1 Wafalme 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 1:1-53

Adoniya Ajitangaza Mfalme

11:1 Yer 29:10-14; Zek 1:12-16; 2Nya 36:22-23; Ezr 5:13; 7:27; Yer 25:12; Law 26:42Mfalme Daudi alipokuwa mzee umri ukiwa umesogea, hakuweza kupata joto hata walipomfunika kwa nguo. 21:2 Amu 4:10; Isa 44:28; Ezr 5:13; Za 72:11Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Turuhusu tumtafute kijana mwanamwali bikira amhudumie mfalme na kumtunza. Anaweza kulala pembeni mwake ili bwana wetu mfalme apate joto.”

31:3 Kum 3:24; 2Sam 22:32; Za 86:10; Dan 6:26; 1Kor 8:6; Isa 37:16; Mk 12:32Kisha wakatafuta katika Israeli yote ili kumpata msichana mzuri wa sura na wakampata Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme. 41:4 Isa 10:20-22; Hes 15:3; Za 116:17; Ezr 3:7; 4:3Msichana huyo alikuwa mzuri sana wa sura, akamtunza mfalme na kumhudumia, lakini mfalme hakufanya naye tendo la ndoa.

51:5 2Nya 34:9; Neh 12:34; Hag 1:4; Mit 16:1Basi Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi, akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini wa kumtangulia wakikimbia. 6(Baba yake hakuwa ameingilia na kumuuliza, “Kwa nini unafanya hivyo?” Alikuwa pia kijana mzuri sana wa sura, na alizaliwa baada ya Absalomu.)

71:7 2Fal 24:13; Ezr 5:14; 6:5; 2Nya 36:7; Yer 52:17-19Adoniya akashauriana pamoja na Yoabu mwana wa Seruya na kuhani Abiathari, nao wakamsaidia. 81:8 Ezr 5:14; Hag 1:1; 1Nya 3:18Lakini kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada, Nathani nabii, Shimei, Rei na walinzi maalum wa Daudi hawakujiunga na Adoniya.

9Ndipo Adoniya akatoa dhabihu ya kondoo, ngʼombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote, wana wa mfalme na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa mfalme, 10lakini hakumwalika nabii Nathani, Benaya, walinzi maalum wa mfalme, wala ndugu yake Solomoni.

11Ndipo Nathani akamuuliza Bathsheba, mama yake Solomoni, “Je, hujasikia kwamba Adoniya, mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili? 12Sasa basi, acha nikushauri jinsi utakavyookoa uhai wako mwenyewe na uhai wa mwanao Solomoni. 13Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi juu ya kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adoniya amekuwa mfalme?’ 14Utakapokuwa ukizungumza na mfalme, nitaingia na kuthibitisha hayo uliyoyasema.”

15Hivyo Bathsheba akaenda kumwona mfalme chumbani mwake mahali ambapo Abishagi, Mshunami, alikuwa akimhudumia, naye mfalme alikuwa mzee sana. 16Bathsheba akasujudu na kupiga magoti mbele ya mfalme.

Mfalme akauliza, “Ni nini hiki unachotaka?”

17Akamwambia, “Bwana wangu, wewe mwenyewe uliniapia mimi mtumishi wako kwa Bwana Mungu wako kwamba: ‘Solomoni Mwanao atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme.’ 18Lakini sasa Adoniya amekuwa mfalme, nawe, bwana wangu mfalme huna habari kuhusu jambo hilo. 19Ametoa dhabihu idadi kubwa ya ngʼombe, ndama walionona na kondoo, naye amewaalika wana wa mfalme wote, kuhani Abiathari, na Yoabu jemadari wa jeshi, lakini hakumwalika Solomoni mtumishi wako. 20Bwana wangu mfalme, macho ya Israeli yote yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa ni nani atakayeketi katika kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake. 21Kama sivyo, mara tu bwana wangu mfalme atakapopumzishwa pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Solomoni tutatendewa kama wahalifu.”

22Alipokuwa angali anazungumza na mfalme, nabii Nathani akafika. 23Wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa.” Kisha akaenda mbele ya mfalme na kumsujudia hadi uso wake ukagusa ardhi.

24Nathani akasema, “Je, bwana wangu mfalme, umetangaza kuwa Adoniya atakuwa mfalme baada yako na kwamba ataketi kwenye kiti chako cha ufalme? 25Leo ameshuka na kutoa dhabihu idadi kubwa ya ngʼombe, ndama walionona na kondoo. Amewaalika wana wote wa mfalme, jemadari wa jeshi na kuhani Abiathari. Sasa hivi, wanakula na kunywa pamoja naye wakisema, ‘Aishi maisha marefu, Mfalme Adoniya!’ 26Lakini mimi mtumishi wako, kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada na mtumishi wako Solomoni hakutualika. 27Je, hili ni jambo ambalo bwana wangu mfalme amelifanya pasipo kuwajulisha watumishi wake ili wapate kujua ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake?”

Daudi Amfanya Solomoni Kuwa Mfalme

28Ndipo Mfalme Daudi akasema, “Mwite Bathsheba, aingie ndani.” Hivyo akaingia mbele ya mfalme na kusimama mbele yake.

29Ndipo mfalme akaapa: “Hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ameniokoa kutoka kila taabu, 30hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli: Mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.”

31Kisha Bathsheba akasujudu akipiga magoti mbele ya mfalme uso wake ukigusa ardhi akasema, “Bwana wangu Mfalme Daudi na aishi milele!”

32Mfalme Daudi akasema, “Mwite kuhani Sadoki ndani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Walipofika mbele ya mfalme, 33akawaambia: “Wachukueni watumishi wa bwana wenu pamoja nanyi na mkamkalishe mwanangu Solomoni juu ya nyumbu wangu mwenyewe mkamteremshe hadi Gihoni. 34Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, ‘Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!’ 35Kisha mtapanda pamoja naye, atakuja na kuketi kwenye kiti changu cha ufalme na kutawala badala yangu. Nimemweka awe mtawala juu ya Israeli na Yuda.”

36Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, “Amen! Bwana, Mungu wa bwana wangu mfalme, na aseme vivyo hivyo. 37Kama vile Bwana alivyokuwa na bwana wangu mfalme, vivyo hivyo na awe na Solomoni kukifanya kiti chake cha utawala kuwa kikuu kuliko kile cha bwana wangu Mfalme Daudi!”

38Hivyo kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi wakampandisha Solomoni juu ya nyumbu wa Mfalme Daudi, nao wakamsindikiza hadi Gihoni. 39Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!” 40Na watu wote wakakwea wakimfuata, wakipiga filimbi na kushangilia sana, hata ardhi ikatikisika kwa ile sauti.

41Adoniya pamoja na wageni wote waliokuwa pamoja naye wakasikia sauti hiyo walipokuwa wakimalizia karamu yao. Waliposikia sauti ya tarumbeta, Yoabu akauliza, “Nini maana ya makelele yote haya katika mji?”

42Hata alipokuwa anasema, Yonathani mwana wa kuhani Abiathari akafika. Adoniya akasema, “Ingia ndani. Mtu mstahiki kama wewe ni lazima alete habari njema.”

43Yonathani akajibu, “La hasha! Mfalme Daudi bwana wetu amemfanya Solomoni kuwa mfalme. 44Mfalme amemtuma pamoja naye kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi, nao wamempandisha juu ya nyumbu wa mfalme, 45nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme huko Gihoni. Kuanzia hapo wameendelea kushangilia na sauti zimeenea pote mjini. Hizo ndizo kelele unazosikia. 46Zaidi ya hayo, Solomoni ameketi juu ya kiti chake cha ufalme. 47Pia, maafisa wa mfalme wamekuja ili kumtakia heri bwana wetu Mfalme Daudi wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la Solomoni kuwa mashuhuri kuliko lako na kiti chake cha ufalme kiwe na ukuu kuliko chako!’ Naye mfalme akasujudu akiabudu kitandani mwake 48na kusema, ‘Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye ameruhusu macho yangu kuona mrithi juu ya kiti changu cha ufalme leo hii.’ ”

49Katika hili, wageni wote wa Adoniya wakainuka kwa mshtuko wa hofu na kutawanyika. 50Lakini Adoniya kwa kumwogopa Solomoni, akaenda na kushika pembe za madhabahu. 51Kisha Solomoni akaambiwa, “Adoniya anamwogopa Mfalme Solomoni na ameshikilia pembe za madhabahu. Anasema, ‘Mfalme Solomoni na aniapie leo kwamba hatamuua mtumishi wake kwa upanga.’ ”

52Solomoni akajibu, “Kama akijionyesha kuwa mtu mstahiki, hakuna unywele wake utakaoanguka juu ya ardhi, lakini kama uovu ukionekana ndani yake, atakufa.” 53Ndipo Mfalme Solomoni akawatuma watu, nao wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye Adoniya akaja akamwinamia Mfalme Solomoni, naye Solomoni akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪上 1:1-53

王位之争

1大卫王年纪老迈,虽然盖了几层被子,仍然觉得冷。 2他的臣仆建议:“不如选一位少女进宫伺候、照顾我主我王,让她睡在王怀中给王取暖。”

3于是,他们在以色列全国寻找美貌女子,找到了一位名叫雅比莎书念少女,把她带到王那里。 4这女子长得花容月貌,她照顾、伺候王,但王没有与她同房。

5那时,哈姬的儿子亚多尼雅妄自尊大,说:“我必做王。”他为自己制备了车辆和骑兵,派五十人在前面开路。 6他父亲从不干涉、责问他:“你这是做什么?”他是押沙龙的弟弟,长得英俊非凡。

7亚多尼雅洗鲁雅的儿子约押及祭司亚比亚他商议,二人都答应支持他。 8不过,撒督祭司、耶何耶大的儿子比拿雅拿单先知、示每利以大卫的勇士却没有跟随他。

9一天,亚多尼雅隐·罗结附近的琐希列磐石那里宰了牛羊和肥牛犊献祭,并邀请了众王子和犹大的群臣。 10可是他没有邀请拿单先知、比拿雅大卫的勇士和他的兄弟所罗门

11拿单所罗门的母亲拔示芭说:“你没有听说吗?哈姬的儿子亚多尼雅做王了,我们的主大卫还不知道。 12事到如今,我有一个主意,可以保住你和你儿子所罗门的性命。 13你去见大卫王,对他说,‘我主我王啊,你不是起誓说让臣妾的儿子所罗门继承王位吗?怎么现在亚多尼雅做了王呢?’ 14你跟王说话的时候,我会进去证实你的话。”

15拔示芭就进内室去见年迈的王,书念的少女雅比莎正在伺候他。 16拔示芭向王屈身下拜。王问道:“你有什么事吗?” 17拔示芭回答说:“我主啊,你曾经凭你的上帝耶和华起誓说让臣妾的儿子所罗门继承你的王位,坐你的宝座。 18但现在亚多尼雅已经称王了,我主我王还不知道。 19他宰了许多牛羊和肥牛犊献祭,邀请众王子、亚比亚他祭司和约押元帅,却没有邀请你的仆人所罗门20我主我王啊!以色列举国拭目以待,等着王来指定谁继承王位。 21不然,到我主我王与祖先同眠之后,我和我儿所罗门必被定为罪人。”

22她与王正说话间,拿单先知进宫来了。 23有人奏告王,说:“拿单先知来了。”拿单来到王面前,俯伏在地, 24说:“我主我王啊,你已经宣布让亚多尼雅继承你的王位,坐你的宝座吗? 25他今天宰了许多牛羊和肥犊献祭,宴请众王子、将领和亚比亚他祭司,他们正在他那里一边吃喝一边说,‘亚多尼雅王万岁!’ 26但他没有邀请臣仆我、撒督祭司、耶何耶大的儿子比拿雅和你的仆人所罗门27这是我主我王的旨意吗?王还没有对臣仆们说过谁继承王位。”

28于是,大卫王召见拔示芭拔示芭立刻晋见,侍立在王面前。 29王起誓说:“我凭救我脱离一切苦难的永活的耶和华起誓, 30我今天必实现我凭以色列的上帝耶和华向你起的誓。你的儿子所罗门必继承王位,坐在我的宝座上。”

31拔示芭就向王俯伏下拜说:“我主我王万岁!”

32大卫王又召见撒督祭司、拿单先知和耶何耶大的儿子比拿雅。他们都来到王面前。 33王嘱咐道:“你们要率领我的随从,让我儿所罗门骑上我的骡子,护送他下到基训34撒督祭司和拿单先知要在那里膏立他为以色列王。你们要吹响号角,高喊,‘所罗门王万岁!’ 35然后,你们要随他回来,他要登基,继承我的王位。我已立他做以色列犹大的君王了。”

36耶何耶大的儿子比拿雅说:“遵命,愿我主我王的上帝耶和华成全这事。 37耶和华怎样与我主我王同在,愿祂也照样与所罗门同在,使他的国比我主大卫王的国更强大。” 38于是,撒督祭司、拿单先知、耶何耶大的儿子比拿雅,以及基利提人和比利提人请所罗门骑上大卫王的骡子,护送他前往基训39撒督祭司从圣幕里拿来盛膏油的角,膏立所罗门为王。他们吹响号角,民众高声欢呼:“所罗门王万岁!” 40众人浩浩荡荡地随着所罗门回京,一路上吹笛欢呼,声音震动大地。 41亚多尼雅和他的众宾客刚刚饮宴完毕,听见了这声音。约押听见号角声,便问:“城里为什么如此喧闹?” 42就在这时候,亚比亚他祭司的儿子约拿单来了,亚多尼雅说:“进来!你是个忠勇的人,一定带来了好消息。”

43约拿单说:“我们的主大卫王已经立所罗门为王了。 44王派撒督祭司、拿单先知、耶何耶大的儿子比拿雅,以及基利提人和比利提人护送所罗门骑上王的骡子。 45撒督祭司和拿单先知在基训膏立他为王,他们一路上欢呼着回来了,全城轰动。你们听到的就是他们的声音。 46所罗门已经登基掌权, 47王的臣仆也来向我们的主大卫王道喜说,‘愿王的上帝使所罗门比王更声名显赫,使他的国比王的国更强大。’王在床上俯伏敬拜, 48说,‘以色列的上帝耶和华当受称颂,因为祂让我亲眼看见我的继承人今天登基。’”

49亚多尼雅的众宾客听后,吓得四散而去。 50亚多尼雅惧怕所罗门,就去抓住祭坛的角。 51有人告诉所罗门:“亚多尼雅惧怕王,现在正抓住祭坛的角,要王今天起誓不要杀他。”

52所罗门说:“如果他是个忠义的人,必毫发无损;如果他作恶,必死无疑。” 53于是,所罗门王便派人去把亚多尼雅从祭坛上带下来。亚多尼雅前来向所罗门王俯伏下拜,所罗门对他说:“你回家去吧。”