1 Wafalme 19 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 19:1-21

Eliya Akimbilia Horebu

119:1 1Fal 16:31; Kut 22:20Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 219:2 Rut 1:17; Za 13:4Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.”

319:3 Mwa 31:21; Yos 19:2Eliya aliogopa, na akakimbia kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko, 419:4 Hes 11:15; Yon 4:8lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, Bwana, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.” 519:5 Mwa 28:11Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.

Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.” 6Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.

7Yule malaika wa Bwana akaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.” 819:8 Kut 3:1; Mt 4:2Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu. 9Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.

Bwana Amtokea Eliya

Nalo neno la Bwana likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Eliya?”

1019:10 1Fal 18:30; Rum 11:3Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize.” 1119:11 Kut 34:2; Nah 1:6Bwana akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Bwana, kwa kuwa Bwana yu karibu kupita hapo.”

Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini Bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko. 1219:12 Kut 3:2; 1Sam 14:6; Ay 4:16Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini Bwana hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona. 1319:13 Kut 3:6Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango.

Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?”

14Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize.”

1519:15 2Fal 8:7-15Bwana akamwambia, “Rudi kwa njia uliyoijia, uende kwenye Jangwa la Dameski. Wakati utakapofika huko, mtie Hazaeli mafuta awe mfalme wa Aramu19:15 Yaani Shamu (ambayo leo ni Syria). 16Pia mtie mafuta Yehu mwana wa Nimshi awe mfalme wa Israeli, na umtie Elisha mwana wa Shafati kutoka Abel-Mehola mafuta awe nabii badala yako. 1719:17 2Fal 8:12, 29; Yer 48:44Yehu atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Hazaeli, naye Elisha atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Yehu. 1819:18 Rum 11:4; Hos 13:2Hata sasa nimeweka akiba watu elfu saba katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, na wote ambao midomo yao haijambusu.”

Wito Wa Elisha

19Hivyo Eliya akaondoka kutoka huko na kumkuta Elisha mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliongoza ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akamrushia vazi lake. 2019:20 Lk 9:61Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.”

Eliya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?”

21Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀上 19:1-21

以利亞逃亡

1亞哈以利亞做的一切事以及他怎樣殺掉所有巴力先知的經過,都告訴了耶洗別2耶洗別就派人去告訴以利亞,說:「明天這個時候,我若不使你像那些人一樣喪命,願神明重重地懲罰我。」

3以利亞很害怕,連忙逃命,來到猶大別示巴。他讓僕人留在那裡, 4自己在曠野走了一天的路程,來到一棵羅騰樹下,坐下來禱告求死,說:「耶和華啊,我受夠了,求你取走我的性命吧,我不比我的祖先強。」 5他躺在樹下睡著了。有一位天使拍醒他,說:「起來吃東西吧。」 6他睜開眼睛,見頭邊有用炭火烤好的餅和一瓶水。他吃喝完畢,又躺下來。 7耶和華的天使第二次來拍醒他,說:「起來吃東西吧,你還要走很遠的路。」 8以利亞起來吃喝,就有了力氣,走了四十晝夜,來到上帝的山——何烈山。

9他進了一個山洞,在裡面過夜。耶和華就問他:「以利亞,你在這裡做什麽?」 10以利亞回答說:「我一向熱心事奉萬軍之上帝耶和華。但以色列人背棄你的約,拆毀你的祭壇,殘殺你的先知。現在只剩下我一個人,他們還要殺我。」 11耶和華說:「你出來站在山上,站在我面前。」耶和華從那裡經過時,疾風大作,劈山碎石,但耶和華不在風中。疾風過後又有地震,但耶和華不在其中。 12地震之後又有火,但耶和華也不在火中。之後,傳來微小的聲音。 13以利亞聽見後,就用外袍蒙著臉出去站在洞口。那聲音問他:「以利亞,你在這裡做什麽?」 14以利亞回答說:「我一向熱心事奉萬軍之上帝耶和華。但以色列人背棄你的約,拆毀你的祭壇,殘殺你的先知。現在只剩下我一個人,他們還要殺我。」 15耶和華吩咐他說:「你原路返回,前往大馬士革附近的曠野,到了之後要膏立哈薛亞蘭王。 16然後,再膏立寧示的孫子耶戶以色列王,還要膏立亞伯·米何拉沙法的兒子以利沙做先知來接替你。 17將來從哈薛刀下逃生的,必被耶戶殺死;從耶戶刀下逃生的,必被以利沙殺死。 18此外,我在以色列留下七千人,他們未曾跪拜巴力,也未曾親吻巴力。」

呼召以利沙

19於是,以利亞離開那裡,找到沙法的兒子以利沙,他正在耕田。他前面有十二對牛,他正趕著第十二對。以利亞走過以利沙身邊時,將自己的外袍搭在他身上。 20以利沙就撇下牛,追上以利亞說:「請你讓我先回去與父母親吻道別,再跟你走吧。」以利亞說:「你回去吧,別忘了我剛才對你做的事。」 21以利沙就回去了。他宰了兩頭耕牛,用耕具作柴煮肉分給眾人,然後去跟隨以利亞,服侍他。