1 Wakorintho 2 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wakorintho 2:1-16

Kumtangaza Kristo Aliyesulubiwa

12:1 1Kor 1:17; 2:4; 13; 2Kor 10:10; 11; 1Kor 1:6Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu. 22:2 Gal 6:14; 1Kor 1:23Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa. 32:3 Mdo 18:1-18; 1Kor 4:10; 9:22; 2Kor 11:29-30; 12:5-10; 13:9; 7:15Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana. 42:4 Rum 15:13; 1Kor 2:1; 1:17; 2Pet 1:16Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho 5ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.

Hekima Ya Kweli Itokayo Kwa Mungu

62:6 Efe 4:13; Flp 3:15; Kol 4:12; Ebr 5:14; 6:1; Yak 1:4; 1Kor 1:20; Za 146:4Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. 72:7 Rum 16:25; Efe 3:5, 9; Kol 1:26; 2Tim 1:9Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 82:8 1Kor 1:20; Za 24:7; Mdo 7:2; Yak 2:1Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu. 92:9 Isa 64:4; 65:17Lakini ni kama ilivyoandikwa:

“Hakuna jicho limepata kuona,

wala sikio limepata kusikia,

wala hayakuingia moyoni wowote,

yale Mungu amewaandalia

wale wampendao”:

102:10 Mt 13:11; 2Kor 12:1-7; Gal 1:12; 2:2; Efe 3:3-5; Yn 14:26Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake.

Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu. 112:11 Yer 17:9; Mit 20:27Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 122:12 Rum 8:15; 1Kor 1:20-27; Yak 2:5Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. 132:13 1Kor 1:17Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa maneno ya kiroho. 142:14 Yn 14:17; 1Kor 3:1Mtu ambaye hana Roho hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni. 152:15 1Kor 3:1; Gal 6:1Mtu wa kiroho hubainisha mambo yote, lakini yeye mwenyewe habainishwi na mtu yeyote.

162:16 Isa 40:13; Rum 11:34; Yn 15:15“Kwa maana ni nani aliyefahamu mawazo ya Bwana

ili apate kumfundisha?”

Lakini sisi tunayo mawazo ya Kristo.

King James Version

1 Corinthians 2:1-16

1And I, brethren, when I came to you, came not with excellency of speech or of wisdom, declaring unto you the testimony of God. 2For I determined not to know any thing among you, save Jesus Christ, and him crucified. 3And I was with you in weakness, and in fear, and in much trembling. 4And my speech and my preaching was not with enticing words of man’s wisdom, but in demonstration of the Spirit and of power: 5That your faith should not stand in the wisdom of men, but in the power of God. 6Howbeit we speak wisdom among them that are perfect: yet not the wisdom of this world, nor of the princes of this world, that come to nought: 7But we speak the wisdom of God in a mystery, even the hidden wisdom, which God ordained before the world unto our glory: 8Which none of the princes of this world knew: for had they known it, they would not have crucified the Lord of glory. 9But as it is written, Eye hath not seen, nor ear heard, neither have entered into the heart of man, the things which God hath prepared for them that love him. 10But God hath revealed them unto us by his Spirit: for the Spirit searcheth all things, yea, the deep things of God. 11For what man knoweth the things of a man, save the spirit of man which is in him? even so the things of God knoweth no man, but the Spirit of God. 12Now we have received, not the spirit of the world, but the spirit which is of God; that we might know the things that are freely given to us of God. 13Which things also we speak, not in the words which man’s wisdom teacheth, but which the Holy Ghost teacheth; comparing spiritual things with spiritual. 14But the natural man receiveth not the things of the Spirit of God: for they are foolishness unto him: neither can he know them, because they are spiritually discerned. 15But he that is spiritual judgeth all things, yet he himself is judged of no man. 16For who hath known the mind of the Lord, that he may instruct him? But we have the mind of Christ.