2 Petro 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Petro 2:1-22

Walimu Wa Uongo Na Uangamivu Wao

1Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Bwana wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka. 2Hata hivyo, wengi watafuata njia zao za ufisadi, na kwa ajili yao njia ya kweli itatukanwa. 32:3 2Kor 2:17; 1The 2:5Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi.

42:4 1Tim 3:6; Ufu 20:1, 2Kwa maana, kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu2:4 Kuzimu hapa linalotokana na neno Tartarus la Kiyunani; maana yake ni kule ndani sana katika mahali pa mateso kwa watu waliopotea. katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu; 52:5 2Pet 3:6; Ebr 11:7; 1Pet 3:20kama hakuusamehe ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya watu wale wasiomcha Mungu, bali akamhifadhi Noa, mhubiri wa haki, pamoja na watu wengine saba; 62:6 Mwa 19:24, 25kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza kwa moto ikawa majivu, na kuifanya kuwa kielelezo kwa yale yatakayowapata wale wasiomcha Mungu; 72:7 Mwa 19:16; 2Pet 3:17na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki, ambaye alihuzunishwa na maisha machafu ya watu wapotovu 82:8 Ebr 11:4; Eze 9:4; Za 119:130, 158(kwa sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya siku): 92:9 Za 37:33; 1Kor 10:13ikiwa hivyo ndivyo, basi Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa wamchao Mungu kutoka majaribu, na kuwaweka waasi katika adhabu hadi siku ya hukumu. 102:10 2Pet 3:3Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka.

Kwa ushupavu na kwa kiburi, watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni. 11Lakini hata malaika, ingawa wana nguvu na uwezo zaidi, hawaleti mashtaka mabaya dhidi ya viumbe kama hao mbele za Bwana. 122:12 Za 49:12Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiyoyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawaliwa na hisia za mwili, waliozaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa. Hawa nao kama wanyama wataangamizwa pia.

132:13 Isa 38:12; 2Kor 5:1, 4Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu zenu. 142:14 2Tim 4:6; Yn 13:36; 21:18, 19Wakiwa na macho yaliyojaa uzinzi, kamwe hawaachi kutenda dhambi. Huwashawishi wale wasio imara. Wao ni hodari kwa kutamani; ni wana wa laana! 152:15 Lk 9:31; Hes 22:4-20; 31:16; Kum 23:4; Yud 11; Ufu 2:14Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa mshahara wa uovu. 162:16 Mk 13:26; Hes 22:21-30Lakini kwa ajili ya uovu wake, alikemewa na punda, mnyama asiyejua kusema, akaongea akitumia sauti ya mwanadamu na kuzuia wazimu wa huyo nabii.

172:17 Mt 3:17; Yud 12, 13Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji, na ukungu upeperushwao na tufani. Giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao. 182:18 Mt 17:6; Yud 16; 2Pet 2:20; 1:4Kwa maana wao hunena maneno makuu mno ya kiburi cha bure, na kwa kuvutia tamaa mbaya za asili ya mwili, huwashawishi watu ambao ndipo tu wamejiondoa miongoni mwa wale wanaoishi katika ufisadi. 192:19 Za 119:105; Ufu 22:16Huwaahidi uhuru hao waliowanasa, wakati wao wenyewe ni watumwa wa ufisadi: kwa maana mtu ni mtumwa wa kitu chochote kinachomtawala. 202:20 2Tim 3:16; 2Sam 23:2Kama wameukimbia upotovu wa dunia kwa kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kisha wakanaswa tena humo na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. 212:21 Eze 18:24; Ebr 10:26, 27Ingelikuwa afadhali kwao kama wasingeliijua kamwe njia ya haki, kuliko kuijua kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyokabidhiwa. 222:22 Mit 26:11Imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli isemayo: “Mbwa huyarudia matapiko yake mwenyewe,” tena, “Nguruwe aliyeoshwa hurudi kugaagaa matopeni.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

彼得后书 2:1-22

假教师

1以往曾经有假先知在百姓中出现,将来在你们中间也同样会有假教师出现。他们暗地里引进使人沉沦的异端邪说,甚至否认那位买赎他们的主。这些人正迅速地自招灭亡。 2许多人会效法他们邪恶无耻的行为,致使真理之道被人毁谤。 3他们贪婪成性,想用花言巧语在你们身上谋利。这种人的刑罚自古已经判定,他们很快就会灭亡。

4即使天使犯了罪,上帝也没有容忍他们,而是把他们丢在地狱里,囚在幽暗的深坑等候审判。 5上帝也没有容忍远古的世代,曾用洪水淹灭了世上不敬虔的恶人,只留下传讲上帝公义的挪亚和他的七位家人。 6上帝也审判了所多玛蛾摩拉,将二城毁灭,烧为灰烬,作为以后不敬虔之人的警戒。 7祂只拯救了因恶人的淫乱放荡而忧伤的义人罗得8因为义人罗得住在他们当中,天天耳闻目睹他们一切无法无天的丑行,他正直的心很痛苦。 9上帝知道怎样拯救敬虔的人脱离试炼,把不义的人拘禁在刑罚之下,等候审判的日子, 10尤其是那些放纵污秽的情欲、轻视权柄的人。他们胆大妄为,肆无忌惮地毁谤有尊荣的。 11即使力量和权能更大的天使都不敢在主面前用毁谤的话控告有尊荣的。 12但他们好像没有理性,生下来就是预备让人捉去宰杀的牲畜,连自己不懂的事也随口毁谤。他们在毁坏别人的时候,自己也必灭亡。 13他们多行不义,必自食恶果。他们喜爱在大白天寻欢作乐,是你们中间的败类和渣滓,一面和你们同席,一面以欺骗为乐。 14他们眼中充满淫欲,不停地犯罪,引诱那些信心不坚定的人。他们贪婪成性,实在是该受咒诅! 15他们离弃正道,走入歧途,重蹈比珥之子巴兰先知的覆辙。巴兰贪爱不义之财, 16因自己的罪而受了责备。不能说话的驴竟然像人一样说起话来,制止了他狂妄的行为。

17他们如同枯干的水井和被狂风吹散的雾气,有幽幽黑暗留给他们。 18他们口出狂言,空话连篇,以肉体的邪情私欲为饵,诱惑那些刚刚摆脱了荒谬生活的人。 19他们应许那些人可以得自由,而自己却做罪恶的奴隶,因为人被什么制服,就被什么奴役。

20如果他们借着认识我们的主和救主耶稣基督,已经摆脱了世俗的污秽,但后来又被这些事缠住、俘虏了,他们的处境会比以前更糟糕。 21他们明知道正路,却背弃了传给他们的神圣诫命,这样倒不如不知道的好。 22俗语说得好:“狗转过身来,吃自己所吐的;猪洗干净了,又回到污泥里去打滚。”这些话正好用在他们身上。