1 Wafalme 22 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 22:1-53

Mikaya Anatabiri Dhidi Ya Ahabu

(2 Nyakati 18:2-27)

1Kwa miaka mitatu hapakuwa na vita kati ya Aramu na Israeli. 2Lakini katika mwaka wa tatu Yehoshafati mfalme wa Yuda akashuka kwenda kumwona mfalme wa Israeli. 322:3 Kum 4:43Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia maafisa wake, “Je, hamjui Ramoth-Gileadi ni mali yetu na bado hatufanyi chochote kuirudisha kwetu kutoka kwa mfalme wa Aramu?”

422:4 2Fal 3:7Kwa hiyo akamuuliza Yehoshafati, “Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?”

Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.” 522:5 Kut 33:7; Ay 38:2; 2Fal 3:11Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta shauri la Bwana.”

622:6 Amu 18:6Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, niende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?”

Wakajibu, “Naam, nenda, kwa kuwa Bwana ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”

722:7 Hes 27:21; 2Fal 3:11Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Bwana hapa ambaye tunaweza kumuuliza?”

822:8 Amo 5:10; Yer 23:17Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumuuliza shauri la Bwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.”

Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”

9Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.”

10Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, pamoja na manabii wote wakiwa wakitabiri mbele yao. 1122:11 Kum 33:17; Zek 1:18-21Wakati huu Sedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma, akatangaza, “Hivi ndivyo Bwana asemavyo, ‘Kwa hizi pembe utawapiga na kuwarudisha Waaramu nyuma mpaka wameangamizwa.’ ”

12Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Bwana ataitia mkononi mwa mfalme.”

13Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”

1422:14 Hes 22:18Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, nitamwambia kile tu Bwana atakachoniambia.”

15Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?”

Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa Bwana atawatia mkononi mwa mfalme.”

16Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu chochote ila kweli tu kwa jina la Bwana?”

1722:17 Mt 9:36Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Bwana akasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”

18Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu, bali mabaya tu?”

1922:19 Isa 6:1; Dan 7:9; Ay 1:6Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto. 20Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’

“Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. 21Mwishoni, pepo mchafu akajitokeza, akasimama mbele za Bwana na kusema, ‘Nitamshawishi.’

2222:22 Amu 9:23; 2The 2:11Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’

“Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’

Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’

2322:23 Eze 14:9; Kum 31:29“Kwa hiyo sasa Bwana ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Bwana ameamuru maafa kwa ajili yako.”

24Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Bwana alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”

2522:25 1Fal 20:30Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.”

26Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme. 2722:27 2Nya 16:10; Ebr 11:36Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ”

2822:28 Kum 18:22Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi Bwana hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”

Ahabu Auawa Ramoth-Gileadi

(2 Nyakati 18:28-34)

29Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi. 3022:30 1Sam 28:8Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani.

3122:31 Mwa 10:22; 2Sam 10:19Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” 32Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, 33wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli, nao wakaacha kumfuatilia.

3422:34 2Fal 9:24; 2Nya 35:23Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma. Mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.” 35Vita vikaendelea mchana kutwa, naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari kuelekea Waaramu. Damu kutoka kwenye jeraha lake ikachuruzika ndani ya gari na jioni yake akafa. 36Jua lilipokuwa linazama, mbiu ikaenea katika jeshi lote: “Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake!”

37Basi mfalme akafa na akaletwa Samaria, nao wakamzika huko. 3822:38 1Fal 21:19Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la Bwana lilivyokuwa limesema.

3922:39 Za 45:8; Amo 3:15Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kupambwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea maboma, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 40Ahabu akalala pamoja na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Yehoshafati Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 20:31–21:1)

41Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme wa Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli. 42Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka ishirini na mitano. Jina la mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi. 4322:43 2Nya 17:3; 1Fal 3:2Katika kila jambo alitembea katika njia za Asa baba yake wala hakwenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. 44Yehoshafati pia alikuwa na amani na mfalme wa Israeli.

45Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, mafanikio aliyokuwa nayo na uhodari wake katika vita, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 4622:46 Kum 23:17Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa. 4722:47 2Fal 3:9; 8:20Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye alitawala.

4822:48 1Fal 9:26; Hes 33:35Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara22:48 Au: za Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16; 60:9). ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Esion-Geberi. 49Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa.

50Kisha Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.

Ahazia Mfalme Wa Israeli

51Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili. 5222:52 1Fal 15:26Akafanya maovu machoni mwa Bwana kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi. 5322:53 Amu 2:11; 1Fal 21:25Alimtumikia na kumwabudu Baali na kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀上 22:1-53

米該雅先知警告亞哈王

1亞蘭以色列之間三年無戰事。 2第三年,猶大約沙法來見以色列亞哈3以色列王對臣僕說:「你們都知道基列拉末是我們的領土,我們豈能坐視不理,不從亞蘭王手中奪回來呢?」 4他問約沙法:「你願意跟我一起去攻打基列拉末嗎?」約沙法回答說:「你我不分彼此,我的民就是你的民,我的馬就是你的馬。」 5約沙法又對以色列王說:「你要先求問耶和華。」

6於是,以色列王就召來了大約四百名先知,問他們:「我可以去攻打基列拉末嗎?」他們說:「可以去,主必把那城交在王手中。」 7約沙法問:「這裡沒有耶和華的先知供我們求問嗎?」 8以色列王回答說:「這裡還有一個人,是音拉的兒子米該雅,我們可以託他求問耶和華。可是我厭惡他,因為他給我的預言都是有凶無吉。」約沙法說:「王不要這樣說。」 9以色列王召來一名內侍,說:「你快把音拉的兒子米該雅帶來。」 10以色列王和猶大約沙法撒瑪利亞城門前的麥場,身穿朝服,坐在寶座上,眾先知都在他們面前說預言。 11基拿拿的兒子西底迦造了兩隻鐵角,說:「耶和華這樣說,『你必用這鐵角牴亞蘭人,直到毀滅他們。』」 12所有的先知也都預言說:「去攻打基列拉末吧,一定得勝,耶和華必將那城交在王的手中。」

13去召米該雅的使者對米該雅說:「眾先知都異口同聲地向王說吉言,你就像他們一樣說些吉言吧。」 14米該雅回答說:「我憑永活的耶和華起誓,耶和華對我說什麼,我就說什麼。」 15米該雅來到以色列王面前,王就問他:「米該雅啊,我可不可以去攻打基列拉末?」米該雅回答說:「上去攻打吧,一定得勝,耶和華必將那城交在王手中。」 16王卻說:「我要囑咐你多少次,你才肯奉耶和華的名對我說實話呢?」 17米該雅說:「我看見以色列人四散在山上,好像沒有牧人的羊群一樣。耶和華說,『這些人沒有主人,讓他們各自平安地回家去吧。』」 18以色列王對約沙法說:「我不是告訴過你嗎?他給我的預言都是有凶無吉。」 19米該雅說:「你要聽耶和華的話。我看見耶和華坐在寶座上,眾天軍侍立在祂左右。 20耶和華說,『誰願意去引誘亞哈基列拉末去送死呢?』眾天軍議論紛紛。 21後來,有一個靈站出來對耶和華說他願意去。 22耶和華問他用什麼方法,他說,『我要做謊言之靈,進入他眾先知的口中。』耶和華說,『你必能成功,就這樣做吧。』 23現在,耶和華已經把謊言之靈放進這些先知口中,耶和華已決意降禍給你。」

24基拿拿的兒子西底迦聽了米該雅的話就上前打他的臉,說:「耶和華的靈怎會離開我向你說話呢?」 25米該雅說:「你躲進密室的那天就知道了。」 26以色列王下令說:「把米該雅交給亞們總督和約阿施王子, 27告訴他們,『王說,要把這人關在監牢,只給他一些餅和水,直到我平安地回來。』」 28米該雅說:「如果你能夠平安地回來,耶和華就沒有藉著我說話。」他又說:「眾民啊,你們都記住我的話。」

亞哈之死

29以色列王和猶大約沙法出兵攻打基列拉末30以色列王對約沙法說:「我要改裝上陣,你就穿王袍吧。」以色列王就改裝上陣。 31亞蘭王已經吩咐他的三十二名戰車長不要跟對方的大小軍兵交鋒,只攻擊以色列王。 32戰車長看見約沙法,以為他一定是以色列王,便轉過來攻擊他。約沙法高聲喊叫, 33戰車長見他不是以色列王,便不再追殺他。 34有人隨手放了一箭,射進了以色列王的鎧甲縫中。王對駕車的說:「調轉車頭拉我離開戰場吧,我受了重傷。」 35那天的戰事非常激烈,亞哈王被人扶著站在車上,迎戰亞蘭人。到了黃昏,王就死了,車上流滿了血。 36太陽快要下山的時候,以色列軍中傳出號令,叫人各回本鄉本城。

37王死後,他們把王的屍體運回撒瑪利亞安葬, 38並在撒瑪利亞妓女洗浴的池邊洗他的戰車,有狗來舔他的血,正如耶和華所言。 39亞哈其他的事,他的一切所作所為和他建造的象牙宮及各城邑,都記在以色列的列王史上。 40亞哈與祖先同眠後,他兒子亞哈謝繼位。

約沙法做猶大王

41亞哈以色列王第四年,亞撒的兒子約沙法登基做猶大王。 42約沙法三十五歲登基,在耶路撒冷執政二十五年。他母親叫阿蘇巴,是示利希的女兒。 43約沙法事事效法他父親亞撒,不偏不離,做耶和華視為正的事。但他沒有拆毀邱壇,百姓仍然在那裡獻祭燒香。 44約沙法以色列王修好。

45約沙法其他的事,包括他的功業和戰績,都記在猶大的列王史上。 46約沙法除掉了他父親亞撒時代遺留的男廟妓。 47那時以東沒有王,由總督治理。 48約沙法又建造了一批他施船,要到俄斐去運載黃金,可是沒有成行,因為船隻在以旬·迦別失事了。 49後來,亞哈的兒子亞哈謝請求約沙法讓他的人跟約沙法的人一起出海,但約沙法拒絕了。 50約沙法與祖先同眠後葬在大衛城他的祖墳裡。他兒子約蘭繼位。

亞哈謝做以色列王

51猶大約沙法執政第十七年,亞哈的兒子亞哈謝撒瑪利亞登基做以色列王,執政兩年。 52他做耶和華視為惡的事,步他父母的後塵,效法使以色列人陷入罪中的尼八之子耶羅波安53他像他父親一樣供奉、祭拜巴力,惹以色列的上帝耶和華發怒。