1 Wathesalonike 2 – NEN & CRO

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wathesalonike 2:1-20

Huduma Ya Paulo Huko Thesalonike

12:1 1The 1:5-9Ndugu zangu, kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ya kwamba kuja kwetu kwenu hakukuwa bure, 22:2 Mdo 16:22; Flp 1:30kama vile mjuavyo, tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu wetu, tulikuwa na ujasiri wa kuwaambia Injili ya Mungu ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa. 32:3 2Kor 2:17Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. 42:4 Gal 2:7; 1:10Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. 52:5 Mdo 20:33; Rum 1:9Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu. 62:6 1Kor 9:1-2Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote.

Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, 72:7 1The 2:11; 1Kor 2:3; 9:22; 2Kor 1:4; 7:6, 7lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo. 82:8 2Kor 12:15; 1Yn 3:16Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu. 92:9 Mdo 18:3; 2Kor 11:9; 2The 3:8Ndugu zetu, mnakumbuka juhudi yetu na taabu yetu. Tulifanya kazi usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote wa kwenu wakati tulipokuwa tunawahubiria Injili ya Mungu.

102:10 2Kor 1:12Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini. 112:11 1Kor 4:14Maana mnajua kwamba tuliwatendea kila mmoja wenu kama vile baba awatendeavyo watoto wake. 122:12 Efe 4:1Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza kuishi maisha yampendezayo Mungu, anayewaita katika Ufalme na utukufu wake.

132:13 Ebr 4:12Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 142:14 Gal 1:22; Mdo 17:5; 2The 1:4Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyoko ndani ya Kristo Yesu katika Uyahudi. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi, 152:15 Mdo 2:23; Mt 5:12wale waliomuua Bwana Yesu na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote, 162:16 Mdo 13:45-50; Mt 23:32wakijitahidi kutuzuia tusizungumze na watu wa Mataifa ili kwamba wapate kuokolewa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao hadi kikomo. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.

Paulo Atamani Kuwaona Wathesalonike

172:17 1Kor 5:3; Kol 2:5; 1The 3:10Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa kitambo kidogo (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso. 182:18 Mt 4:10; Rum 1:13; 15:22Maana tulitaka kuja kwenu, hasa mimi Paulo, nilitaka kuja tena na tena, lakini Shetani akatuzuia. 192:19 Flp 4:1; 2Kor 1:14; Mt 16:27; 1The 3:13Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu au taji yetu ya kujisifia mbele za Bwana Yesu Kristo wakati wa kuja kwake? Je, si ni ninyi? 202:20 2Kor 1:14Naam, ninyi ndio fahari yetu na furaha yetu.

Knijga O Kristu

1 Solunjanima 2:1-20

Pavao se sjeća posjeta Solunjanima

1Znate i sami, draga braćo i sestre, da naš dolazak k vama nije bio uzaludan. 2Znate da su nas prije toga u Filipima zlostavljali i izvrgnuli ruglu. Ipak smo se odvažili, pouzdajući se u Boga, propovijedati vam evanđelje, iako uz tešku borbu. 3Vidite dakle da u našemu propovijedanju nema govora o zabludi, nečistim pobudama ili prijevari.

4Navješćujemo Radosnu vijest upravo onako kako nam je Bog povjerio da činimo. Ne trudimo se ugoditi ljudima, nego Bogu koji proniče srca. 5Nikada vas nismo pokušali pridobiti laskanjem. Bog nam je svjedok i da nikada ništa nismo činili iz pohlepe. 6Niti smo od ljudi tražili slavu—ni od vas ni od bilo koga drugoga. 7Mogli smo od vas kao Kristovi apostoli što i zahtijevati, ali nismo. Bili smo prema vama blagi poput majke koja s ljubavlju njeguje svoju djecu. 8Toliko smo vas voljeli da smo vam htjeli predati ne samo Božju Radosnu vijest nego i vlastiti život.

9Pa sjećate se, draga braćo i sestre, našega teškog truda i umora! Dok smo vam propovijedali evanđelje, radili smo noću i danju da nikomu od vas ne budemo na teret. 10I vi i Bog ste nam svjedoci da smo se sveto, pravedno i besprijekorno vladali prema vama vjernicima. 11Postupali smo prema svakomu od vas kao otac prema vlastitoj djeci. 12Poticali smo vas, hrabrili i zaklinjali da živite životom dostojnim Boga koji vas je pozvao u svoje kraljevstvo da s njime dijelite njegovu slavu.

13Zato bez prestanka zahvaljujemo Bogu što Božju poruku koju smo vam navijestili niste primili kao ljudsku, nego kao Božju riječ, što ona uistinu i jest. A ona djeluje u vama koji vjerujete.

14Vi ste, draga braćo, pretrpjeli od svojih sunarodnjaka progonstvo te ste tako prošli jednako kao i članovi Božjih kršćanskih crkava u Judeji, koje su zbog vjere u Krista Isusa progonili njihovi vlastiti sunarodnjaci, Židovi. 15Oni su poubijali vlastite proroke, pa čak i Gospodina Isusa. Nas su žestoko progonili. Ne ugađaju Bogu i neprijatelji su svim ljudima 16jer nam priječe propovijedati poganima da se oni ne bi spasili. Navršili su tako mjeru svojih zlodjela. Navukli su na sebe najveći Božji gnjev.

Timotejeva pohvala Crkvi

17Draga braćo, pošto smo zakratko bili odvojeni od vas (ali ne i srcem), vruće smo čeznuli za vama te smo pokušali doći da vas vidimo. 18Zaista smo nastojali doći k vama, ja Pavao i više puta, ali Sotona nas je spriječio. 19Tko će, na koncu, biti naša nada i radost, naš ponos i naša nagrada pred našim Gospodinom Isusom kada opet dođe? 20Vi ste naša slava i naša radost!