1 Wakorintho 15 – NEN & SZ-PL

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wakorintho 15:1-58

Kufufuka Kwa Kristo

115:1 Isa 40:9; Rum 2:16; 1Kor 3:6Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. 215:2 Rum 1:16; 11:22Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

315:3 Gal 1:12; 1Kor 11:2; Isa 53:5; Yn 1:29; Gal 1:4; 1Pet 2:24; Mt 26:24; Lk 24:27; Mdo 17:2; 26:22; 23Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 415:4 Mt 27:59-61; Mdo 2:24; Mt 16:21; Yn 2:21-22ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko, 515:5 Lk 24:34-43; Mk 16:14na kwamba alimtokea Kefa,15:5 Yaani Petro. kisha akawatokea wale kumi na wawili. 615:6 Mt 9:24Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. 715:7 Mdo 15:13; Lk 24:33-37; Mdo 1:3-4Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote. 815:8 Mdo 9:3-6; 1Kor 9:1; Gal 1:16Mwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.

915:9 2Kor 12:11; Efe 3:8; 1Tim 1:15; Mdo 8:3; 1Kor 10:32Kwa maana mimi ndiye mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 1015:10 Rum 3:24; 12:3; 2Kor 11:23; Kol 1:29; Flp 2:13Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 1115:11 Gal 2:6Hivyo basi, kama ilikuwa mimi au wao, hili ndilo tunalohubiri, na hili ndilo mliloamini.

Ufufuo Wa Wafu

1215:12 Yn 11:24; Mdo 17:32; 23:8; 2Tim 2:18Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa. 1415:14 1The 4:14Tena ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. 1515:15 Mdo 2:24; 4:10, 33; 13:30Zaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi. 1615:16 1Kor 6:14Kwa kuwa kama wafu hawafufuliwi, basi hata Kristo hajafufuka. 1715:17 Rum 4:25Tena kama Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni batili; nanyi bado mko katika dhambi zenu. 1815:18 Mt 9:24Hivyo basi, wote waliolala katika Kristo wamepotea. 1915:19 1Kor 4:9Ikiwa tumaini letu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wote.

2015:20 1Pet 1:3; Mdo 26:23; Ufu 1:5; Mt 9:24Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala. 2115:21 Rum 5:12Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 2215:22 Rum 5:14-18; 1Kor 6:14Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai. 2315:23 1The 2:19; 1Kor 3:23Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja. 2415:24 Dan 2:44; 7:14; 2Pet 1:11; Rum 8:38Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. 2515:25 Isa 9:7; 52:7; Mt 22:44Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. 2615:26 2Tim 1:10; Ufu 20:14; 21:4Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti. 2715:27 Za 8:6; Mt 22:44; 28:18Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa. 2815:28 Flp 3:21; 1Kor 3:23Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.

29Basi kama hakuna ufufuo, watafanyaje wale wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa ajili yao? 3015:30 2Kor 11:26Nasi kwa upande wetu kwa nini tunajihatarisha kila saa? 3115:31 Rum 8:36Kama majivuno yangu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu ni kweli, ndugu zangu, ninakufa kila siku. 3215:32 2Kor 1:8; Mdo 18:19; Isa 22:13; Lk 12:19Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi,

“Tuleni na kunywa,

kwa kuwa kesho tutakufa.”

3315:33 1Kor 6:9; Mit 22:24-25Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 3415:34 Gal 4:8; 1Kor 4:8; 4:14Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.

Mwili Wa Ufufuo

3515:35 Rum 9:19; Eze 37:3Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?” 3615:36 Lk 11:40; 12:20; Yn 12:24Ninyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. 37Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine. 3815:38 Mwa 1:11Lakini Mungu huipa mbegu umbo kama alivyokusudia mwenyewe na kila aina ya mbegu huipa umbo lake. 39Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine, kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari wa ile miili ya mbinguni ni wa aina moja na fahari wa ile miili ya duniani ni wa aina nyingine. 4115:41 Za 19:4-6; 8:1-3Jua lina fahari ya aina moja, mwezi nao una fahari yake na nyota pia, nazo nyota hutofautiana katika fahari.

4215:42 Dan 12:3; Mt 13:43Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika, 4315:43 Flp 3:21; Kol 3:4unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu, 4415:44 1Kor 15:50unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho.

Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 4515:45 Mwa 2:7; Rum 5:14; Yn 5:21; 6:57-58; Rum 8:2Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. 46Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. 47Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 4815:48 Flp 3:20-21Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 4915:49 Mwa 5:3; Rum 8:29Kama vile tulivyochukua mfano wa mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni.

5015:50 Efe 6:12; Ebr 2:14; Mt 25:34Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika. 5115:51 1Kor 13:2; 14:2; Mt 9:24; 2Kor 5:4; Flp 3:21Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 5215:52 Mt 24:31; Yn 5:25ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 5315:53 2Kor 5:2-4Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa. 5415:54 Isa 25:8; Ebr 2:14; Ufu 20:14Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

5515:55 Hos 13:14; Isa 25:8“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?

Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

5615:56 Rum 5:12; 14:15Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 5715:57 2Kor 2:14; Rum 8:37; Ebr 2:14-15Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

5815:58 1Kor 16:10; Isa 65:23Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.

Słowo Życia

1 Koryntian 15:1-58

Zmartwychwstanie Chrystusa

1Przyjaciele, chciałbym wam teraz przypomnieć dobrą nowinę, którą przekazałem wam, którą przyjęliście, której jesteście wierni, 2i która daje wam zbawienie—o ile trzymacie się tego, co wam głosiłem. Chyba że uwierzyliście na próżno…

3Na samym początku przekazałem wam to, co sam przyjąłem, mianowicie że Chrystus umarł za nasze grzechy—zgodnie z zapowiedziami Pisma, 4że został pogrzebany, że trzeciego dnia zmartwychwstał—również zgodnie z Pismem, 5i że ukazał się Piotrowi, a następnie pozostałym Dwunastu. 6Później widziało Go równocześnie pięciuset wierzących, z których większość jeszcze żyje—niektórzy jednak już zmarli. 7Potem Jezus ukazał się Jakubowi i wszystkim innym apostołom. 8Na samym końcu, jakby najmniej godnemu, ukazał się także mnie. 9Jestem bowiem najmniejszym z apostołów i nie powinienem nawet używać tego tytułu, gdyż prześladowałem kościół Boga. 10Tylko dzięki Jego łasce jestem więc tym, kim jestem—a łaska ta przyniosła owoce. Trudziłem się o wiele bardziej niż inni—oczywiście nie ja sam, zawsze bowiem Bóg wspierał mnie swoją łaską. 11Zresztą czy ja, czy inni, i tak głosimy tę samą dobrą nowinę, w którą wy uwierzyliście.

Zmartwychwstanie zmarłych

12Skoro więc głosimy zmartwychwstanie Chrystusa, to dlaczego niektórzy z was twierdzą, że coś takiego jak zmartwychwstanie w ogóle nie istnieje? 13Jeśli nie istnieje, to i Chrystus nie zmartwychwstał. 14A jeśli On nie zmartwychwstał, to głoszenie dobrej nowiny nie ma sensu—i również wasza wiara jest pozbawiona podstaw. 15W takiej sytuacji okazujemy się fałszywymi świadkami, bo twierdzimy, że Bóg ożywił z martwych Chrystusa. A nie mógł tego zrobić, skoro umarli nie zmartwychwstają. 16Jeśli umarli nie mogą powstać z martwych, Chrystus też nie zmartwychwstał. 17A jeśli On nie ożył, niepotrzebnie Mu uwierzyliście i, co za tym idzie, nadal jesteście obciążeni waszymi grzechami. 18Ci zaś wierzący, którzy już zmarli, poszli na potępienie. 19Jeżeli nasza nadzieja w Chrystusie dotyczy tylko tego ziemskiego życia, to jesteśmy najbardziej godni pożałowania ze wszystkich ludzi.

20Lecz Chrystus naprawdę zmartwychwstał—jako pierwszy z umarłych! 21Skoro śmierć przyszła na świat z powodu człowieka—Adama, to również zmartwychwstanie przyjdzie przez Człowieka—Chrystusa. 22Z powodu Adama wszyscy umierają, ale dzięki Chrystusowi wszyscy zmartwychwstaną. 23Każdy we właściwym czasie: najpierw powstał z martwych Chrystus, w czasie Jego powrotu ożyją natomiast ci, którzy do Niego należą. 24Potem nastąpi koniec i Chrystus przekaże królestwo Bogu Ojcu, a wszelkie władze i potęgi przestaną istnieć. 25Chrystus ma bowiem panować do czasu, aż wszyscy Jego przeciwnicy padną u Jego stóp. 26Ostatnim pokonanym wrogiem będzie śmierć. 27Bóg poddał bowiem wszystko władzy Chrystusa—oczywiście wszystko oprócz siebie samego, bo to On jest Tym, który poddał wszystko Chrystusowi. 28Gdy więc już wszystko zostanie poddane Synowi Bożemu, wtedy także On przekaże władzę Ojcu, który dał Mu wszystko we władanie. Odtąd Bóg będzie obecny we wszystkich i będzie panował nad wszystkim.

29Co robią ci, którzy przyjmują chrzest za zmarłych? Jeśli umarli w ogóle nie powstaną do życia, to jaki jest sens tego, co robią? 30A my? Po co ciągle narażamy się na niebezpieczeństwa? 31Przyjaciele—moja dumo w Chrystusie Jezusie, naszym Panu!—wiecie przecież, że codziennie ryzykuję życie. 32Po co, jak niewolnik na arenie, walczyłem z dzikimi bestiami w Efezie? Jeśli umarli nie zmartwychwstają, to:

„Jedzmy i pijmy,

bo jutro czeka nas śmierć!”

33Nie dajcie się oszukać! „Złe towarzystwo prowadzi do rozwiązłości”. 34Opamiętajcie się i przestańcie grzeszyć! Niektórzy z was w ogóle nie znają Boga! Mówię to, aby was zawstydzić.

Nowe ciała

35Ktoś może zapytać: „Jak umarli zmartwychwstaną? W jakich ciałach?”. 36Niemądry człowieku! Żeby jakaś roślina wyrosła, najpierw musi zginąć ziarno, które zostało rzucone w ziemię. 37Nie siejesz przecież tego, co ma wyrosnąć, ale rzucasz w ziemię ziarno tej rośliny, na przykład pszenicy lub czegoś innego. 38A Bóg, zgodnie ze swoją wolą, daje mu nową postać—każdemu rodzajowi ziarna inną. 39Dotyczy to nie tylko roślin. Inne ciała mają ludzie, inne zwierzęta, inne ptaki, a jeszcze inne ryby. 40Są ciała niebieskie i ciała ziemskie—każde z nich ma inne piękno. 41Słońce ma swój blask, inne światło daje jednak księżyc, a jeszcze inne gwiazdy. A nawet one różnią się między sobą.

42Podobnie jest ze zmartwychwstaniem. Posiane jest ciało śmiertelne, a zmartwychwstanie ciało nieśmiertelne. 43Posiane jest ciało materialne—słabe i sprawiające wiele kłopotów, 44a zmartwychwstanie ciało duchowe—pełne mocy i wspaniałe! Istnieją bowiem ciała materialne i ciała duchowe.

45Pismo mówi: „Adam, pierwszy człowiek, stał się istotą mającą życie”. Ale ostatni „Adam”—czyli Jezus—stał się duchem dającym życie! 46Najpierw przyszedł ten, który miał ciało ziemskie. Potem dopiero przyszedł Ten, który ma ciało duchowe. 47Adam, pierwszy człowiek, przyszedł z ziemi. Jezus, drugi Człowiek, przyszedł z nieba. 48Ci, którzy żyją na ziemi, mają ciało podobne do Adama, człowieka z ziemi. Ci jednak, którzy należą do nieba, otrzymają ciała podobne do Jezusa, Człowieka z nieba. 49Teraz jesteśmy podobni do ziemskiego Adama, ale będziemy podobni do niebiańskiego Chrystusa.

50Zapewniam was, przyjaciele, że nikt nie wejdzie do królestwa Bożego w ludzkim, śmiertelnym ciele—to, co jest doczesne, nie może bowiem stać się częścią tego, co jest wieczne. 51Pragnę wam jednak zdradzić wspaniałą tajemnicę: Nie wszyscy umrzemy, ale wszyscy otrzymamy nowe ciała. 52Stanie się to w jednej chwili, w mgnieniu oka, przy dźwięku ostatniej trąby. Gdy ona zabrzmi, zmarli powstaną do życia w nieśmiertelnych ciałach, a my, żywi, również otrzymamy nowe ciała. 53Bo to, co jest doczesne i śmiertelne, musi zostać zastąpione tym, co wieczne i nieśmiertelne. 54Gdy więc nasze doczesne i śmiertelne ciała przemienią się w ciała wieczne i nieśmiertelne, wypełnią się słowa Pisma:

„Zwycięstwo pochłonęło śmierć.

55Gdzie jest triumf śmierci?

Gdzie jest jej żądło?”.

56Żądłem, którym śmierć zaatakowała ludzi, jest grzech, a Prawo ujawniło siłę grzechu. 57Dziękujmy jednak Bogu za to, że posłał Jezusa Chrystusa, naszego Pana, i pozwolił nam odnieść zwycięstwo!

58Moi kochani przyjaciele, bądźcie wytrwali i nieugięci, nieustannie oddani pracy dla Pana. I pamiętajcie, że wasz wysiłek jest cenny w Jego oczach i nie pójdzie na marne.