2 Nyakati 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 1:1-17

Solomoni Aomba Hekima

(1 Wafalme 3:1-15)

11:1 1Fal 2:26; 2Nya 12:1; Mwa 39:2; Hes 14:43; 1Nya 29:25; Mwa 21:22; 1Nya 17:8; Mt 28:20Solomoni mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwa Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno.

21:2 1Nya 28:1; 2Nya 29:20; 30:2Ndipo Solomoni akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa. 31:3 Law 17:4; Kut 36:8; 40:18; 1Fal 3:4Naye Solomoni na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko Hema la Kukutania la Mungu lilipokuwa, ambalo Mose mtumishi wa Bwana alikuwa amelitengeneza huko jangwani. 41:4 2Sam 6:2, 17; 1Nya 15:25Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu. 51:5 Kut 38:2; 31:2; 1Nya 13:3Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko. 61:6 1Fal 3:4Solomoni akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.

71:7 2Nya 7:12; Isa 58:9; 1Fal 3:5; Mit 3:5Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”

81:8 1Nya 23:1; 28:5Solomoni akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake. 91:9 2Sam 7:25; 1Fal 8:25; Mwa 12:2Sasa, Bwana Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi. 101:10 Hes 27:17; Mit 8:15-16; Kum 31:2; 1Fal 3:9; Za 119:34; Mit 3:13; Yak 1:5Nakuomba unipe mimi hekima na maarifa, ili niweze kuongoza watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kutawala hawa watu wako walio wengi hivi?”

111:11 Kum 17:17; 1Sam 16:7; 1Fal 3:11; 8:18Mungu akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao, 121:12 1Nya 29:12-25; Neh 13:26; Efe 3:20; 2Nya 9:22; Za 34:9-10; Mt 6:33; Mhu 2:9kwa hiyo utapewa hekima na maarifa. Tena nitakupa pia mali, utajiri na heshima, ambavyo hakuna mfalme yeyote aliyekuwepo kabla yako amewahi kuwa navyo, na hakuna yeyote baada yako atakayekuwa navyo.”

Fahari Ya Solomoni

(1 Wafalme 10:26-29)

13Ndipo Solomoni akaenda mpaka Yerusalemu kutoka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kutoka mbele ya Hema la Kukutania. Naye akatawala Israeli.

141:14 1Sam 8:11; 1Fal 9:19; 4:26Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 151:15 1Fal 9:28; Isa 60:5; Ay 22:24; 1Fal 10:27Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 16Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.1:16 Yaani Kilikia. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. 171:17 Wim 1:9Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 6001:17 Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7. za fedha, na farasi kwa shekeli 150.1:17 Shekeli 150 ni sawa na kilo 1.7. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 1:1-17

所罗门王求智慧

1大卫的儿子所罗门巩固了自己的王位。因为他的上帝耶和华与他同在,使他极其伟大。

2所罗门召集所有以色列人,包括千夫长、百夫长、审判官、首领和族长, 3与他们一起去基遍的丘坛,因为那里有上帝的会幕,是耶和华的仆人摩西在旷野制造的。 4大卫已经把上帝的约柜从基列·耶琳搬到耶路撒冷,因为他在那里为约柜搭了一个帐篷。 5户珥的孙子、乌利的儿子比撒列造的铜坛在基遍耶和华的会幕前,所罗门和会众就在那里求问耶和华。 6所罗门上到耶和华会幕前的铜坛那里,献上一千头祭牲作为燔祭。

7当天晚上,上帝向所罗门显现,问他:“你要我给你什么?只管求吧。” 8所罗门回答说:“你厚待我父大卫,并让我继位。 9耶和华上帝啊,求你成就你给我父大卫的应许。你立我为王,使我统治这多如地上尘土的百姓。 10现在,求你赐我智慧和知识以带领他们。不然,谁能治理这么多的百姓呢?” 11上帝对所罗门说:“你既然有此心愿,不为自己求富贵、资财、尊荣、长寿,也没有求灭绝你的敌人,只求智慧和知识以治理我的子民——我交在你王权之下的百姓, 12我必赐你智慧和知识,并且我还要赐你空前绝后的富贵、资财和尊荣。”

13于是,所罗门基遍丘坛的会幕前回到耶路撒冷治理以色列

所罗门王的兵力和财富

14所罗门组建了战车和骑兵,有一千四百辆战车、一万二千名骑兵,驻扎在屯车城和他所在的耶路撒冷15王使耶路撒冷的金银多如石头,使香柏木多如丘陵的无花果树。 16所罗门的马匹都是由王室商队从埃及古厄按定价买来的。 17他们从埃及买来的车马,每辆车六百块银子,每匹马一百五十块银子,他们也把车马卖给人诸王和亚兰诸王。