2 Nyakati 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 5:1-14

15:1 1Fal 6:14; 2Sam 8:11; 1Nya 26:26-28; 22:14Hivyo Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni

(1 Wafalme 8:1-9)

25:2 2Sam 6:12; 1Nya 15:25; 1Fal 8:1; 1Nya 29:1Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 35:3 2Nya 7:8-10; 1Fal 8:2Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba.

45:4 Yos 3:6Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, 55:5 Hes 3:31; 1Nya 15:2nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, 6naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

75:7 Ufu 11:19Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. 85:8 Mwa 3:24Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea. 95:9 1Fal 8:8Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 105:10 Ebr 9:4; Kum 10:2; Kut 16:34; 2Nya 6:11Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

115:11 1Nya 24:1Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. 125:12 1Nya 15:16-24; 9:33Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. 135:13 1Nya 16:34; Yer 33:11; Za 106:1; 2Nya 7:3; Za 136:1-6Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema:

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu, 145:14 Kut 40:35; 19:16; 2Nya 7:2-3; Ufu 15:8; Hes 19:5; Isa 6:4; Eze 43:4; Hag 2:7; 2Kor 3:11nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu la Mungu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 5:1-14

1这样,所罗门完成了耶和华殿的一切工作。所罗门把他父亲大卫献给上帝的金银和一切器具都搬进上帝殿的库房。

运约柜入圣殿

2所罗门以色列的长老、各支派的首领和族长召集到耶路撒冷,准备把耶和华的约柜从大卫锡安运上来。 3在七月住棚节的时候,以色列人都聚集到所罗门王那里。 4以色列的长老到齐后,祭司便抬起约柜, 5祭司和利未人将约柜、会幕和会幕里的一切圣器运上来。 6所罗门王和聚集到他那里的以色列全体会众在约柜前献祭,献上的牛羊多得不可胜数。 7祭司把耶和华的约柜抬进内殿,即至圣所,放在两个基路伯天使的翅膀下面。 8基路伯天使展开翅膀,遮盖约柜和抬约柜的横杠。 9横杠非常长,在至圣所前面的圣所中也看得见横杠的末端,但在圣所外面看不见。横杠至今仍在那里。 10约柜里除了两块石版,没有别的东西。石版是以色列人离开埃及后,耶和华在何烈山跟他们立约时,摩西放进去的。

耶和华的荣耀

11随后,祭司退出圣所,所有在场的祭司不分班次都已洁净自己。 12所有负责歌乐的利未亚萨希幔耶杜顿,以及他们的儿子和亲族都穿着细麻布衣服,站在祭坛的东边,敲钹、鼓瑟、弹琴,同时还有一百二十位祭司吹号。 13吹号的和歌乐手一起同声赞美和称谢耶和华,伴随着号、钹及各种乐器的声音,高声赞美耶和华:

“祂是美善的,

祂的慈爱永远长存!”

那时,有云彩充满了耶和华的殿, 14以致祭司不能在殿里供职,因为殿里充满了耶和华上帝的荣光。