1 Samweli 7 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 7:1-17

17:1 Yos 6:7; 2Sam 6:3; 1Nya 13:7; 1Sam 6:21; Za 132:6Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la Bwana. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la Bwana.

Samweli Awatiisha Wafilisti Huko Mispa

27:2 1Nya 13:5; Za 132:6; 1Nya 13:3Sanduku la Bwana lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafuta Bwana. 37:3 Kut 30:10; 2Fal 18:5; 23:25; Yer 24:7; Mwa 31:19; Amu 2:12-13; 1Sam 12:10; 31:10; Yoe 2:12; Yos 24:14; Kum 6; 13; Mt 4:10; Lk 4:8; Amu 2:18Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa Bwana na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.” 4Hivyo Waisraeli wakaweka mbali Mabaali yao na Maashtorethi, nao wakamtumikia Bwana peke yake.

57:5 1Sam 1:20; Za 99:6; Yer 15:1; Yos 11:3; Amu 21:5; 1Sam 10:17; Mwa 20:7; Kum 9:19Kisha Samweli akasema, “Wakusanyeni Israeli wote huko Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa Bwana.” 67:6 Yos 11:3; Mao 2:19; Amu 2:16; 16:31; Neh 9:1, 2; 2Sam 14:14; Dan 9:3; Yoe 2:12; Law 26:40; Amu 10:10; 1Fal 8:47; Ay 33:27, 28; Za 106:6Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za Bwana. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana.” Naye Samweli alikuwa kiongozi7:6 Kiongozi hapa maana yake mwamuzi. wa Israeli huko Mispa.

77:7 1Sam 17:11Wafilisti waliposikia kwamba Israeli wamekusanyika huko Mispa, watawala wa Wafilisti wakapanda ili kuwashambulia. Waisraeli waliposikia habari hiyo, waliogopa kwa sababu ya Wafilisti. 87:8 Kut 32:30; Hes 21:7; 1Sam 12:19, 23; 1Fal 18:24; Isa 37:4; Yer 15:1; 27:18Wakamwambia Samweli, “Usiache kumlilia Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, ili apate kutuokoa na mikono ya Wafilisti.” 97:9 Za 99:6; Kut 32:11; Kum 19:9; Yer 15:1Kisha Samweli akamchukua mwana-kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. Akamlilia Bwana kwa niaba ya Israeli, naye Bwana akamjibu.

107:10 Kut 9:23; 14:24; 1Sam 2:10; Mwa 35:5; 2Sam 22:14-15; Yos 10:10Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile Bwana alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka hivi kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli. 11Watu wa Israeli wakatoka mbio huko Mispa na kuwafuatia Wafilisti, wakiwachinja njiani hadi mahali chini ya Beth-Kari.

127:12 Mwa 28:22; Kum 27:2; Yos 4:9; 1Sam 4; 1Ndipo Samweli akachukua jiwe na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita Ebenezeri,7:12 Ebenezeri maana yake jiwe la usaidizi. akisema, “Hata sasa Bwana ametusaidia.” 137:13 Amu 13:5; 1Sam 13:5Basi Wafilisti wakashindwa na hawakuvamia nchi ya Israeli tena.

Katika maisha yote ya Samweli, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi ya Wafilisti. 147:14 Yos 13:3; Amu 1:34Miji kuanzia Ekroni hadi Gathi, ile ambayo Wafilisti walikuwa wameiteka kutoka Israeli, ilirudishwa kwake, naye Israeli akazikomboa nchi jirani mikononi mwa Wafilisti. Kukawepo amani kati ya Israeli na Waamori.

157:15 1Sam 12:11; Amu 2:16-18Samweli akaendelea kama mwamuzi juu ya Israeli siku zote za maisha yake. 167:16 Mwa 12:8; Yos 10:43; 1Sam 10:8; Amo 5:5; Mdo 13; 20Mwaka hadi mwaka aliendelea kuzunguka kutoka Betheli mpaka Gilgali na Mispa, akiamua Israeli katika sehemu hizo zote. 177:17 Yos 18:25; 1Sam 8:4; 15:34; 19:18; 25:1; 28:3; 9:12; 14:35; 20:6; 2Sam 24:25Lakini kila mara alirudi Rama, kulikokuwa nyumbani kwake, huko pia aliwaamua Israeli. Naye huko alimjengea Bwana madhabahu.

Nueva Versión Internacional

1 Samuel 7:1-17

1Los de Quiriat Yearín fueron a Bet Semes y se llevaron el arca del Señor a la casa de Abinadab, que estaba en una loma. Luego consagraron a su hijo Eleazar para que estuviera a cargo de ella.

Samuel derrota a los filisteos en Mizpa

2El arca permaneció en Quiriat Yearín durante mucho tiempo, unos veinte años, y todo el pueblo de Israel buscaba con ansiedad al Señor. 3Por eso Samuel dijo al pueblo: «Si ustedes desean volverse al Señor de todo corazón, desháganse de los dioses extranjeros y de las imágenes de Astarté. Dedíquense totalmente a servir solo al Señor, y él los librará del poder de los filisteos». 4Así que los israelitas echaron fuera a los ídolos de Baal y a las imágenes de Astarté y sirvieron solo al Señor.

5Luego Samuel ordenó: «Reúnan a todo Israel en Mizpa para que yo ruegue al Señor por ustedes». 6Cuando los israelitas se reunieron en Mizpa, sacaron agua y la derramaron ante el Señor. También ayunaron durante el día, y públicamente confesaron: «Hemos pecado contra el Señor». Fue en Mizpa donde Samuel comenzó a liderar a los israelitas.

7Cuando los filisteos se enteraron de que los israelitas se habían reunido en Mizpa, los jefes filisteos marcharon contra Israel. Al darse cuenta de esto, los israelitas tuvieron miedo de los filisteos 8y dijeron a Samuel: «No dejes de clamar al Señor por nosotros, para que nos salve del poder de los filisteos». 9Samuel tomó entonces un cordero pequeño y lo ofreció en holocausto al Señor. Luego clamó al Señor en favor de Israel, y el Señor respondió.

10Mientras Samuel ofrecía el sacrificio, los filisteos avanzaron para atacar a Israel. Pero aquel día el Señor lanzó grandes truenos contra los filisteos. Esto creó confusión entre ellos y cayeron derrotados ante los israelitas. 11Entonces los israelitas persiguieron a los filisteos desde Mizpa hasta más allá de Bet Car, matándolos por el camino.

12Después Samuel tomó una piedra, la colocó entre Mizpa y Sen, y la llamó Ebenezer,7:12 En hebreo, Ebenezer significa piedra de ayuda. «El Señor no ha dejado de ayudarnos».

13Durante toda la vida de Samuel, el Señor manifestó su poder sobre los filisteos. Estos fueron subyugados por los israelitas y no volvieron a invadir su territorio. 14Fue así como los israelitas recuperaron las ciudades que los filisteos habían capturado anteriormente, desde Ecrón hasta Gat, y libraron todo ese territorio del dominio de los filisteos. También hubo paz entre Israel y los amorreos.

15Samuel siguió gobernando a Israel toda su vida. 16Todos los años recorría las ciudades de Betel, Guilgal y Mizpa, y atendía los asuntos del país en esas regiones. 17Luego regresaba a Ramá, donde residía, y desde allí lideraba a Israel. También allí erigió un altar al Señor.