2 Petro 1 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Petro 1:1-21

11:1 Rum 1:1; 1Pet 1:1; Rum 3:21-26; Tit 2:13Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo:

Kwa wale ambao kwa njia ya haki ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo mmepokea imani iliyo na thamani kama yetu:

21:2 2Pet 3:18; Rum 1:7; Flp 3:8; 2Pet 2:20; 1:3, 8Neema na amani iwe kwenu kwa wingi katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.

Wito Wa Mkristo Na Uteule

31:3 1Pet 1:5; Rum 8:28; 1The 2:12Uweza wake wa uungu umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 41:4 2Kor 7:1; Efe 4:24; Ebr 12:10; Yak 1:27Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya uungu, na kuokoka kutoka upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya.

51:5 Kol 2:3; 2Pet 3:18; 1Pet 3:7; Gal 5:6, 22; Yud 3Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; 61:6 Mdo 24:25; Ebr 10:36; 2Pet 1:3katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa;1:6 Maana yake kumcha Mungu. 71:7 Rum 12:10; 1The 3:12; Gal 6:18; 1The 5:15; 1Yn 4:21katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo. 81:8 Yn 15:2; Kol 1:10Kwa maana haya yakiwa ndani yenu kwa wingi na kuzidi kuongezeka, yanawasaidia msikose bidii wala kutozaa matunda katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 91:9 1Yn 2:11; Mt 1:21Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya haoni mbali, na ni kipofu, naye amesahau kule kutakaswa kutoka dhambi zake za zamani.

101:10 Za 15:5; Rum 8:28; Za 15:5; 2Pet 3:17; Yud 24Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu. Kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe, 111:11 Za 145:13; 2Tim 4:18; 2Pet 2:20; 3:18na mtajaliwa kwa ukarimu mwingi kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Unabii Wa Maandiko

121:12 1Yn 2:21; Flp 3:1; Yud 5; 2Yn 2Hivyo nitawakumbusha mambo haya siku zote, hata ingawa mnayajua na mmethibitishwa katika kweli mliyo nayo. 131:13 Isa 38:12; 2Kor 5:14; 2Pet 3:1; 2Kor 5:1, 4Naona ni vyema kuwakumbusha mambo haya wakati wote niwapo katika hema hili ambalo ni mwili wangu, 141:14 2Tim 4:6; Yn 13:36; 21:18, 19kwa sababu najua ya kwamba hivi karibuni nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Yesu Kristo alivyoliweka wazi kwangu. 151:15 Lk 9:31; Hes 22:4-20; 31:16; Kum 23:4; Yud 11; Ufu 2:14Nami nitafanya kila juhudi kuona kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaweza kuyakumbuka mambo haya siku zote.

161:16 Mk 13:26; Hes 22:21-30; 1Kor 1:17; 2:1, 4; 2Kor 2:17; 4:2Tulipowafahamisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulishuhudia kwa macho yetu ukuu wake. 17Alipewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, sauti ilipomjia katika Utukufu Mkuu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana.” 18Sisi wenyewe tuliisikia sauti hii ambayo ilitoka mbinguni, wakati tulipokuwa pamoja naye kwenye ule mlima mtakatifu.

191:19 Za 119:105; Ufu 22:16Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyongʼaa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu. 201:20 Rum 12:6; 2Pet 3:3Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe. 211:21 2Tim 3:16; 2Sam 23:2; Mdo 1:16Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

彼得後書 1:1-21

1我是耶穌基督的奴僕和使徒西門·彼得,寫信給藉著我們的上帝和救主耶穌基督的義,與我們得到同樣寶貴信心的人。

2願你們因認識上帝和我們主耶穌而得到豐富的恩典和平安!

追求長進

3因為我們認識了用自己的榮耀和美德呼召我們的上帝,上帝以祂神聖的能力將生命與敬虔所需要的一切賜給了我們。 4藉此,祂已將既寶貴又偉大的應許賞給了我們,使我們脫離世上私慾帶來的敗壞,能夠有份於上帝的性情。

5正因如此,你們要加倍努力,不僅要有信心,還要有好的德行;不僅要有好的德行,還要有知識; 6不僅要有知識,還要有節制;不僅要有節制,還要有忍耐;不僅要有忍耐,還要有敬虔; 7不僅要有敬虔,還要有愛弟兄姊妹的心;不僅要有愛弟兄姊妹的心,還要有愛眾人的心。 8如果充分具備了這些品德,你們對我們主耶穌基督的認識就不會停滯不前,毫無收穫。 9缺乏上述品德的人不是瞎眼就是目光短淺,忘記他從前的罪已經得到潔淨。

10所以,弟兄姊妹,你們要更加努力,以確定自己蒙了呼召和揀選。這樣,你們就絕不會失足犯罪, 11進入我們的主和救主耶穌基督永恆國度的大門必為你們敞開。

12雖然你們已經知道這些事,並且在所領受的真道上也很堅固,但我還是要常常提醒你們。 13我覺得應當趁著我還在世的時候1·13 還在世的時候」希臘文是「還在這帳篷裡的時候」,作者用帳篷代表自己的身體。提醒你們,激勵你們, 14因我知道自己離世的日子已經不遠了,正如我們的主耶穌基督指示我的。 15我要盡力使你們在我離世以後仍然常常記得這些事。

見證基督的榮耀

16我們從前告訴你們有關主耶穌基督的大能和祂降臨的事,並非根據巧妙虛構的神話,而是我們親眼見過祂的威榮。 17祂從父上帝那裡得到了尊貴和榮耀,那時從極大的榮光中有聲音對祂說:「這是我的愛子,我甚喜悅祂。」 18當時我們和祂一同在聖山上,親耳聽見了這來自天上的聲音。

19這使我們更加確信先知的預言。你們要留意這些預言,把這些預言看作照耀在黑暗中的明燈,一直到天破曉、晨星在你們心中升起。 20你們首先該知道:聖經上的一切預言都不可隨人的私意解釋, 21因為預言絕非出於人的意思,都是人受了聖靈的感動,講出上帝的信息。