1 Wafalme 14 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 14:1-31

Unabii Wa Ahiya Dhidi Ya Yeroboamu

1Wakati ule Abiya mwana wa Yeroboamu akaugua, 214:2 1Fal 11:29naye Yeroboamu akamwambia mke wake, “Nenda ukajibadilishe, ili watu wasijue kwamba wewe ni mke wa Yeroboamu. Kisha uende Shilo. Nabii Ahiya yuko huko, yule aliyeniambia kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa. 314:3 1Sam 9:7Chukua mikate kumi, maandazi kadhaa na gudulia la asali na umwendee. Atakuambia kitakachotokea kwa kijana.” 4Basi mke wa Yeroboamu akafanya kama alivyosema mumewe, akaenda kwenye nyumba ya Ahiya huko Shilo.

Wakati huu Ahiya alikuwa kipofu naye alishindwa kuona kwa sababu ya umri wake. 5Lakini Bwana alikuwa amemwambia Ahiya, “Mke wa Yeroboamu anakuja kukuuliza kuhusu mwanawe, kwa kuwa ni mgonjwa, nawe utamjibu hivi na hivi. Atakapowasili, atajifanya kuwa ni mtu mwingine.”

6Hivyo Ahiya aliposikia kishindo cha hatua zake mlangoni, akasema, “Karibu ndani, mke wa Yeroboamu. Kwa nini kujibadilisha? Nimetumwa kwako nikiwa na habari mbaya. 714:7 1Sam 15:29Nenda, ukamwambie Yeroboamu kwamba hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Nilikuinua miongoni mwa watu na kukufanya kiongozi juu ya watu wangu Israeli. 814:8 1Sam 15:27; 1Fal 3:3Nikararua ufalme kutoka kwa nyumba ya Daudi na kukupa wewe, lakini hukuwa kama mtumishi wangu Daudi, ambaye aliyashika maagizo yangu na kunifuata kwa moyo wake wote, akifanya tu lile lililokuwa sawa machoni pangu. 914:9 2Nya 11:15; Za 50:17Umefanya maovu mengi kuliko wote waliokutangulia. Umejitengenezea miungu mingine, sanamu za chuma, umenighadhibisha na kunitupa nyuma yako.

1014:10 Kum 32:36; 1Fal 15:29“ ‘Kwa sababu ya hili, nitaleta maafa juu ya nyumba ya Yeroboamu. Nitakatilia mbali kutoka kwa Yeroboamu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, mtumwa au mtu huru. Nitachoma nyumba ya Yeroboamu mpaka iteketee yote kama mtu achomaye kinyesi. 1114:11 1Fal 16:4; Mwa 40:19Mbwa watawala wale walio wa nyumba ya Yeroboamu watakaofia ndani ya mji na ndege wa angani watajilisha kwa wale watakaofia mashambani. Bwana amesema!’

12“Kukuhusu wewe, rudi nyumbani. Wakati utakapotia mguu katika mji wako, kijana atakufa. 1314:13 2Nya 12:12; 19:3Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Kwa sababu ni yeye pekee wa nyumba ya Yeroboamu atakayezikwa, kwa sababu ni yeye peke yake ndani ya nyumba ya Yeroboamu ambaye Bwana, Mungu wa Israeli, ameona kitu chema kwake.

14Bwana atajiinulia mwenyewe mfalme juu ya Israeli ambaye ataikatilia mbali jamaa ya Yeroboamu. Siku ndiyo hii! Nini? Naam, hata sasa hivi. 1514:15 Yer 44:3; Kum 12:3Naye Bwana ataipiga Israeli, hata iwe kama unyasi unaosukwasukwa juu ya maji. Ataingʼoa Israeli kutoka nchi hii nzuri aliyowapa baba zao na kuwatawanya ngʼambo ya Mto Frati, kwa sababu wamemghadhibisha Bwana kwa kutengeneza nguzo za Ashera14:15 Yaani mfano wa mungu wa kike Ashera. 1614:16 1Fal 12:30Naye atawaacha Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu aliyoyatenda na kusababisha Israeli kuyatenda.”

1714:17 1Fal 15:33; Yos 12:24Kisha mke wa Yeroboamu akainuka, akaondoka kwenda Tirsa. Mara alipokanyaga kizingiti cha mlango, kijana akafa. 18Wakamzika na Israeli yote ikamwombolezea, kama Bwana alivyokuwa amesema kupitia mtumishi wake, nabii Ahiya.

19Matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, vita vyake na jinsi alivyotawala, vimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. 20Yeroboamu akawatawala kwa miaka ishirini na miwili, kisha akalala na baba zake. Naye Nadabu mwanawe akawa mfalme baada yake.

Rehoboamu Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 11:5–12:15)

21Rehoboamu mwana wa Solomoni alikuwa mfalme wa Yuda. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji ambao Bwana alikuwa ameuchagua kutoka makabila yote ya Israeli ili apate kuliweka humo Jina lake. Mama yake aliitwa Naama, ambaye alikuwa Mwamoni.

2214:22 2Nya 12:1; Kum 32:21Yuda wakatenda maovu machoni pa Bwana. Kwa dhambi walizotenda wakachochea hasira yake yenye wivu zaidi kuliko baba zao walivyofanya. 2314:23 Kut 23:24; Kum 12:3Pia wakajijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu, mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kilichoinuka na kila mti uliotanda. 2414:24 Mit 21:27; Kum 23:17Walikuwepo hata wanaume mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu katika nchi; watu wakajiingiza katika kutenda machukizo ya mataifa ambayo Bwana aliyafukuza mbele ya Waisraeli.

2514:25 2Nya 12:2Katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu. 2614:26 1Fal 15:15, 18; 2Sam 8:7Akachukua hazina za Hekalu la Bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao zote za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza. 2714:27 2Fal 11:5Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme. 28Kila wakati mfalme alipokwenda katika Hekalu la Bwana, walinzi walizichukua hizo ngao, na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.

29Kwa matukio mengine ya utawala wa Rehoboamu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 3014:30 1Fal 12:21Kulikuwa na vita vinavyoendelea kati ya Rehoboamu na Yeroboamu. 3114:31 1Fal 11:1Naye Rehoboamu akalala na baba zake, na akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mama yake aliitwa Naama, ambaye alikuwa Mwamoni. Naye Abiya14:31 Maandishi mengine ya Kiebrania yanamwita Abiyamu. mwanawe akawa mfalme baada yake.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀上 14:1-31

亞希雅對耶羅波安的預言

1那時,耶羅波安的兒子亞比雅病了, 2耶羅波安就吩咐妻子:「你喬裝改扮使人認不出你是我妻子,然後去示羅找那位預言我做王的先知亞希雅3你要帶十個餅、一些薄餅和一瓶蜂蜜去,他將告訴你孩子的病情會怎樣。」

4耶羅波安的妻子就照他的話做,前往示羅,來到亞希雅家。那時亞希雅因年紀老邁,眼睛已失明。 5耶和華預先告訴亞希雅說:「耶羅波安的妻子會喬裝成別的婦女,前來問你有關她兒子的病情,你要如此如此回答她。」

6她剛進門,亞希雅聽見她的腳步聲就說:「耶羅波安的妻子啊,你進來吧,為什麼喬裝改扮呢?我奉命告訴你一個噩耗。 7你回去告訴耶羅波安,『以色列的上帝耶和華說,我從百姓中擢升你,立你做我以色列子民的王。 8我把國從大衛家奪走賜給你,你卻沒有像我僕人大衛那樣遵守我的誡命,全心聽從我,做我視為正的事, 9反而比前人行惡更甚,為自己設立其他神明,鑄造神像,惹我發怒,把我拋在腦後。 10所以,我要降禍給耶羅波安家,從以色列剷除耶羅波安家所有的男子,不論是奴隸還是自由人。我要像清除糞便一樣,把耶羅波安家焚燒淨盡。 11耶羅波安家人中,死在城中的必被狗吃,死在田野的必被鳥吃。這是耶和華說的。』

12「現在你回家去吧,你一進城,孩子就會死。 13以色列會為他哀悼,把他埋葬。耶羅波安家人中只有他將得到安葬,因為以色列的上帝耶和華在他身上看見了良善。 14耶和華必為自己立一位君王統治以色列,他必剷除耶羅波安家。現在就是時候了。 15耶和華將擊打以色列人,使他們像水中的蘆葦一樣顫抖不已。耶和華將把以色列人從祂賜給他們祖先的佳美之地連根拔起,拋散到幼發拉底河的彼岸,這都是因為他們製造亞舍拉神像,惹耶和華發怒。 16因為耶羅波安犯罪作孽,使以色列人陷入罪中,耶和華必拋棄以色列。」

17耶羅波安的妻子動身回到得撒,剛邁過家門檻,孩子就死了。 18以色列人埋葬了他,為他哀悼,正應驗了耶和華藉祂僕人亞希雅先知說的話。

19耶羅波安其他的事,不論文治武功,都記在以色列的列王史上。 20他做王二十二年,然後與祖先同眠。他兒子拿答繼位。

羅波安做猶大王

21所羅門的兒子羅波安猶大王。他四十一歲登基,在耶路撒冷,就是耶和華從以色列眾支派中選擇來立祂名的城執政十七年。羅波安的母親是亞捫拿瑪22猶大人做耶和華視為惡的事,他們的罪行比他們祖先所做的更惹耶和華發怒。 23他們在各高崗上、樹蔭下為自己建造邱壇,豎立神柱和亞舍拉神像, 24國中甚至男廟妓充斥。猶大人仿效耶和華在以色列人面前趕走的外族人,行各種可憎之事。

25羅波安王執政第五年,埃及示撒上來攻陷耶路撒冷26搶走了耶和華的殿和王宮裡所有的寶物,包括所羅門製造的金盾牌。 27羅波安王就造了銅盾牌代替那些金盾牌,交給看守宮門的護衛長看管。 28每次王進耶和華的殿,護衛軍就帶上盾牌,用完後放回護衛房。

29羅波安其他的事及其一切所作所為都記在猶大的列王史上。 30羅波安常常與耶羅波安爭戰。 31羅波安與祖先同眠後,葬在大衛城的祖墳裡。他母親是亞捫拿瑪。他兒子亞比央繼位。