1 Wakorintho 3 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wakorintho 3:1-23

Kuhusu Mgawanyiko Katika Kanisa

13:1 1Kor 2:15; Rum 7:14; 1Kor 2:14; 14:20Ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo. 23:2 Ebr 5:12-14; 1Pet 2:2; Yn 16:12Naliwanywesha maziwa, wala si chakula kigumu, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa hicho chakula. Naam, hata sasa hamko tayari. 33:3 Rum 13:13; 1Kor 1:11; Gal 5:20Ninyi bado ni watu wa mwilini. Kwa kuwa bado kuna wivu na magombano miongoni mwenu, je, ninyi si watu wa mwilini? Je, si mwaendelea kama watu wa kawaida? 43:4 1Kor 1:12Kwa maana mmoja anaposema, “Mimi ni wa Paulo,” na mwingine, “Mimi ni wa Apolo,” je, ninyi si wanadamu wa kawaida?

53:5 Mdo 18:24; 1Kor 4:1; 2Kor 6:4; Efe 3:7; Kol 1:23-25Kwani, Apolo ni nani? Naye Paulo ni nani? Ni watumishi tu ambao kupitia wao mliamini, kama vile Bwana alivyompa kila mtu huduma yake. 63:6 Mdo 18:4-11; 1Kor 4:15; 9:1; 15:1Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliikuza. 73:7 2Kor 12:11; Gal 6:3Hivyo mwenye kupanda na mwenye kutia maji si kitu, bali Mungu peke yake ambaye huifanya ikue. 83:8 Za 18:20; 62:12; Mt 25:21; 1Kor 9:17Apandaye mbegu ana lengo sawa na yule atiaye maji na kila mmoja atalipwa kulingana na kazi yake. 93:9 Mk 16:20; 2Kor 6:1; 1The 2:2; Isa 61:3; Efe 2:20-22; 1Pet 5:5Kwa kuwa sisi tu watendakazi pamoja na Mungu. Ninyi ni shamba la Mungu, jengo la Mungu.

103:10 Rum 12:3; 15:20; Efe 2:20Kwa neema Mungu aliyonipa, niliweka msingi kama mjenzi stadi na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mmoja inampasa awe mwangalifu jinsi anavyojenga. 113:11 Isa 28:16; Efe 2:20Kwa maana hakuna mtu yeyote awezaye kuweka msingi mwingine wowote isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa, ambao ni Yesu Kristo. 12Kama mtu yeyote akijenga juu ya msingi huu kwa kutumia dhahabu, fedha, vito vya thamani, miti, majani au nyasi, 133:13 1Kor 4:5; 1:8; 2The 1:7-10; 2Tim 1:12-18; 4:8; Hes 31:22-23; Yer 23:28-29; Mal 3:3; 2The 1:7kazi yake itaonekana ilivyo, kwa kuwa Siku ile itaidhihirisha. Itadhihirishwa kwa moto, nao moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. 143:14 1Kor 3:8; 4:5Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu yake. 153:15 Yud 23Kama kazi kitateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini tu kama mtu aliyenusurika kwenye moto.

163:16 1Kor 6:9; 2Kor 6:16; Efe 2:21-22; Ebr 3:6; Rum 8:9Je, hamjui ya kwamba ninyi wenyewe ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17Kama mtu yeyote akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza; kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ndiyo hilo hekalu.

183:18 Isa 5:12; 1Kor 8:2; Gal 6:3; 1Kor 1:20Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima. 193:19 Rum 1:22; 1Kor 1:20-27; Ay 5:13Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kama ilivyoandikwa: “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao,” 203:20 Za 94:11tena, “Bwana anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.” 213:21 1Kor 4:6; Rum 8:32Hivyo basi, mtu asijivune kuhusu wanadamu! Vitu vyote ni vyenu, 223:22 1Kor 1:12; Rum 8:38ikiwa ni Paulo au Apolo au Kefa3:22 Yaani Petro. au dunia au uzima au mauti, au wakati uliopo au wakati ujao, haya yote ni yenu 233:23 1Kor 15:23; 2Kor 10:7; Gal 3:29na ninyi ni wa Kristo, naye Kristo ni wa Mungu.

King James Version

1 Corinthians 3:1-23

1And I, brethren, could not speak unto you as unto spiritual, but as unto carnal, even as unto babes in Christ. 2I have fed you with milk, and not with meat: for hitherto ye were not able to bear it, neither yet now are ye able.

3For ye are yet carnal: for whereas there is among you envying, and strife, and divisions, are ye not carnal, and walk as men? 4For while one saith, I am of Paul; and another, I am of Apollos; are ye not carnal? 5Who then is Paul, and who is Apollos, but ministers by whom ye believed, even as the Lord gave to every man? 6I have planted, Apollos watered; but God gave the increase. 7So then neither is he that planteth any thing, neither he that watereth; but God that giveth the increase. 8Now he that planteth and he that watereth are one: and every man shall receive his own reward according to his own labour. 9For we are labourers together with God: ye are God’s husbandry, ye are God’s building. 10According to the grace of God which is given unto me, as a wise masterbuilder, I have laid the foundation, and another buildeth thereon. But let every man take heed how he buildeth thereupon. 11For other foundation can no man lay than that is laid, which is Jesus Christ. 12Now if any man build upon this foundation gold, silver, precious stones, wood, hay, stubble; 13Every man’s work shall be made manifest: for the day shall declare it, because it shall be revealed by fire; and the fire shall try every man’s work of what sort it is. 14If any man’s work abide which he hath built thereupon, he shall receive a reward. 15If any man’s work shall be burned, he shall suffer loss: but he himself shall be saved; yet so as by fire. 16Know ye not that ye are the temple of God, and that the Spirit of God dwelleth in you? 17If any man defile the temple of God, him shall God destroy; for the temple of God is holy, which temple ye are.

18Let no man deceive himself. If any man among you seemeth to be wise in this world, let him become a fool, that he may be wise. 19For the wisdom of this world is foolishness with God. For it is written, He taketh the wise in their own craftiness. 20And again, The Lord knoweth the thoughts of the wise, that they are vain. 21Therefore let no man glory in men. For all things are yours; 22Whether Paul, or Apollos, or Cephas, or the world, or life, or death, or things present, or things to come; all are yours; 23And ye are Christ’s; and Christ is God’s.