的长老都赞成这个提议。

5押沙龙说:“召亚基户筛进来,我们也听听他的意见。” 6户筛来了,押沙龙就把亚希多弗的建议告诉他,问他:“我们应该照亚希多弗的提议去做吗?如果不可行,说说你的看法吧。” 7户筛答道:“亚希多弗这次的主意不好! 8你知道你父亲和他的部下,他们都是勇士,现在他们就像丢了熊崽的母熊一样凶猛。况且你父亲是个身经百战的人,他一定不会跟部下睡在一处。 9他现在可能藏在山洞或某个地方。要是他袭击我们的人马,听见的人会说押沙龙的军队惨败了。 10那时候,你手下的人再胆量过人,也会胆战心惊。因为全以色列都知道你父亲是英雄,他的部下都是勇士。 11因此,我认为你应该把从别示巴的那多如海沙的以色列人都聚集起来,然后你亲自率领他们出征。 12这样不管在哪里找到大卫,我们就像露水一样铺天盖地袭击他,让他全军覆没。 13如果大卫退进一座城里,我们以色列全军就拿绳索把那城拉到河谷,连一块石头都不留。”

14押沙龙以色列众人都说:“亚基户筛的主意比亚希多弗的好!”其实是耶和华决定破坏亚希多弗的巧计,好把灾祸降在押沙龙身上。

15户筛亚希多弗和自己为押沙龙以色列长老所提的建议告诉祭司撒督亚比亚他16并说:“你们现在快派人去通知大卫,告诉他今晚不可在旷野的渡口过夜,务必要渡过约旦河,免得他和部下全军覆没。”

17当时,约拿单亚希玛斯躲在隐·罗结,不敢进城,怕被人看见。有一个婢女从城中出来给他们报信,他们便去通知大卫王。 18不料,有一个少年发现了他们,就去告诉押沙龙。他们二人急忙逃走,来到巴户琳的一户人家,藏到那家院子里的一口井内, 19那家的妇人用盖子盖上井口,然后在上面撒了一些麦子,没有人知道这件事。 20押沙龙的部下来到妇人家查问约拿单亚希玛斯的下落,妇人说他们已经过河了。押沙龙的部下就去搜索,结果一无所获,就返回耶路撒冷21押沙龙的部下离开后,约拿单亚希玛斯便从井里爬出来,去向大卫王报信,把亚希多弗的计谋告诉他,请他赶快渡过约旦河。 22大卫王和部下就动身过约旦河,在黎明之前,所有的人都过去了。

23亚希多弗见自己的提议不被接纳,便备上驴,启程回乡,安顿好家事以后,就自缢身亡了。他被安葬在他父亲的墓穴里。

24大卫来到玛哈念押沙龙也率领以色列全军渡过了约旦河。 25押沙龙任命亚玛撒为元帅,代替约押的位置。亚玛撒以实玛利以特拉的儿子,母亲是拿辖的女儿亚比该亚比该约押的母亲洗鲁雅是姊妹。 26押沙龙以色列人在基列地区安营。

27大卫来到玛哈念,受到亚扪拉巴拿辖的儿子朔比罗·底巴亚米利的儿子玛吉基列罗基琳巴西莱的热情招待。 28他们带来被褥、碗盆、瓦器、小麦、大麦、面粉、炒麦、豆子、扁豆、 29蜂蜜、奶油、绵羊和奶酪,送给大卫和跟随他的人,因为他们想:“众人在旷野跋涉,一定饥渴疲乏了。”