1 Wafalme 20 – NEN & AKCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 20:1-43

Ben-Hadadi Aishambulia Samaria

120:1 1Fal 15:18; 13:32Wakati huu, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira kwa jeshi Samaria na kuishambulia. 2Akawatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: 3‘Fedha yako na dhahabu ni yangu, nao wake zako walio wazuri sana na watoto ni wangu.’ ”

4Mfalme wa Israeli akajibu, “Iwe kama usemavyo, bwana wangu mfalme. Mimi na vyote nilivyo navyo ni mali yako.”

5Wale wajumbe wakaja tena na kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: ‘Nimetuma kutaka fedha yako na dhahabu, wake zako na watoto wako. 6Lakini kesho wakati kama huu, nitawatuma maafisa wangu kukagua jumba lako la kifalme na nyumba za maafisa wako. Watatwaa kitu unachokithamini nao watakichukua.’ ”

720:7 1Sam 11:3; 2Fal 5:7Mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi na akawaambia, “Tazama jinsi mtu huyu anavyochokoza! Wakati alipotuma apelekewe wake zangu na watoto wangu, fedha zangu na dhahabu yangu, sikumkatalia.”

8Wazee na watu wote wakajibu, “Usimsikilize, wala usiyakubali matakwa yake.”

9Kwa hiyo akawajibu wajumbe wa Ben-Hadadi, “Mwambieni bwana wangu mfalme, ‘Mtumishi wako atafanya yote uliyoyadai mwanzoni, lakini dai hili la sasa siwezi kulitekeleza.’ ” Wakaondoka na kupeleka jibu kwa Ben-Hadadi.

1020:10 2Sam 22:43Kisha Ben-Hadadi akatuma ujumbe mwingine kwa Ahabu, kusema “Miungu iniletee maafa, tena makubwa zaidi, ikiwa vumbi la Samaria litatosheleza konzi moja ya kila mtu ya wale wafuatanao nami.”

1120:11 Mit 27:1; Amo 2:14Mfalme wa Israeli akajibu, “Mwambieni, ‘Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ ”

1220:12 1Fal 16:9; 20:13Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati ambapo yeye na wafalme walikuwa wanakunywa katika mahema yao, na akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kuushambulia mji.

Ahabu Amshinda Ben-Hadadi

1320:13 Amu 6:8; Kut 6:7Wakati ule ule nabii akamjia Ahabu mfalme wa Israeli na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Je, unaona jeshi hili kubwa? Nitalitia mkononi mwako leo, nawe ndipo utajua kwamba mimi ndimi Bwana.’ ”

1420:14 Amu 1:1Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?”

Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ”

Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?”

Nabii akamjibu, “Ni wewe.”

15Kwa hiyo Ahabu akawaita maafisa vijana majemadari wa majimbo, wanaume 232. Kisha akawakusanya Waisraeli wote waliobaki, jumla yao 7,000. 1620:16 1Fal 16:9Wakaondoka wakati wa adhuhuri, Ben-Hadadi na wale wafalme thelathini na wawili walioungana naye walipokuwa katika mahema yao wakilewa. 17Maafisa vijana majemadari wa majimbo waliondoka kwanza.

Wakati huu Ben-Hadadi alikuwa amewatuma wapelelezi, ambao walileta taarifa kusema kwamba, “Askari wanasonga mbele kutoka Samaria.”

18Akasema, “Ikiwa wamekuja kwa amani, wakamate wakiwa hai; ikiwa wamekuja kwa vita, wakamate wakiwa hai.”

19Wale maafisa vijana majemadari wa majimbo wakatoka nje ya mji jeshi likiwa nyuma yao, 20kila mmoja akamuua adui yake. Hii ilisababisha Waaramu kukimbia, huku Waisraeli wakiwafuatia. Lakini Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akatoroka akiwa amepanda farasi wake pamoja na baadhi ya wapanda farasi wake. 21Mfalme wa Israeli akasonga mbele na kushinda farasi na magari ya vita na kusababisha hasara kubwa kwa Waaramu.

2220:22 2Sam 11:1Baadaye nabii akaja kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Jiandae vizuri ufikirie la kufanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Aramu atakuja kukushambulia tena.”

23Wakati ule ule, maafisa wa mfalme wa Aramu wakamshauri, wakamwambia, “Miungu yao ni miungu ya vilimani. Ndiyo sababu walikuwa na nguvu sana kutuzidi. Lakini kama tukipigana nao katika nchi tambarare, hakika tutawashinda. 24Fanya hivi: Waondoe hao wafalme wote thelathini na wawili kutoka nafasi zao na uweke maafisa wengine mahali pao. 25Ni lazima pia uandae jeshi jingine kama lile ulilopoteza, farasi kwa farasi, gari la vita kwa gari la vita, ili tuweze kupigana na Israeli katika nchi tambarare. Kisha kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.” Akakubaliana nao naye akashughulika ipasavyo.

2620:26 2Fal 13:17Mwaka uliofuata, majira kama hayo, Ben-Hadadi akawakusanya Waaramu mpaka Afeki kupigana dhidi ya Israeli. 2720:27 Amu 6:6; 1Sam 13:6Baada ya Waisraeli kukusanywa na kupewa mahitaji, walikwenda kukabiliana nao. Waisraeli wakapiga kambi mkabala nao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, wakati Waaramu walienea katika nchi yote.

2820:28 Kut 6:7; Yer 16:19-21Mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyo Bwana asemavyo: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiri Bwana ni Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitatia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimi Bwana.’ ”

29Kwa siku saba walipiga kambi wakitazamana na siku ya saba vita vikaanza. Waisraeli wakawajeruhi askari wa miguu wa Waaramu 100,000 kwa siku moja. 3020:30 1Fal 22:25; Za 62:4Waliobaki wakatorokea katika mji wa Afeki, mahali ambapo watu 27,000 waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi akakimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani.

3120:31 Ay 41:3; Mwa 37:34Maafisa wake wakamwambia, “Tazama, tumesikia kwamba wafalme wa nyumba ya Israeli wana huruma. Twendeni kwa mfalme wa Israeli tukiwa tumevaa nguo za gunia viunoni mwetu na kamba kuzunguka vichwa vyetu. Huenda akakuacha hai.”

32Wakiwa wamevaa nguo za gunia viunoni mwao na kamba kuzunguka vichwa vyao, walikwenda kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Mtumishi wako Ben-Hadadi anasema: ‘Tafadhali, naomba uniache hai.’ ”

Mfalme akajibu, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.”

33Wale watu wakalipokea jambo lile kama dalili nzuri nao wakawa wepesi kulichukua neno lake wakisema, “Ndiyo, yeye ni ndugu yako Ben-Hadadi!”

Mfalme akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ikawa Ben-Hadadi alipokuja, Ahabu akampandisha katika gari lake la vita.

Ben-Hadadi akajitolea, akisema, 3420:34 1Fal 15:20; Kut 23:32“Nitairudisha ile miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Unaweza kuweka maeneo yako ya soko katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya huko Samaria.”

Ahabu akasema, “Katika misingi ya mkataba, nitakuachilia huru.” Kwa hiyo akaweka mkataba naye, akamruhusu aende zake.

Nabii Amlaumu Ahabu

3520:35 1Sam 10:5; 1Fal 13:21Kwa neno la Bwana, mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake, “Nipige kwa silaha yako,” lakini yule mtu akakataa.

3620:36 1Fal 13:24Kwa hiyo yule nabii akasema, “Kwa sababu hukumtii Bwana, mara tu tutakapoachana utauawa na simba.” Na baada ya yule mtu kuondoka, simba akatokea na kumuua.

37Nabii akamkuta mtu mwingine na kumwambia, “Nipige tafadhali.” Kisha yule mtu akampiga na kumjeruhi. 38Ndipo nabii akaenda na kusimama barabarani akimsubiri mfalme. Akajibadilisha kwa kushusha kitambaa cha kichwani mwake hadi kwenye macho. 3920:39 Yos 2:14Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alikwenda vitani wakati vita vilipopamba moto, mtu mmoja akanijia na mateka akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Kama akitoroka itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama vipande 3,000 vya fedha.’ 4020:40 2Sam 12:5Wakati mtumishi wako alipokuwa na shughuli nyingi hapa na pale, yule mtu akatoweka.”

Mfalme wa Israeli akasema, “Hiyo ndiyo hukumu yako. Wewe umeitaja mwenyewe.”

41Kisha yule nabii akajifunua macho yake haraka, na mfalme wa Israeli akamtambua kama mmoja wa manabii. 4220:42 2Sam 12:7; Yer 48:10Akamwambia mfalme, “Hivi ndivyo Bwana asemavyo: ‘Umemwacha huru mtu niliyekusudia afe. Kwa hiyo ni uhai wako kwa uhai wake, watu wako kwa watu wake.’ ” 4320:43 1Fal 21:4Kwa uchungu na hasira, mfalme wa Israeli akaenda kwenye jumba lake la kifalme huko Samaria.

Akuapem Twi Contemporary Bible

1 Ahemfo 20:1-43

Ben-Hadad Tow Hyɛ Samaria So

1Aramhene Ben-Hadad boaboaa nʼakofo nyinaa ano, a nteaseɛnam ne apɔnkɔ a wɔyɛ ahemfo aboafo aduasa abien de ka ne ho. Wokotuaa Israel kuropɔn Samaria ano, tow hyɛɛ so. 2Ben-Hadad somaa abɔfo kɔɔ kurow no mu, sɛ wɔnkɔka nkyerɛ ɔhene Ahab se, “Ben-Hadad se, 3‘Mo dwetɛ ne mo sikakɔkɔɔ yɛ me de. Saa ara na mo yerenom ne mo mma mu apapa no nso yɛ me de.’ ”

4Ahab buae se, “Mate, me wura! Nea mewɔ nyinaa yɛ wo de.”

5Ankyɛ biara Ben-Hadad abɔfo san baa bio bɛkae se, “Ben-Hadad se, ‘Maka dedaw sɛ momfa mo dwetɛ, sikakɔkɔɔ, mo yerenom ne mo mma mma me. 6Ɔkyena sesɛɛ, mɛsoma me mpanyimfo, na wɔabɛhwehwɛ mo ahemfi ne mo nkurɔfo afi. Na biribiara a ɛsom bo ma mo no, wɔbɛfa de akɔ.’ ”

7Na Ahab frɛɛ asase no so ntuanofo no nyinaa, ka kyerɛɛ wɔn se, “Monhwɛ sɛnea saa ɔbarima yi pɛ sɛ ɔde ɔhaw ba. Mapene so dedaw sɛ mede me yerenom, me mma, me dwetɛ ne me sikakɔkɔɔ bɛma no.”

8Ntuanofo ne nnipa no nyinaa kae se, “Ntie no, na nnye nʼabisade no nto mu.”

9Enti Ahab ka kyerɛɛ abɔfo a wofi Ben-Hadad nkyɛn bae no se, “Monkɔka saa asɛm yi nkyerɛ me wura ɔhene se, ‘Biribiara a obisaa kan no de, mede bɛma no. Na nea obisaa no akyiri yi de, merentumi mfa mma no.’ ” Enti Ben-Hadad abɔfo no san kɔbɔɔ no amanneɛ.

10Na Ben-Hadad soma kɔka kyerɛɛ Ahab se, “Sɛ mansɛe Samaria pasaa, na emu mfutuma dodow bi ka a ɛbɛboro asraafo no mu biara nsa ma a, anyame no ntwe mʼaso nea ɛyɛ den.”

11Israelhene nso soma ma wɔkɔka kyerɛɛ no se, “Ɛnsɛ sɛ ɔkofo kɛse a ɔrefa nʼafoa akɔ akono tu ne ho sɛ ɔkofo kɛse a wadi nkonim dedaw.”

12Ahab mmuae yi duu Ben-Hadad ne ahemfo a wɔaka no asom bere a na wɔrenom nsa wɔ wɔn ntamadan mu. Ɔhyɛɛ ne mmarima no se, “Munsiesie mo ho nkɔko.” Enti wosiesiee wɔn ho sɛ wɔrekɔtow ahyɛ kuropɔn no so.

Ahab Di Ben-Hadad So Nkonim

13Na odiyifo bi behuu ɔhene Ahab ka kyerɛɛ no se, “Sɛnea Awurade se ni, ‘Wuhu saa atamfo dɔm yi? Nnɛ, mede wɔn bɛhyɛ wo nsa. Na wubehu sɛ mene Awurade.’ ”

14Ahab bisae se, “Na dɛn na ɔbɛyɛ no?” Na odiyifo no buae se, “Sɛnea Awurade se ni, ‘Asraafo so asahene a wotuatua amansin ano no na wɔbɛyɛ.’ ”

Ahab bisae se, “Enti yenni kan ntow nhyɛ wɔn so ana?”

Odiyifo no buae se, “Yiw.”

15Enti Ahab boaboaa asraafo so asahene nkumaa ahannu aduasa abien wɔhyehyɛ amansin asahene ase ano. Afei, ɔfrɛɛ Israel akofo a wɔaka a wɔn nyinaa dodow yɛ mpem ason no. 16Ɛbɛyɛ owigyinae a Ben-Hadad ne nʼapamfo ahemfo aduasa abien gu so rebow nsa wɔ wɔn ntamadan mu no, 17amansin asahene asraafo no tuu teɛe, fii kurow no mu. Wɔrebɛn no, Ben-Hadad akwansrafo ka kyerɛɛ no se, “Asraafo dɔm bi fi Samaria reba.”

18Ben-Hadad hyɛe se, “Sɛ wɔbaa asomdwoe anaa ɔko so a, monkyere wɔn anikann.”

19Nanso saa bere no, na Ahab amansin asahene nkumaa no adi kan a asraafo no bɔ wɔn kyidɔm 20a Israel ɔsraani biara kum ne tamfo Aram ɔsraani a ɔne no dii asi. Ɛno nti, amono mu hɔ ara, Aram asraafo no bɔɔ hu, guanee. Israelfo no taa wɔn, nanso ɔhene Ben-Hadad ne ne nkurɔfo kakra bi de, wɔtenaa apɔnkɔ so guanee. 21Nanso wɔsɛee apɔnkɔ ne nteaseɛnam a ɛkaa hɔ no nyinaa, kunkum Aramfo no.

22Akyiri no, odiyifo no ka kyerɛɛ Ahab se, “Siesie wo ho ma ɔko foforo na Aramhene bɛba asusowbere mu.”

Ben-Hadad Ɔtow A Ɛto So Abien

23Wodii Ben-Hadad so no, ne mpanyimfo no ka kyerɛɛ no se, “Israel anyame no yɛ mmepɔw anyame, na ɛno nti na ɛma wodii nkonim no. Na sɛ wodu tataw so a, yebedi wɔn so nkonim a yɛremmrɛ ho koraa. 24Nea ɛho hia ara ne sɛ, saa bere yi, ɛsɛ sɛ wode akono asahene sisi ahemfo no anan mu. 25Momfa asraafo foforo a wɔn dodow te sɛ wɔn a wohweree wɔn no ara. Ma yɛn apɔnkɔ no dodow, nteaseɛnam ne mmarima dodow saa ara, na yebetumi ne wɔn adi asi wɔ tataw so. Akyinnye biara nni ho sɛ yebedi wɔn so.” Enti ɔhene Ben-Hadad yɛɛ wɔn abisade maa wɔn.

26Na afe so no, ɔfrɛɛ Aram asraafo, tuu teɛ kɔɔ Israelfo so wɔ Afek sɛ wɔne wɔn rekɔko. 27Israel boaboaa nʼasraafo ano, twaa sa, de wɔn ho hyɛɛ ɔko no mu. Na sɛ wɔde Israel asraafo no toto Aram asraafo no dodow a wɔahyɛ hɔ ma no ho a, na Israel asraafo no dodow te sɛ mmirekyikuw nketewa abien bi.

28Onyankopɔn nipa no kɔɔ Israelhene nkyɛn kɔka kyerɛɛ no se, “Sɛnea Awurade se ni: Aramfo no aka se, ‘Awurade yɛ mmepɔw Awurade na ɔnyɛ tataw so Awurade. Enti mɛboa wo ama woadi asraafo buburugyaa yi so. Na ɛbɛma woahu sɛ, mene Awurade no.’ ”

29Asraafo dɔm abien yi bobɔɔ wɔn atenae, ma edii nhwɛanim nnanson. Na nnanson so no, ɔko no hyɛɛ ase. Da no ara, Israelfo no kunkum Aram anammɔnmufo asraafo no mpem ɔha. 30Nkae no guan kɔtɛw Afek fasu akyi, nanso ɔfasu no bu guu wɔn so, kum mpem aduonu ason. Ben-Hadad guan kɔtɛw kokoa mu dan bi mu wɔ kurow no mu.

31Ben-Hadad mpanyimfo ka kyerɛɛ no se, “Owura, yɛate sɛ Israel ahemfo wɔ ahummɔbɔ. Ɛno nti, momma yemfura atweaatam, mfa hama mmɔ yɛn ti ase mfa nkyerɛ ahobrɛase. Na ebia, ɔhene Ahab bɛma woatena ase.”

32Enti wofurafuraa atweaatam, de ahama bobɔɔ wɔn ti, kɔɔ Israelhene nkyɛn kɔsrɛɛ no se, “Wo somfo Ben-Hadad se, ‘Mesrɛ wo, ma me ntena nkwa mu.’ ” Israelhene no bisae se, “Ɔda so te ase ana? Ɔyɛ me nuabarima!”

33Mmarima no yɛɛ ntɛm soo anidaso a enni nnyinaso yi mu, buae se, “Yiw, wo nua Ben-Hadad.”

Israelhene no ka kyerɛɛ wɔn se, “Monkɔfa no mmra.” Bere a wɔde Ben-Hadad bae no, Ahab ma ɔkɔtenaa ne teaseɛnam mu.

34Ben-Hadad ka kyerɛɛ no se, “Mede nkurow a mʼagya gye fii wʼagya nsam no bɛsan ama wo, na woahyehyɛ aguadi wɔ Damasko, sɛnea mʼagya yɛɛ wɔ Samaria no.”

Na Ahab kae se, “Saa nhyehyɛe yi so na megyina na magyaa wo.” Enti, wɔyɛɛ apam, na wogyaa Ben-Hadad.

Odiyifo Bi Bu Ahab Atɛn

35Bere no ara mu, Awurade see adiyifokuw no mu baako se, ɔnka nkyerɛ ɔfoforo se, “Fa wʼakode no bɔ me.” Nanso wanyɛ.

36Na saa odiyifo no ka kyerɛɛ ɔfoforo no se, “Sɛ woantie Awurade nne nti, sɛ wufi ha ara pɛ a, gyata bekum wo.” Ampa ara, ofii hɔ ara pɛ na gyata huu no kum no.

37Na odiyifo no kɔɔ ɔbarima foforo nkyɛn kɔka kyerɛɛ no se, “Fa wʼakode yi bɔ me.” Ɔno de, ɔbɔɔ odiyifo no, piraa no.

38Odiyifo no twɛn ɔhene no wɔ ɔkwankyɛn a ɔde ntamabamma akyekyere nʼani, de pɛɛ sɛ ɔsakra ne ho. 39Ɔhene no retwa mu no, odiyifo no frɛɛ no se, “Owura, na mewɔ akono na ɔbarima bi de odeduani brɛɛ me. Ɔkae se, ‘Wɛn saa ɔbarima yi, na sɛ biribi nti oguan a, wobekum wo anaasɛ wɔbɛbɔ wo ka dwetɛ kilogram aduasa awotwe.’ 40Na bere a mʼani abere redi dwuma bi no, odeduani no guanee. Na ɔhene no kae se, ‘Ɛyɛ wʼankasa wo mfomso. Wo ara woabu wo ho atɛn.’ ”

41Ɛhɔ ara na odiyifo no san ntamabamma no fii nʼani, na Israelhene no huu no sɛ ɔyɛ adiyifo no mu baako. 42Na odiyifo no ka kyerɛɛ no se, “Sɛnea Awurade se ni: Esiane sɛ woagyaa ɔbarima a mekae se, ɛsɛ sɛ wokum no no nti, ɛsɛ sɛ wokum wo mprempren si nʼanan mu. Na anka ɛsɛ sɛ ne nkurɔfo na mukunkum wɔn, na mmom, wo nkurɔfo na wobekunkum wɔn.” 43Israelhene no de abufuw kɔɔ nʼahemfi wɔ Samaria.