1 Samweli 27 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 27:1-12

Daudi Miongoni Mwa Wafilisti

1Daudi akasema moyoni mwake, “Katika mojawapo ya siku hizi nitaangamizwa kwa mkono wa Sauli. Jambo lililo bora ni kutorokea kwenye nchi ya Wafilisti. Hivyo Sauli atakata tamaa ya kunisaka popote katika Israeli, nami nitakuwa nimeponyoka mkononi mwake.”

227:2 1Sam 30:9; 2:3; 21:10; 1Fal 2:39; 1Sam 25:13Hivyo Daudi akaondoka na hao watu mia sita waliokuwa pamoja naye na kwenda kwa Akishi mwana wa Maoki mfalme wa Gathi. 327:3 1Sam 25:43; 30:3Daudi na watu wake wakakaa huko Gathi pamoja na Akishi. Kila mtu alikuwa pamoja na jamaa yake, naye Daudi pamoja na wakeze wawili: yaani Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, mjane wa Nabali. 4Sauli alipokuwa ameambiwa kwamba Daudi alikuwa amekimbilia Gathi, hakuendelea kumsaka tena.

5Ndipo Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, unipe sehemu katika mojawapo ya miji katika nchi nikae huko. Kwa nini mtumwa wako akae pamoja nawe katika mji huu wa kifalme?”

627:6 Yos 15:31; 19:5; 1Sam 30:1; 1Nya 12:30; Neh 11:28Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi mji wa Siklagi, nao Siklagi umekuwa mali ya wafalme wa Yuda tangu wakati huo. 727:7 1Sam 29:3Daudi akaishi katika nchi ya Wafilisti muda wa mwaka mmoja na miezi minne.

827:8 Yos 12:5; Kut 17:14, 16; 1Sam 14:48; 30:1; 2Sam 1:8; 8:12; Mwa 16:5; Kut 15:22; Yos 13:2; Amu 1:29; Mwa 25:18Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.) 927:9 1Sam 15:3Kila mara Daudi aliposhambulia eneo, hakubakiza hai mwanaume wala mwanamke, lakini alichukua kondoo na ngʼombe, punda na ngamia, na nguo. Kisha akarudi kwa Akishi.

1027:10 1Sam 30:29; Amu 1:16; 1Nya 2:9, 25; Za 14:3; Mit 29:25Akishi alipomuuliza, “Je leo umeshambulia wapi?” Daudi humjibu, “Dhidi ya Negebu ya Yuda,” au wakati mwingine husema, “Dhidi ya Negebu ya Yerameeli,” au “Dhidi ya Negebu ya Wakeni.” 11Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana Daudi aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo ilikuwa desturi yake wakati wote aliishi katika nchi ya Wafilisti. 1227:12 Mwa 34:30; 1Sam 29:6Akishi akamsadiki Daudi na kuwaza moyoni mwake, akasema, “Daudi amekuwa kitu cha kuchukiza kabisa kwa watu wake, Waisraeli, hivi kwamba atakuwa mtumishi wangu milele.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

撒母耳記上 27:1-12

大衛投奔非利士人

1大衛心裡想:「終有一天,我會死在掃羅手裡,我最好逃到非利士人那裡。這樣,掃羅就不會在以色列到處追捕我了,我便可以逃離他的手。」 2於是,大衛率領他的六百個隨從去投靠瑪俄的兒子迦特亞吉3他部下的家眷和他的兩位妻子——耶斯列亞希暖拿八的遺孀迦密亞比該也跟他一同住在迦特亞吉那裡。 4掃羅聽到這個消息,就不再追捕他了。 5大衛亞吉說:「如果你開恩,就讓我到郊野的一個城邑去住吧,何必讓僕人與王一同住在都城呢?」 6亞吉當天把洗革拉賜給他,因此那地方至今仍屬猶大王。 7大衛非利士人的地方共住了一年零四個月。 8他率領部下襲擊基述人、基色人和亞瑪力人,這些人自古以來就住在遠至書珥埃及一帶的地方。 9大衛攻打那一帶,殺死所有的人,搶走牛、羊、驢、駱駝和衣物,回去見亞吉10亞吉問:「你們今天攻打了哪裡?」大衛會說:「攻打了猶大南部」,或說:「攻打了耶拉篾南部」,或說:「攻打了基尼南部。」 11大衛把那地方的人都殺掉,一個也不帶到迦特,因為他害怕他們會洩露真相。大衛非利士人那裡居住的時候,常常這樣做。 12亞吉相信了大衛的話,心裡想:「以色列人恨透了大衛,他必永遠留在迦特做我的僕人。」