2 Nyakati 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 2:1-18

Maandalizi Ya Kujenga Hekalu

(1 Wafalme 5:1-18)

12:1 Kum 12:5; 1Fal 5:5; Mhu 2:14Solomoni akatoa amri kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. 22:2 2Nya 10:4; 1Fal 5:15Solomoni akaandika watu 70,000 kuwa wachukuzi wa mizigo, na watu 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na watu 3,600 kuwa wasimamizi wao.

32:3 2Sam 5:11; 1Nya 14:1Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro:

“Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi. 42:4 Kut 12:5; 25:30; Law 24:8; Kut 29:42; Hes 28:10; Kut 30:7; Mt 12:4Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonyesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za Bwana Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.

52:5 1Nya 22:5; 16:25; Za 135:5; Kut 15:11; Za 86:8-9; Yer 10:6“Hekalu nitakalolijenga litakuwa kubwa, kwa sababu Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote. 62:6 1Fal 8:27; Yer 23:24; 2Nya 6:28; Kut 3:11; Isa 66:1Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?

72:7 Kut 35:31; 1Nya 22:16“Hivyo basi nitumie mtu mwenye ustadi wa kufanya kazi ya kutengeneza dhahabu na fedha, shaba na chuma, nyuzi za rangi ya zambarau, nyekundu na buluu, mwenye uzoefu wa kutia nakshi, ili afanye kazi Yuda na Yerusalemu pamoja na mafundi wangu wenye ustadi, ambao baba yangu Daudi aliwaweka.

82:8 1Fal 5:6; 19:11“Pia nitumie magogo ya mierezi, miberoshi na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako 9ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. 102:10 1Fal 5:11; Ezr 3:7Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,0002:10 Kori 20,000 za ngano ni sawa na lita 4,400. za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,0002:10 Bathi 20,000 za mvinyo au mafuta ni sawa na lita 440,000. za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”

112:11 1Fal 10:9; 2Nya 9:8; Kum 33:3Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua:

“Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”

122:12 Neh 9:6; Mdo 4:24; Za 146:6; 1Fal 5:7; Za 33:6; 102:25; Ufu 10:6Naye Hiramu akaongeza kusema:

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.

132:13 1Fal 7:13“Mimi nitamtuma kwako Huramu-Abi, mtu mwenye ustadi mwingi, 142:14 Kut 31:6; 35:31-35; 1Fal 7:13ambaye mama yake alitoka Dani na baba yake alitoka Tiro. Yeye ni stadi wa kutengeneza vitu, kufanya kazi zote za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mbao pamoja na kufuma. Ni stadi katika kutia rangi ya zambarau, buluu, nyekundu na nguo za kitani safi. Yeye ana ujuzi katika aina zote za kutia nakshi na anaweza kufuatiliza mchoro wowote wa kazi anayopewa. Atafanya kazi na mafundi wako na wale wa bwana wangu, Daudi baba yako.

15“Sasa basi bwana wangu na awapelekee watumishi wake ngano, shayiri, mafuta ya zeituni na mvinyo kama alivyoahidi, 162:16 Yos 19:46; Mdo 9:36; Yon 1:3; 1Fal 5:8nasi tutakata magogo yote yale unayohitaji kutoka Lebanoni nasi tutayafunga pamoja na kuyaweka yaelee baharini mpaka Yafa. Kisha utaweza kuyachukua mpaka Yerusalemu.”

172:17 1Nya 22:2; 2Sam 24:2; 2Nya 8:7-8; 1Fal 5:1Ndipo Solomoni akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu 153,600. 18Akawaweka watu 70,000 miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na 3,600 wakiwa wasimamizi juu yao ili wawahimize watu kufanya kazi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 2:1-18

预备建圣殿

1所罗门决定为耶和华的名建造殿宇,也为自己兴建王宫。

2他征用七万名搬运工、八万名在山上凿石的匠人、三千六百名监工, 3并派人去见泰尔希兰,说:“你曾运香柏木给我父亲建造王宫,请你也照样帮助我。 4现在,我要为我的上帝耶和华的名建一座殿,我要把殿献给祂,在祂面前烧芬芳的香,经常献上供饼,在每天早晚、安息日、朔日2:4 朔日”即每月初一。及我们的上帝耶和华所定的节期献上燔祭。这是以色列人应当永远遵守的定例。 5我要建造的殿宇极其宏伟,因为我们的上帝超越一切神明。 6诸天尚且容纳不下祂,谁能为祂建造殿宇呢?我是谁,怎能为祂建造殿宇?我不过是建个向祂烧香的地方。 7现在,请你派一位巧匠来,他要懂得雕刻,会用金银铜铁铸造物品,会编织紫色、朱红色和蓝色的布,好与我父大卫犹大耶路撒冷所预备的巧匠一起工作。 8也请你从黎巴嫩运些香柏木、松木和檀香木来,因为我知道你的仆人擅长砍伐黎巴嫩的树木。我会派人与你的仆人一起工作。 9我要建的殿宇非常宏伟,所以需要的木料非常多。 10我会供给你的伐木工人四百四十万升小麦、四百四十万升大麦、四十四万升酒和四十四万升油。”

11泰尔希兰写信给所罗门说:“耶和华爱祂的子民,所以立你做他们的王。 12创造天地的以色列的上帝耶和华当受称颂!祂赐给大卫王一个有智慧、谋略和悟性的儿子来为耶和华建殿,也为他自己建造王宫。 13现在,我派聪明能干的巧匠户兰去你那里。 14他的母亲是支派的人,父亲是泰尔人。他精于雕刻和设计,善用金银铜铁和木石制造物品,又会编织紫色、蓝色、朱红色的布和细麻布。你可以让他与你的工匠和你父亲大卫的工匠一起工作。 15现在,请我主把许诺的小麦、大麦、油和酒运给仆人。 16我们会在黎巴嫩砍伐你需要的木材,扎成木筏,经海道运到约帕,你可以从那里将木材转运到耶路撒冷。”

17所罗门依照他父亲大卫的方法,统计所有寄居在以色列的外族人,共有十五万三千六百人。 18他指派其中的七万人做搬运工,八万人在山上采凿石头,三千六百人做监工。