2 Samweli 11 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 11:1-27

Daudi Na Bathsheba

111:1 1Fal 20:22; 2Sam 2:18; 1Nya 20:1; Kum 3:11Katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati wafalme watokapo kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu pamoja na watu wa mfalme na jeshi lote la Israeli. Wakawaangamiza Waamoni na kuuzunguka kwa jeshi mji wa Raba. Lakini Daudi akabaki Yerusalemu.

211:2 Kum 22:8; Yos 2:8; Mt 5:28; Mwa 34:2; Ay 31:1; Za 119:37Ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi aliinuka kitandani mwake na kutembeatembea juu ya paa la jumba lake la kifalme. Kutokea kule kwenye paa, akamwona mwanamke akioga. Mwanamke huyo alikuwa mzuri sana wa sura, 311:3 1Nya 3:5; 2Sam 23:34-39naye Daudi akatuma mtu mmoja kuuliza habari za huyo mwanamke. Huyo mtu akamwambia Daudi, “Je, huyu si Bathsheba binti Eliamu, naye ni mke wa Uria, Mhiti?” 411:4 Law 20:10; Za 51; Yak 1:14-15; Kum 22:22; Law 15:25-30; 18:19; Kut 20:17; Ebr 13:4Ndipo Daudi akatuma wajumbe kumleta. Huyo mwanamke akaja kwa Daudi, Daudi akakutana naye kimwili. (Huyo mwanamke ndipo tu alikuwa amejitakasa kutoka siku zake za hedhi.) Kisha akarudi nyumbani kwake. 511:5 Law 20:10Huyo mwanamke akapata mimba akampelekea Daudi ujumbe, kusema, “Mimi ni mjamzito.”

611:6 1Nya 11:41Ndipo Daudi akapeleka ujumbe kwa Yoabu, “Unipelekee Uria, Mhiti.” Naye Yoabu akamtuma Uria kwa Daudi. 7Uria alipofika, Daudi akamuuliza habari za Yoabu, hali za askari na vita kwamba inaendeleaje. 811:8 Mwa 18:4; 43:24; Lk 7:44; Za 44:21; Mwa 19:2Kisha Daudi akamwambia Uria, “Teremka nyumbani kwako ukanawe miguu yako.” Basi Uria akaondoka kutoka kwenye jumba la kifalme, tena zawadi zikamfuata kutoka kwa mfalme. 911:9 Ay 5:12-14Lakini Uria akalala kwenye ingilio la jumba la kifalme pamoja na watumishi wote wa bwana wake, na hakuteremka kwenda nyumbani kwake.

10Daudi alipoambiwa kwamba, “Uria hakwenda nyumbani,” Daudi akamuuliza, “Je, si ndiyo tu umefika kutoka safari ya mbali? Kwa nini hukwenda nyumbani?”

1111:11 2Sam 7:2; 1Sam 21:5; 4:4; 2Sam 20:6; Mt 10:25; 2Tim 2:3Uria akamwambia Daudi, “Sanduku la Mungu, na Israeli na Yuda wanakaa kwenye mahema, naye bwana wangu Yoabu na watu wa bwana wangu wamepiga kambi mahali pa wazi. Ningewezaje kwenda nyumbani kwangu ili nile, ninywe na kukutana na mke wangu? Hakika kama uishivyo sitafanya jambo la namna hiyo!”

1211:12 Ay 20:12-14; Yer 2:22-23Ndipo Daudi akamwambia, “Kaa hapa siku moja zaidi, nami kesho nitakutuma urudi.” Kwa hiyo Uria akakaa Yerusalemu siku ile na siku iliyofuata. 1311:13 Mwa 9:21-22; 19:33-35; Kut 32:21; 1Fal 20:16-21; Mit 20:1; 23:29-35; Hos 4:11; Gal 5:21Kwa ukaribisho wa Daudi, Uria akala na kunywa pamoja naye, Daudi akamlevya. Lakini jioni Uria alitoka kwenda kulala juu ya mkeka wake miongoni mwa watumishi wa bwana wake, hakwenda nyumbani.

1411:14 1Fal 21:8; Za 19:13; 62:9; Mhu 8:11; Yer 9:1-4; Mik 7:3-5Asubuhi yake Daudi akamwandikia Yoabu barua, akamtuma Uria kuipeleka. 1511:15 2Sam 12:9; 12:12Ndani ya barua aliandika, “Mweke Uria mstari wa mbele mahali ambapo mapigano ni makali sana. Kisha wewe uondoke ili Uria aangushwe chini na kuuawa.”

16Hivyo Yoabu alipokuwa ameuzingira mji kwa jeshi, akamweka Uria mahali ambapo alijua kuwa ulinzi wa adui ulikuwa imara sana. 17Wakati watu wa mjini walipotoka kwenda kupigana dhidi ya Yoabu, baadhi ya watu katika jeshi la Daudi wakauawa, zaidi ya hayo, Uria, Mhiti, akafa.

18Yoabu akampelekea Daudi maelezo yote ya vita. 19Akamwagiza mjumbe hivi, “Utakapokuwa umemaliza kumpa mfalme maelezo ya vita, 20hasira ya mfalme yaweza kuwaka, naye aweza kukuuliza, ‘Kwa nini mlisogea karibu hivyo na mji kupigana? Hamkujua kuwa wangeweza kuwapiga mishale kutoka ukutani? 2111:21 Amu 8:31; 9:50-54; 2Sam 20:21; Ay 31:3Ni nani aliyemuua Abimeleki mwana wa Yerub-Besheth? Je, mwanamke hakutupa juu yake jiwe la juu la kusagia kutoka ukutani, kwa hiyo akafa huko Thebesi? Kwa nini mlisogea hivyo karibu ya ukuta?’ Ikiwa atakuuliza hivi, ndipo umwambie, ‘Pia mtumishi wako Uria, Mhiti, amekufa.’ ”

22Mjumbe akaondoka. Alipowasili akamwambia Daudi kila kitu alichokuwa ametumwa na Yoabu kusema. 23Mjumbe akamwambia Daudi, “Watu walituzidi nguvu wakatoka nje ya mji dhidi yetu kwenye eneo la wazi, lakini tuliwarudisha nyuma mpaka kwenye ingilio la mji. 24Ndipo wapiga upinde walitupa mishale kwa watumishi wako kutoka ukutani, na baadhi ya watu wa mfalme wakafa. Zaidi ya hayo, Uria, Mhiti, mtumishi wako amekufa.”

25Daudi akamwambia mjumbe, “Ukamwambie Yoabu hivi, ‘Jambo hili lisikutie wasiwasi, upanga hula huyu sawa na ulavyo mwingine. Zidisha mashambulizi dhidi ya mji na uangamize.’ Mwambie Yoabu hivi ili kumtia moyo.”

26Mke wa Uria aliposikia kwamba mumewe amekufa, akamwombolezea. 2711:27 Kum 34:8; 2Sam 12:9; Za 51:4-5; Ay 10:14; 11:11; Za 45:7; Mit 15:9; Hab 1:13Baada ya muda wa maombolezo kwisha, Daudi akamtaka aletwe nyumbani kwake, naye akawa mkewe, na akamzalia mwana. Lakini jambo alilokuwa amefanya Daudi lilimchukiza Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 11:1-27

大卫犯罪

1第二年春天,诸王又要发动战争。大卫差遣约押率领众将领和以色列大军出征,自己却留在耶路撒冷。他们打败了亚扪人之后又围攻拉巴2一天黄昏,大卫从床上起来在王宫顶上散步,看见一个长得非常漂亮的女人在沐浴。 3大卫就派人去打听这个女人是谁,得知她是以连的女儿、乌利亚的妻子拔示芭4大卫差人把她接来,她来了,大卫就与她同寝,那时她的月经刚洁净。事后,她便回家去了。 5拔示芭怀孕了,就派人去告诉大卫

6大卫便传信给约押,说:“你派乌利亚来见我。”约押就派乌利亚去见大卫7乌利亚来了,大卫问他有关约押、士兵和战争的情况, 8然后吩咐他回家休息。乌利亚离开王宫后,收到大卫送的一份礼物。 9但他跟王的其他仆人一同睡在王宫门口,没有回家。 10大卫得知乌利亚没有回家,便对他说:“你远道而来,为什么不回家休息呢?” 11乌利亚答道:“约柜、以色列人和犹大人都在帐篷里,而我主约押及其军队也在田间扎营,我怎么可以回家吃喝快乐,与妻子同房呢?我敢在王面前起誓,我决不做这样的事!” 12大卫乌利亚说:“你再住一天,明天我会派你回去。”于是乌利亚那日就留在耶路撒冷13第二天,大卫邀请他一同吃饭,把他灌醉了。可是到了晚上,乌利亚还是不肯回家,仍然跟王的其他士兵一同住宿。

14第二天早上,大卫约押写了一封信,要乌利亚带去。 15大卫在信上吩咐约押:“你把乌利亚派到前线最险恶的地方,到时其他人都要撤退,好让敌人杀死他。” 16于是约押围攻城池时,便派乌利亚到最强悍的敌人那里。 17敌人出来迎战,大卫的军中有几位阵亡,乌利亚也死了。 18约押就派人去向大卫禀告战争的详情, 19并叮嘱信使:“你向王禀告战情后, 20他若发怒责问你,‘为什么还冒死逼近呢?你们难道不知道敌人会从城墙上射箭吗? 21难道你们不知道耶路·比设11:21 耶路·比设”又名“耶路·巴力”,参见士师记6:32的儿子亚比米勒是谁杀的吗?一个妇人从城墙上扔下一块磨石,把他砸死在提备斯。你们为什么还要逼近城墙呢?’你就对王说,‘你的仆人乌利亚也死了。’”

22于是,信使前来见大卫,照约押的吩咐向大卫禀告。 23他说:“敌军势力强大,在城外跟我们交战,但我们把他们追到城门口。 24敌军的弓箭手从城墙上射死了王的几个士兵,乌利亚也死了。” 25大卫便对信使说:“你去告诉约押不要为这事难过,因为刀剑无情。让他只管竭力攻陷城池。要这样勉励约押。”

26拔示芭听到丈夫乌利亚的死讯之后就为他守丧。 27守丧结束后,大卫便派人把她接进宫里,她就做了大卫的妻子,并给他生了个儿子。然而,大卫的所作所为令耶和华十分不悦。