1 Timotheo 1 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Timotheo 1:1-20

11:1 Tit 1:3; Kol 1:27Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu.

21:2 Mdo 16:1; 1Kor 4:17; 1The 2:11Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani:

Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Maonyo Dhidi Ya Walimu Wa Uongo

31:3 Mdo 18:19; Gal 1:6, 7Kama nilivyokusihi wakati nilipokwenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili kwamba upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo 41:4 1Tim 4:7; 2Tim 4:4; 1Tim 6:4wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani. 51:5 2Tim 2:22; 1:5Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. 61:6 1Tim 6:4, 20Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa, 71:7 Efe 4:11; Ay 38:2wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.

81:8 Rum 7:12Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa. 91:9 Gal 3:19; 5:23Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, 101:10 1Tim 6:3; 2Tim 1:13kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli, 111:11 1The 2:4ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi nimewekewa amana.

Neema Ya Mungu Kwa Paulo

121:12 Flp 4:13Namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona mwaminifu, akaniteua kwa kazi yake. 131:13 Mdo 8:3; 26:9Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu. 141:14 Rum 5:20; 2Tim 1:13Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.

151:15 1Tim 4:9; 2Tim 2:11Msemo huu ni wa kweli na unaostahili kukubalika, usemao kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote. 161:16 1Tim 1:13; Rum 2:4; Yn 3:15; Mt 25:46Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele. 171:17 Ufu 15:3; Kol 1:15; Rum 11:36Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.

181:18 1Tim 4:14; 2Tim 4:7Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri, 191:19 1Tim 6:21; Mdo 23:1; 1Tim 6:21; 2Tim 2:18ukiishikilia imani na dhamiri njema, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao. 201:20 2Tim 2:17; 4:14; 1Kor 5:5Miongoni mwao wako Himenayo na Aleksanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.

King James Version

1 Timothy 1:1-20

1Paul, an apostle of Jesus Christ by the commandment of God our Saviour, and Lord Jesus Christ, which is our hope; 2Unto Timothy, my own son in the faith: Grace, mercy, and peace, from God our Father and Jesus Christ our Lord.

3As I besought thee to abide still at Ephesus, when I went into Macedonia, that thou mightest charge some that they teach no other doctrine, 4Neither give heed to fables and endless genealogies, which minister questions, rather than godly edifying which is in faith: so do. 5Now the end of the commandment is charity out of a pure heart, and of a good conscience, and of faith unfeigned: 6From which some having swerved have turned aside unto vain jangling; 7Desiring to be teachers of the law; understanding neither what they say, nor whereof they affirm. 8But we know that the law is good, if a man use it lawfully; 9Knowing this, that the law is not made for a righteous man, but for the lawless and disobedient, for the ungodly and for sinners, for unholy and profane, for murderers of fathers and murderers of mothers, for manslayers, 10For whoremongers, for them that defile themselves with mankind, for menstealers, for liars, for perjured persons, and if there be any other thing that is contrary to sound doctrine; 11According to the glorious gospel of the blessed God, which was committed to my trust. 12And I thank Christ Jesus our Lord, who hath enabled me, for that he counted me faithful, putting me into the ministry; 13Who was before a blasphemer, and a persecutor, and injurious: but I obtained mercy, because I did it ignorantly in unbelief. 14And the grace of our Lord was exceeding abundant with faith and love which is in Christ Jesus. 15This is a faithful saying, and worthy of all acceptation, that Christ Jesus came into the world to save sinners; of whom I am chief. 16Howbeit for this cause I obtained mercy, that in me first Jesus Christ might shew forth all longsuffering, for a pattern to them which should hereafter believe on him to life everlasting. 17Now unto the King eternal, immortal, invisible, the only wise God, be honour and glory for ever and ever. Amen. 18This charge I commit unto thee, son Timothy, according to the prophecies which went before on thee, that thou by them mightest war a good warfare; 19Holding faith, and a good conscience; which some having put away concerning faith have made shipwreck: 20Of whom is Hymenaeus and Alexander; whom I have delivered unto Satan, that they may learn not to blaspheme.