1 Wakorintho 10 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wakorintho 10:1-33

Onyo Kutoka Historia Ya Waisraeli

110:1 Rum 11:25; Kut 13:21; Za 105:39; Kut 14:22-29; Za 66:6Ndugu zangu, sitaki mkose kufahamu ukweli huu kwamba baba zetu walikuwa wote chini ya wingu na kwamba wote walipita katikati ya bahari. 210:2 Rum 6:3Wote wakabatizwa kuwa wa Mose ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari. 310:3 Yn 6:31; Kut 16:15, 35; Neh 9:15, 20; Za 78:24Wote walikula chakula kile kile cha roho, 410:4 Kut 17:6; Hes 20:11; Za 78:15na wote wakanywa kile kile kinywaji cha roho, kwa maana walikunywa kutoka ule mwamba wa roho uliofuatana nao, nao ule mwamba ulikuwa Kristo. 510:5 Hes 14:29; Ebr 3:17; Yud 5Lakini Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo miili yao ilitapakaa jangwani.

610:6 1Kor 9:11; Hes 11:4, 34Basi mambo haya yalitokea kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. 710:7 Kut 32:4-19; 1Kor 9:14; Kut 32:6Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 810:8 Hes 25:1-9Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 910:9 Kut 17:2; Za 78:18; 95:9; 106:14; Hes 21:5-6Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 1010:10 Hes 16:41; 17:5, 10; 16:49; Kut 12:23; 1Nya 21:15; Ebr 11:28Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.

1110:11 Rum 4:24; 13:11; 1Kor 10:6; 1Pet 4:7Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. 1210:12 Rum 11:20; 2Kor 1:24Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 1310:13 1Kor 1:9; 2Pet 2:9Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

Karamu Za Sanamu Na Meza Ya Bwana

1410:14 Ebr 6:9; 1Pet 2:11; 1Yn 2:9; 5:21; Yud 3Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu. 15Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 1610:16 Mt 14:19; 26:26-28; 1Kor 11:25Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 1710:17 Rum 12:5; 1Kor 12:27Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.

1810:18 Law 7:6, 14, 15Waangalieni watu wa Israeli: Je, wale wote walao dhabihu si ni wale watendao kazi madhabahuni? 1910:19 1Kor 8:4; Rum 12:5; 1Kor 12:27Je, nina maana kwamba kafara iliyotolewa kwa sanamu ni kitu chenye maana yoyote? Au kwamba sanamu ni kitu chenye maana yoyote? 2010:20 Kum 32:17; Law 17:7; Za 107:37; Ufu 9:20La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani. 2110:21 2Kor 6:15-16; Kum 32:38; Mal 1:7, 12Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani pia. 2210:22 Kum 32:16, 21; 1Fal 14:22; Za 78:58; Yer 44:8; Mhu 6:10; Isa 45:9Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?

Fanyeni Yote Kwa Utukufu Wa Mungu

2310:23 1Kor 6:12“Vitu vyote ni halali,” lakini si vitu vyote vilivyo na faida. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vinavyojenga. 2410:24 Rum 15:1-2; 1Kor 13:5; Flp 2:4, 21Mtu yeyote asitafute yaliyo yake mwenyewe, bali kila mtu atafute yale yanayowafaa wengine.

2510:25 Mdo 10:15; 1Kor 8:7Kuleni chochote kinachouzwa sokoni, bila kuuliza swali lolote kwa ajili ya dhamiri. 2610:26 Za 24:1; Kut 9:29; 19:5; Ay 41:11; Za 50:12; 1Tim 4:4Kwa maana, “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.”

2710:27 Lk 10:7Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 2810:28 1Kor 8:7, 10-12; Kum 10:14Lakini kama mtu yeyote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri. 29Nina maana dhamiri ya huyo aliyekuambia, wala si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 3010:30 Rum 14:6; 1Tim 4:3, 4Kama nikila kwa shukrani, kwa nini nashutumiwa kwa kile ambacho kwa hicho ninamshukuru Mungu?

3110:31 Zek 14:21; Kol 3:17; 1Pet 4:11Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 3210:32 Mt 5:29; Mdo 24:16; 2Kor 6:3; 1Kor 11:16-22; 15:9; 1Tim 3:5Msiwe kikwazo kwa mtu yeyote, wawe Wayahudi au Wayunani, au kwa kanisa la Mungu, 3310:33 Rum 15:2; 1Kor 9:22; Rum 11:14kama hata mimi ninavyojaribu kumpendeza kila mtu kwa kila namna. Kwa maana sitafuti mema kwa ajili yangu mwenyewe bali kwa ajili ya wengi, ili waweze kuokolewa.

King James Version

1 Corinthians 10:1-33

1Moreover, brethren, I would not that ye should be ignorant, how that all our fathers were under the cloud, and all passed through the sea; 2And were all baptized unto Moses in the cloud and in the sea; 3And did all eat the same spiritual meat; 4And did all drink the same spiritual drink: for they drank of that spiritual Rock that followed them: and that Rock was Christ. 5But with many of them God was not well pleased: for they were overthrown in the wilderness. 6Now these things were our examples, to the intent we should not lust after evil things, as they also lusted. 7Neither be ye idolaters, as were some of them; as it is written, The people sat down to eat and drink, and rose up to play. 8Neither let us commit fornication, as some of them committed, and fell in one day three and twenty thousand. 9Neither let us tempt Christ, as some of them also tempted, and were destroyed of serpents. 10Neither murmur ye, as some of them also murmured, and were destroyed of the destroyer. 11Now all these things happened unto them for ensamples: and they are written for our admonition, upon whom the ends of the world are come. 12Wherefore let him that thinketh he standeth take heed lest he fall. 13There hath no temptation taken you but such as is common to man: but God is faithful, who will not suffer you to be tempted above that ye are able; but will with the temptation also make a way to escape, that ye may be able to bear it.

14Wherefore, my dearly beloved, flee from idolatry. 15I speak as to wise men; judge ye what I say. 16The cup of blessing which we bless, is it not the communion of the blood of Christ? The bread which we break, is it not the communion of the body of Christ? 17For we being many are one bread, and one body: for we are all partakers of that one bread. 18Behold Israel after the flesh: are not they which eat of the sacrifices partakers of the altar? 19What say I then? that the idol is any thing, or that which is offered in sacrifice to idols is any thing? 20But I say, that the things which the Gentiles sacrifice, they sacrifice to devils, and not to God: and I would not that ye should have fellowship with devils. 21Ye cannot drink the cup of the Lord, and the cup of devils: ye cannot be partakers of the Lord’s table, and of the table of devils. 22Do we provoke the Lord to jealousy? are we stronger than he? 23All things are lawful for me, but all things are not expedient: all things are lawful for me, but all things edify not. 24Let no man seek his own, but every man another’s wealth. 25Whatsoever is sold in the shambles, that eat, asking no question for conscience sake: 26For the earth is the Lord’s, and the fulness thereof. 27If any of them that believe not bid you to a feast, and ye be disposed to go; whatsoever is set before you, eat, asking no question for conscience sake. 28But if any man say unto you, This is offered in sacrifice unto idols, eat not for his sake that shewed it, and for conscience sake: for the earth is the Lord’s, and the fulness thereof: 29Conscience, I say, not thine own, but of the other: for why is my liberty judged of another man’s conscience? 30For if I by grace be a partaker, why am I evil spoken of for that for which I give thanks? 31Whether therefore ye eat, or drink, or whatsoever ye do, do all to the glory of God. 32Give none offence, neither to the Jews, nor to the Gentiles, nor to the church of God: 33Even as I please all men in all things, not seeking mine own profit, but the profit of many, that they may be saved.