1 Nyakati 21 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 21:1-30

Daudi Ahesabu Wapiganaji

(2 Samweli 24:1-25)

121:1 2Nya 18:21; 1Fal 22:20-22; Za 109:6; 2Nya 14:8; Ufu 12:9; 2Nya 25:5; Mt 4:2; Yn 13:2; Mdo 5:3Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. 221:2 1Nya 27:23-24Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.”

3Yoabu akajibu, “Bwana na aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?”

421:4 Mit 29:25; Mdo 5:29; 4:19; Mhu 8:4Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu. 5Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.

621:6 Hes 1:47-49; 1Nya 27:24Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme. 7Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli.

821:8 2Sam 24:10; Ay 42:6; Hos 14:2; Za 25:11; 51:1-3; Mit 28:13-14; 2Kor 7:10Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

921:9 1Sam 22:5; 9:9Bwana akamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi, 10“Nenda ukamwambie Daudi, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

11Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Chagua: 1221:12 Kum 32:24; Eze 30:25; Mwa 19:13; 2Sam 24:13miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Bwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa Bwana akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”

1321:13 Neh 9:17; Za 6:4; 130:4-7; Mao 3:22; Za 100:5; 145:9; Yoe 2:13Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa Bwana kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”

1421:14 1Nya 27:24Basi Bwana akatuma tauni katika Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa. 1521:15 Mwa 32:1; 2Sam 24:16; Mwa 6:6; Kut 32:14; Mwa 19:13; Yer 26:18; Mt 23:37-38; Amu 2:18Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, Bwana akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna21:15 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi.

1621:16 Hes 14:5; Yos 7:6; 2Nya 3:1Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa Bwana akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.

1721:17 2Sam 7:8; Za 74:1; Yon 1:12Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Ee Bwana, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.”

18Kisha malaika wa Bwana akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea Bwana madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi. 19Kwa hiyo Daudi akakwea, akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina la Bwana.

2021:20 Amu 6:11Arauna alipokuwa akipura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano. 21Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akiuinamisha uso wake ardhini.

2221:22 Hes 16:48; 25:8Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya Bwana tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”

23Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”

24Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili ya Bwana au kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.”

2521:25 2Sam 24:24Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 60021:25 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 7. kwa ajili ya ule uwanja. 2621:26 Kut 19:18; 2Nya 7:1Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita Bwana naye Bwana akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

27Kisha Bwana akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake. 28Wakati huo, Daudi alipoona kwamba Bwana amemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko. 2921:29 Yos 9:3; 1Fal 3:4; 1Nya 16:39Maskani ya Bwana ambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. 3021:30 1Nya 13:12; Ay 13:21; 2Sam 6:9; Ay 21:6; Za 119:120Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumuuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika wa Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志上 21:1-30

大卫统计人口

1撒旦为了攻击以色列,就挑动大卫统计以色列人的数目。 2大卫约押和其他军中的首领说:“你们要走遍以色列,从别示巴一直到,统计以色列的人口,然后回来禀告我,我好知道他们的数目。” 3约押说:“愿耶和华使祂子民的人数比现在增加百倍。但我主我王啊,他们不都是你的仆人吗?我主为什么要这样做,使以色列人陷于罪中呢?” 4大卫不听约押的规劝。约押只好出去,走遍以色列,然后回到耶路撒冷5将人数呈报大卫:全以色列有一百一十万刀兵,犹大有四十七万。 6约押没有把利未人和便雅悯人算在其中,因为他厌恶王的这个命令。 7上帝也不喜悦这事,便降灾给以色列人。 8大卫对上帝说:“我做这事犯了大罪。求你赦免仆人的罪,我做了极其愚昧的事。” 9耶和华对大卫的先见迦得说: 10“你去告诉大卫,我有三样灾祸,他可以选择让我降哪一样给他。”

11迦得就来见大卫,把耶和华的话告诉他,说:“你可以任选一样, 12或三年的饥荒,或被敌人追杀三个月,或国中遭三天的瘟疫,让耶和华的天使在以色列全境施行毁灭。请你考虑好后告诉我,我好回复那差我来的。” 13大卫说:“我实在为难!不过我宁愿落在耶和华的手中,也不愿落在人的手中,因为耶和华有无限的怜悯。”

14于是,耶和华在以色列降下瘟疫,有七万人死亡。 15上帝差遣天使去毁灭耶路撒冷。天使正要毁灭的时候,耶和华见了就心生怜悯,对施行毁灭的天使说:“够了,住手吧!”当时,耶和华的天使正站在耶布斯阿珥楠的麦场上。 16大卫举目看见耶和华的天使站在天地之间,手握着已出鞘的刀,指向耶路撒冷大卫和众长老都身披麻衣,脸伏于地。 17大卫对上帝说:“吩咐统计人民数目的不是我吗?是我犯了罪,做了恶事,这些百姓有什么过错呢?我的上帝耶和华啊,愿你的手惩罚我和我的家族,不要把瘟疫降在你的子民身上。”

18耶和华的天使吩咐迦得去告诉大卫耶布斯阿珥楠的麦场上为耶和华建一座祭坛。 19大卫照耶和华借迦得所说的话去了麦场。 20那时,阿珥楠正在打麦子,他转身看见了天使,跟他在一起的四个儿子都躲了起来。 21阿珥楠看见大卫来了,就从麦场出来,俯伏叩拜大卫22大卫对他说:“请你将这块麦场卖给我,我要在这里为耶和华筑一座祭坛,好止住民间的瘟疫。你全价卖给我吧。” 23阿珥楠说:“我主我王只管用我的麦场!我愿献出牛作燔祭,打麦的器具作柴,麦子作素祭,我愿献出这一切。”

24大卫王说:“不可,我一定要付你全价,我不能拿你的东西献给耶和华,不能把白白得来的献作燔祭。” 25于是,大卫就用七公斤金子买了阿珥楠的麦场。 26大卫在那里为耶和华建了一座坛,献上燔祭和平安祭,并求告耶和华。耶和华垂听了他的祷告,从天上降火在祭坛上, 27又命令天使收刀入鞘。

28大卫见耶和华在耶布斯阿珥楠的麦场上应允了他的祷告,就在那里献祭。 29那时候,摩西在旷野为耶和华所造的圣幕和燔祭坛都在基遍的高地。 30大卫因为惧怕耶和华天使的刀,不敢去那里求问上帝。