1 Timotheo 5 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Timotheo 5:1-25

Maagizo Kuhusu Wajane, Wazee Na Watumwa

15:1 Tit 2:2; Law 19:32; Tit 2:6Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako; 2nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote.

35:3 1Tim 5:5, 16Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. 45:4 Efe 6:1-2; Rum 12:2Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu. 55:5 1Kor 7:34; 1Pet 3:5; Lk 2:37Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie. 65:6 Lk 15:24Lakini mjane aishiye kwa anasa amekufa, ingawa anaishi. 75:7 1Tim 4:11Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. 85:8 Tit 1:16; Yud 4Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.

95:9 Lk 2:36; 1Tim 3:2Mjane yeyote asiwekwe kwenye orodha ya wajane isipokuwa awe ametimiza umri wa miaka sitini, na ambaye alikuwa mke wa mume mmoja, 105:10 Mdo 9:36; 1Pet 2:12; Lk 7:44awe ameshuhudiwa kwa matendo yake mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliye mkarimu, aliyewanawisha watakatifu miguu, aliyewasaidia wenye shida na aliyejitolea kwa ajili ya matendo mema ya kila namna.

11Lakini kwa habari za wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena. 12Nao kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kukiuka ahadi yao ya kwanza. 135:13 2The 3:11Zaidi ya hayo, wajane kama hao huwa na tabia ya uvivu wakizurura nyumba kwa nyumba, wala hawawi wavivu tu, bali pia huwa wasengenyaji, wajiingizao katika mambo yasiyowahusu na kusema mambo yasiyowapasa kusema. 145:14 1Kor 7:9; 1Tim 6:1Hivyo nawashauri wajane vijana waolewe, wazae watoto na wasimamie nyumba zao, wasije wakampa adui nafasi ya kutushutumu. 155:15 Mt 4:10Kwa maana kwa kweli wajane wengine wamepotoka ili kumfuata Shetani.

165:16 1Tim 5:3, 5Lakini kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane katika jamaa yake, inampasa awasaidie wala si kuwaacha wakililemea kanisa, ili kanisa liweze kuwasaidia wale ambao ni wajane kweli kweli.

Wazee Wa Kanisa

175:17 Mdo 11:30; Flp 2:29; 1The 5:12Wazee wa kanisa wanaoongoza shughuli za kanisa vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha. 185:18 Kum 25:4; 1Kor 9:7-9; Law 19:13; Mt 10:10Kwa maana Maandiko husema, “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka,” tena, “Mfanyakazi anastahili mshahara wake.” 195:19 Mdo 11:30; Mt 18:16Usiendekeze mashtaka dhidi ya mzee isipokuwa yawe yameletwa na mashahidi wawili au watatu. 205:20 2Tim 4:2; Tit 1:13; Kum 13:11Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa.

215:21 1Tim 6:13; 2Tim 4:1Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.

225:22 Mdo 6:6; Efe 5:11Usiwe na haraka kumwekea mtu mikono wala usishiriki dhambi za watu wengine. Jilinde nafsi yako uwe safi.

235:23 1Tim 3:8Acha kunywa maji peke yake, tumia divai kidogo kwa sababu ya tumbo lako na maumivu yako ya mara kwa mara.

245:24 Gal 5:19Dhambi za watu wengine ni dhahiri nazo zinawatangulia kwenda hukumuni; na dhambi za watu wengine zinawafuata nyuma yao. 25Vivyo hivyo, matendo mema yako dhahiri, na hata yale ambayo si mema hayawezi kufichika.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

提摩太前書 5:1-25

信徒的責任

1不要斥責年長的,要像對待父親一樣勸他們;對待青年男子要情同手足; 2對待年長的婦女要情同母親;對待青年女子要心思純正,視她們如姊妹。

3要敬重和幫助那些真正有需要的寡婦。 4如果寡婦有兒孫,就要叫她們的兒孫在家中學習盡孝道,奉養她們,以報答養育之恩,這是上帝所悅納的。 5真正有需要、無依無靠的寡婦仰賴上帝的幫助,晝夜不住地禱告祈求。 6但貪圖享受的寡婦雖然活著,卻已經死了。 7你當教導眾人這些事,好叫他們無可指責。 8誰不照顧自己的親屬,尤其是不照顧自己的家人,就是違背真道,比不信的人還壞。

9列入名冊的寡婦必須年滿六十歲,在婚姻上從一而終, 10並且在善事上有好名聲,如教養兒女、接待外人、服侍聖徒、救助困苦、竭力做各種善事。

11不要把年輕的寡婦列入名冊,因為當她們情慾衝動,無法持守對基督的委身時,就想再嫁, 12以致違背了起初的誓言而受審判。 13況且,她們不僅懶散成性,四處串門,還說長道短,好管閒事,搬弄是非。 14所以,我建議年輕的寡婦再嫁,生兒育女,料理家務,不要給仇敵毀謗的機會, 15因為有些人已經偏離正道,去追隨撒旦了。 16女信徒的家裡若有寡婦,就應該自己照顧她們,免得加重教會的負擔,這樣教會才能照顧那些真正無依無靠的寡婦。

17那些善於管理教會的長老,尤其是那些辛勤傳道和教導人的,理當得到加倍的尊敬和報酬。 18因為聖經上說:「牛在踩穀時,不可籠住牠的嘴。」又說:「做工的得報酬是應該的。」 19若有人向你控告長老,必須有兩三個證人,否則不要受理。 20那些一直犯罪的人,你要當眾責備他們,以警戒眾人。

21我在上帝和主耶穌基督以及蒙揀選的眾天使面前吩咐你:要遵行這些話,不要有成見,不要偏心; 22為人行按手禮,不要操之過急。不要沾染別人的罪,要潔身自好。

23你的胃不好,經常生病,不要只喝水,要稍微喝一點酒。

24有些人的罪很明顯,自招審判,有些人的罪日後才暴露出來。 25同樣,有些善行很明顯,不明顯的也不會被長久埋沒。