1 Wathesalonike 4 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wathesalonike 4:1-18

Maisha Yanayompendeza Mungu

14:1 2Kor 13:11; 5:9Hatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Yesu kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo. 2Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Yesu.

34:3 1Kor 6:18Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, 44:4 1Kor 7:2-9ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, 54:5 Rum 1:26; Efe 4:17si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. 64:6 1Kor 6:8; Ebr 13:4Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. 74:7 Law 11:44; 1Pet 1:15Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu. 84:8 Rum 5:5; Gal 4:6Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.

94:9 Rum 12:10; Yn 13:34; 1The 5:1Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. 104:10 1The 1:7; 3:12Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.

114:11 Efe 4:28; 2The 3:10-12Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, 124:12 Mk 4:11ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.

Kuja Kwake Bwana

134:13 Efe 2:12Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. 144:14 1Kor 15:18Kwa kuwa tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake. 154:15 1Kor 15:52Kulingana na neno la Bwana mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia waliolala mauti. 164:16 Mt 24:31; 1Kor 15:23; 2The 2:1Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Kristo watafufuka kwanza. 174:17 Mdo 1:9; Ufu 11:12; 1Kor 15:52; Yn 12:26Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.

King James Version

1 Thessalonians 4:1-18

1Furthermore then we beseech you, brethren, and exhort you by the Lord Jesus, that as ye have received of us how ye ought to walk and to please God, so ye would abound more and more. 2For ye know what commandments we gave you by the Lord Jesus. 3For this is the will of God, even your sanctification, that ye should abstain from fornication: 4That every one of you should know how to possess his vessel in sanctification and honour; 5Not in the lust of concupiscence, even as the Gentiles which know not God: 6That no man go beyond and defraud his brother in any matter: because that the Lord is the avenger of all such, as we also have forewarned you and testified. 7For God hath not called us unto uncleanness, but unto holiness. 8He therefore that despiseth, despiseth not man, but God, who hath also given unto us his holy Spirit. 9But as touching brotherly love ye need not that I write unto you: for ye yourselves are taught of God to love one another. 10And indeed ye do it toward all the brethren which are in all Macedonia: but we beseech you, brethren, that ye increase more and more; 11And that ye study to be quiet, and to do your own business, and to work with your own hands, as we commanded you; 12That ye may walk honestly toward them that are without, and that ye may have lack of nothing.

13But I would not have you to be ignorant, brethren, concerning them which are asleep, that ye sorrow not, even as others which have no hope. 14For if we believe that Jesus died and rose again, even so them also which sleep in Jesus will God bring with him. 15For this we say unto you by the word of the Lord, that we which are alive and remain unto the coming of the Lord shall not prevent them which are asleep. 16For the Lord himself shall descend from heaven with a shout, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first: 17Then we which are alive and remain shall be caught up together with them in the clouds, to meet the Lord in the air: and so shall we ever be with the Lord. 18Wherefore comfort one another with these words.