Isaiah 3 – KJV & NEN

King James Version

Isaiah 3:1-26

1For, behold, the Lord, the LORD of hosts, doth take away from Jerusalem and from Judah the stay and the staff, the whole stay of bread, and the whole stay of water, 2The mighty man, and the man of war, the judge, and the prophet, and the prudent, and the ancient, 3The captain of fifty, and the honourable man, and the counsellor, and the cunning artificer, and the eloquent orator.3.3 the honourable…: Heb. a man eminent in countenance3.3 eloquent…: or, skilful of speech 4And I will give children to be their princes, and babes shall rule over them. 5And the people shall be oppressed, every one by another, and every one by his neighbour: the child shall behave himself proudly against the ancient, and the base against the honourable. 6When a man shall take hold of his brother of the house of his father, saying, Thou hast clothing, be thou our ruler, and let this ruin be under thy hand: 7In that day shall he swear, saying, I will not be an healer; for in my house is neither bread nor clothing: make me not a ruler of the people.3.7 swear: Heb. lift up the hand3.7 healer: Heb. binder up 8For Jerusalem is ruined, and Judah is fallen: because their tongue and their doings are against the LORD, to provoke the eyes of his glory.

9¶ The shew of their countenance doth witness against them; and they declare their sin as Sodom, they hide it not. Woe unto their soul! for they have rewarded evil unto themselves. 10Say ye to the righteous, that it shall be well with him: for they shall eat the fruit of their doings. 11Woe unto the wicked! it shall be ill with him: for the reward of his hands shall be given him.3.11 given…: Heb. done to him

12As for my people, children are their oppressors, and women rule over them. O my people, they which lead thee cause thee to err, and destroy the way of thy paths.3.12 lead…: or, call thee blessed3.12 destroy: Heb. swallow up 13The LORD standeth up to plead, and standeth to judge the people. 14The LORD will enter into judgment with the ancients of his people, and the princes thereof: for ye have eaten up the vineyard; the spoil of the poor is in your houses.3.14 eaten: or, burnt 15What mean ye that ye beat my people to pieces, and grind the faces of the poor? saith the Lord GOD of hosts.

16¶ Moreover the LORD saith, Because the daughters of Zion are haughty, and walk with stretched forth necks and wanton eyes, walking and mincing as they go, and making a tinkling with their feet:3.16 wanton…: Heb. deceiving with their eyes3.16 mincing: or, tripping nicely 17Therefore the Lord will smite with a scab the crown of the head of the daughters of Zion, and the LORD will discover their secret parts.3.17 discover: Heb. make naked 18In that day the Lord will take away the bravery of their tinkling ornaments about their feet, and their cauls, and their round tires like the moon,3.18 cauls: or, networks 19The chains, and the bracelets, and the mufflers,3.19 chains: or, sweet balls3.19 mufflers: or, spangled ornaments 20The bonnets, and the ornaments of the legs, and the headbands, and the tablets, and the earrings,3.20 tablets: Heb. houses of the soul 21The rings, and nose jewels, 22The changeable suits of apparel, and the mantles, and the wimples, and the crisping pins, 23The glasses, and the fine linen, and the hoods, and the vails. 24And it shall come to pass, that instead of sweet smell there shall be stink; and instead of a girdle a rent; and instead of well set hair baldness; and instead of a stomacher a girding of sackcloth; and burning instead of beauty. 25Thy men shall fall by the sword, and thy mighty in the war.3.25 mighty: Heb. might 26And her gates shall lament and mourn; and she being desolate shall sit upon the ground.3.26 desolate: or, emptied: Heb. cleansed

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 3:1-26

Hukumu Juu Ya Yerusalemu Na Yuda.

13:1 Law 26:26; Eze 4:16; Amo 4:6; Yer 37:21; Za 18:18; Isa 5:13; 65:13Tazama sasa, Bwana,

Bwana Mwenye Nguvu Zote,

yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda

upatikanaji wa mahitaji na misaada,

upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,

23:2 Eze 17:13; Isa 9:14-15; 2Fal 24:14; Kum 18:10shujaa na mtu wa vita,

mwamuzi na nabii,

mwaguzi na mzee,

33:3 Ay 22:8; 2Fal 24:14; Mhu 10:11; Yer 8:17; 2Fal 1:9jemadari wa kikosi cha watu hamsini

na mtu mwenye cheo, mshauri,

fundi stadi na mlozi mjanja.

43:4 Mhu 10:16Nitawafanya wavulana wawe maafisa wao,

watoto ndio watakaowatawala.

53:5 Za 28:3; Yer 9:8; Isa 9:19; Mik 7:2-6Watu wataoneana wao kwa wao:

mtu dhidi ya mtu, na jirani dhidi ya jirani yake.

Kijana atainuka dhidi ya mzee,

mtu mnyonge dhidi ya mtu mwenye heshima.

6Mtu atamkamata mmoja wa ndugu zake

katika nyumba ya baba yake na kusema,

“Unalo joho, sasa uwe kiongozi wetu,

tawala lundo hili la magofu!”

73:7 Yer 30:12; Hos 5:13; Isa 2:11; 24:2; Eze 34:4; Yoe 1:16Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema,

“Sina uponyaji.

Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu,

msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

83:8 Isa 30:9; 9:15-17; 28:15; 1:7; Ay 1:11; Za 73:9-11; 2Nya 33:6; Isa 65:7Yerusalemu inapepesuka,

Yuda inaanguka;

maneno yao na matendo yao ni kinyume na Bwana,

wakiudharau uwepo wake uliotukuka.

93:9 Mwa 13:13; 2Nya 34:24; Rum 6:23; Hes 32:23; Isa 59:12; Yer 14:7; Mit 8:36; Hos 5:5Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao,

hujivunia dhambi yao kama Sodoma,

wala hawaifichi.

Ole wao!

Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.

103:10 Za 37:17; Yer 22:15; Mwa 15:1; Za 128:2; Kum 12:28; 5:33Waambie wanyofu itakuwa heri kwao,

kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao.

113:11 Kum 28:15-68; Ay 9:13; Isa 57:20; Kum 28:15-68; 2Nya 6:23; Yer 21:14; Mao 5:16; Eze 24:14Ole kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao!

Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.

123:12 Yer 25:16; Mik 3:5; Isa 9:16; 19:14; 28:7; Yer 23:13; 25:16Vijana wanawatesa watu wangu,

wanawake wanawatawala.

Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha,

wanawapoteza njia.

133:13 Ay 10:2; Za 82:1; Isa 2:4Bwana anachukua nafasi yake mahakamani,

anasimama kuhukumu watu.

143:14 1Sam 12:7; Yak 2:6; Ay 22:4; 24:9; Isa 25:4; 11:4Bwana anaingia katika hukumu

dhidi ya wazee na viongozi wa watu wake:

“Ninyi ndio mlioharibu shamba langu la mizabibu,

mali zilizonyangʼanywa maskini zimo nyumbani mwenu.

153:15 Za 94:5; Ay 24:14; Isa 10:6; 26:6; 29:19; 32:6; 5:7Mnamaanisha nini kuwaponda watu wangu

na kuzisaga nyuso za maskini?”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

163:16 Wim 3:11; Ay 15:25Bwana asema,

“Wanawake wa Sayuni wana kiburi,

wanatembea na shingo ndefu,

wakikonyeza kwa macho yao,

wanatembea kwa hatua za madaha,

wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.

173:17 Eze 27:31; Amo 8:10Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni;

Bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”

183:18 Mwa 41:42; Amu 8:21; Isa 2:11Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo, 193:19 Mwa 24:47; Eze 16:11-12vipuli, vikuku, shela, 203:20 Kut 39:28; Eze 44:18; 24:17, 23vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi, 213:21 Mwa 24:22; Kut 29:6pete zenye muhuri, pete za puani, 223:22 Rut 3:15majoho mazuri, mitandio, mavazi, kifuko cha kutilia fedha, 233:23 Eze 26:10; 23:26; Kut 29:6; Wim 3:11; Isa 61:3; 62:3vioo, mavazi ya kitani, taji na shali.

243:24 Es 2:12; Mit 31:24; Law 13:40; Yon 3:5-8; Isa 4:4; 20:2; Ay 1:20; 16:15; Mwa 37:34; Yer 4:8; Mao 2:10Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo;

badala ya mishipi, ni kamba;

badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara;

badala ya mavazi mazuri, ni nguo za magunia;

badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.

253:25 Isa 1:20; Yer 15:8Wanaume wako watauawa kwa upanga,

nao mashujaa wako watauawa vitani.

263:26 Yer 14:2; 4:28; Mao 2:10; Ay 2:13; Isa 14:12, 31; 33:9; 24:4, 7; Za 137:1Malango ya Sayuni yataomboleza na kulia,

ataketi mavumbini akiwa fukara.