1 Petro 5 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Petro 5:1-14

Kulichunga Kundi La Mungu

15:1 Mdo 11:30; Lk 24:48; 1Pet 4:13; Ufu 1:9Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa: 25:2 Yn 21:6; 1Tim 3:3lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika. 35:3 Eze 34:4; Mt 20:25-28; Flp 3:17; 1Tim 4:12Msijifanye mabwana juu ya wale walio chini ya uangalizi wenu, bali kuweni vielelezo kwa hilo kundi. 45:4 1Kor 9:25; Ebr 13:20; 1Kor 9:25; 2Tim 4:8; Yak 1:12; 1Pet 1:4Naye Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu isiyoharibika.

55:5 Efe 5:21; Mit 3:34; Yak 4:6Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa,

“Mungu huwapinga wenye kiburi,

lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

65:6 Yak 4:10Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. 75:7 Mit 27:5; Mt 6:25; Ebr 13:5Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

85:8 Ay 1:7; Lk 21:34, 36; 1The 5:6; 1Pet 4:7; Ufu 12:12Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza. 95:9 Yak 4:7; Kol 2:5; Mdo 14:22Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.

105:10 2Kor 4:17; 2The 2:17Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha. 115:11 Rum 11:36; 1Pet 4:11; Ufu 1:6Uweza una yeye milele na milele. Amen.

Salamu Za Mwisho

125:12 2Kor 1:19; Ebr 13:22Kwa msaada wa Silvano,5:12 Yaani Sila. ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.

135:13 Mdo 12:12Kanisa lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu. 145:14 Rum 16:16; Efe 6:23Salimianeni kwa busu la upendo.

Amani iwe nanyi nyote mlio katika Kristo.

King James Version

1 Peter 5:1-14

1The elders which are among you I exhort, who am also an elder, and a witness of the sufferings of Christ, and also a partaker of the glory that shall be revealed: 2Feed the flock of God which is among you, taking the oversight thereof, not by constraint, but willingly; not for filthy lucre, but of a ready mind; 3Neither as being lords over God’s heritage, but being ensamples to the flock. 4And when the chief Shepherd shall appear, ye shall receive a crown of glory that fadeth not away. 5Likewise, ye younger, submit yourselves unto the elder. Yea, all of you be subject one to another, and be clothed with humility: for God resisteth the proud, and giveth grace to the humble.

6Humble yourselves therefore under the mighty hand of God, that he may exalt you in due time: 7Casting all your care upon him; for he careth for you. 8Be sober, be vigilant; because your adversary the devil, as a roaring lion, walketh about, seeking whom he may devour: 9Whom resist stedfast in the faith, knowing that the same afflictions are accomplished in your brethren that are in the world. 10But the God of all grace, who hath called us unto his eternal glory by Christ Jesus, after that ye have suffered a while, make you perfect, stablish, strengthen, settle you. 11To him be glory and dominion for ever and ever. Amen.

12By Silvanus, a faithful brother unto you, as I suppose, I have written briefly, exhorting, and testifying that this is the true grace of God wherein ye stand. 13The church that is at Babylon, elected together with you, saluteth you; and so doth Marcus my son. 14Greet ye one another with a kiss of charity. Peace be with you all that are in Christ Jesus. Amen.