1 Wafalme 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 6:1-38

Solomoni Ajenga Hekalu

(2 Nyakati 3)

16:1 Ezr 4:15; 5:17Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana.

2Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini,6:2 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27. upana wa dhiraa ishirini6:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na kimo cha dhiraa thelathini6:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. kwenda juu. 36:3 Ezr 3:10; Hag 2:3Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. 46:4 1Fal 6:36; Ezr 7:20; Isa 60:6; Za 68:29Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. 56:5 1Nya 29:2; Yer 27:18-22; Ezr 5:14Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. 66:6 Ezr 5:3Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano,6:6 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba.6:6 Dhiraa saba ni sawa na mita 3.15. Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu.

7Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika sauti yake katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa.

86:8 1Sam 9:10Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. 9Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha, akiliweka paa za boriti na mbao za mierezi. 106:10 Ezr 7:23; Yer 29:7; Law 1:9; Mwa 8:21; 1Tim 2:1-2Mfalme Solomoni akajenga vyumba vya pembeni kuzunguka Hekalu lote. Kimo cha kila kimoja kilikuwa dhiraa tano. Navyo vilikuwa vimeunganishwa na Hekalu kwa boriti za mierezi.

116:11 Kum 21:22-23; Es 2:23; Ezr 7:26; Dan 2:5Neno la Bwana likamjia Solomoni kusema: 126:12 Kut 20:24; Kum 12:11; 1Fal 9:3; 2Nya 7:16; Za 132:13“Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako. 136:13 Ay 5:12; Ezr 4:9; Za 9:16; 1Kor 3:19Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.”

146:14 Ezr 5:1; 7:1; Neh 2:1; Ezr 4:24Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha. 156:15 Zek 4:9Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari. 166:16 1Fal 8:63; 2Nya 7:15; Yn 10:22Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu. 176:17 2Sam 6:13; 1Nya 16:1-3; 2Nya 29:21; Hes 7:2-3; Ezr 8:25Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini.6:17 Dhiraa 40 ni sawa na mita 18. 186:18 1Nya 24:1; 23:6; Hes 3:6-9; 8:9-11Hekalu ndani ilikuwa ya mierezi iliyonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.

196:19 Kut 12:11; Hes 28:16Ndani ya Hekalu akatengeneza sehemu takatifu ya ndani, kwa ajili ya kuweka Sanduku la Agano la Bwana. 206:20 2Nya 30:15-17; 35:11; Kut 12:25; 2Nya 29:34Sehemu takatifu ya ndani ilikuwa na upana, urefu na kimo cha dhiraa ishirini ndani kwa ndani. Akaifunika ndani kwa dhahabu safi, pia akaifunika madhabahu ya mierezi vivyo hivyo. 216:21 Kut 12:48; Za 93:5Solomoni akaifunika sehemu ya ndani ya Hekalu kwa dhahabu safi, naye akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande moja hadi ule mwingine mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, ambako palifunikwa kwa dhahabu. 226:22 Kut 12:17; Mit 21:1; Ezr 1:1Basi akafunika sehemu yote ya ndani kwa dhahabu. Pia akafunika madhabahu yale yaliyokuwa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kwa dhahabu.

23Katika Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni, kila moja likiwa na dhiraa kumi6:23 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. kwenda juu. 24Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na bawa jingine dhiraa tano, hivyo urefu kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa jingine ulikuwa dhiraa kumi. 25Kerubi wa pili alikuwa na urefu wa dhiraa kumi pia, hivyo makerubi hao wawili walifanana kwa vipimo na kwa umbo. 26Kimo cha kila kerubi kilikuwa dhiraa kumi. 27Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba. 28Akafunika wale makerubi kwa dhahabu.

29Juu ya kuta zote zilizozunguka Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi zilizokatwa za makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua. 30Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu.

31Kwa ingilio la Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza milango ya mbao za mzeituni, zikiwa na miimo na vizingiti vyenye umbo la pembe tano. 32Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa. 33Kwa njia iyo hiyo akatengeneza miimo yenye pande nne ya miti ya mizeituni, kwa ajili ya ingilio la ukumbi mkubwa. 34Kulikuwa na milango miwili iliyoweza kukunjuka iliyotengenezwa kwa mbao za msunobari na kila mmoja ulikuwa na bawaba ambazo zingeuwezesha kujikunja kila kipande juu ya kingine. 35Akanakshi makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua juu yake na kufunika kwa dhahabu iliyonyooshwa vizuri juu ya michoro.

36Tena akajenga ua wa ndani safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa.

37Msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano. 38Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀上 6:1-38

建造聖殿

1所羅門在做以色列王的第四年二月,即西弗月,開始為耶和華建殿。那時正是以色列人離開埃及後第四百八十年。 2所羅門王為耶和華建造的殿長二十七米,寬九米,高十三米半。 3殿前的門廊和殿一樣寬九米,深四米半。 4殿有精緻的窗戶。 5靠殿牆、圍著外殿和內殿又造了三層廂房, 6底層寬二點二五米,中層寬二點七米,上層寬三點一米。廂房的橫樑都搭在殿牆突出的地方,免得插入殿牆。 7建殿的石頭都在採石場鑿好了,建殿的時候聽不到錘子、斧頭或其他鐵器的響聲。

8底層廂房的進口在殿的南面,沿著一道螺旋樓梯可以通到第二層和第三層。 9殿建成後,殿頂裝上香柏木的梁木和木板。 10靠著殿牆所造的廂房每一層高二點二五米,用香柏木的梁木與殿牆接連起來。

耶和華的約

11耶和華對所羅門說: 12「關於你所建的這殿,若你遵行我的律例,順從我的典章,謹守我的一切誡命,我必實現我對你父親大衛的應許。 13我必住在以色列人當中,不拋棄我的以色列子民。」

14所羅門建造的殿落成了。 15殿裡的牆壁和天花板都鋪上了香柏木,地面都鋪上了松木板。 16在殿的後部,從地面至天花板用香柏木板隔出長九米的內殿,就是至聖所。 17在至聖所外面是外殿,長十八米。 18殿內全部鋪上香柏木,不露一點石頭,香柏木上刻著野瓜和花朵的圖案。 19殿的至聖所用來安放耶和華的約櫃。 20至聖所長、寬和高都是九米,裡面全貼上純金,香柏木造的祭壇也包上純金。 21殿內全部貼上純金,至聖所前面有金鏈攔著。 22殿內都貼上純金,至聖所內的祭壇也都包上純金。

23至聖所裡面放著兩個橄欖木造的基路伯天使,各高四米半, 24各有兩個二點二五米長的翅膀,雙翅展開,兩翅尖相距四點五米。 25兩個基路伯的大小和形狀一模一樣, 26高度都是四點五米。 27他將兩個基路伯安在至聖所內,兩個基路伯展開翅膀,各有一個翅膀在至聖所的中央相接,另一個翅膀的尖端觸到牆壁。 28這兩個基路伯天使也包上金。

29內殿和外殿的牆壁都刻上基路伯天使、棕樹和花朵的圖案, 30地板是鋪金的。 31至聖所的門、門楣和門柱都是橄欖木造的,門柱呈五角形。 32兩扇用橄欖木造的門上都刻著基路伯天使、棕樹和花朵的圖案,並包上金。 33外殿的四角形門柱也是用橄欖木造的, 34兩扇門是松木造的,每一扇門都分為可折疊的兩片, 35上面刻著基路伯天使、棕樹和花朵的圖案,並包上金。 36內院的牆是由三層鑿好的石頭和一層香柏木建的。

37耶和華的殿在所羅門執政第四年的西弗月奠基, 38在他執政的第十一年的布勒月,即八月全部按規格建成,歷經七年。