Colossians 4 – KJV & NEN

King James Version

Colossians 4:1-18

1Masters, give unto your servants that which is just and equal; knowing that ye also have a Master in heaven.

2Continue in prayer, and watch in the same with thanksgiving; 3Withal praying also for us, that God would open unto us a door of utterance, to speak the mystery of Christ, for which I am also in bonds: 4That I may make it manifest, as I ought to speak. 5Walk in wisdom toward them that are without, redeeming the time. 6Let your speech be alway with grace, seasoned with salt, that ye may know how ye ought to answer every man.

7All my state shall Tychicus declare unto you, who is a beloved brother, and a faithful minister and fellowservant in the Lord: 8Whom I have sent unto you for the same purpose, that he might know your estate, and comfort your hearts; 9With Onesimus, a faithful and beloved brother, who is one of you. They shall make known unto you all things which are done here.

10Aristarchus my fellowprisoner saluteth you, and Marcus, sister’s son to Barnabas, (touching whom ye received commandments: if he come unto you, receive him;) 11And Jesus, which is called Justus, who are of the circumcision. These only are my fellowworkers unto the kingdom of God, which have been a comfort unto me. 12Epaphras, who is one of you, a servant of Christ, saluteth you, always labouring fervently for you in prayers, that ye may stand perfect and complete in all the will of God. 13For I bear him record, that he hath a great zeal for you, and them that are in Laodicea, and them in Hierapolis. 14Luke, the beloved physician, and Demas, greet you. 15Salute the brethren which are in Laodicea, and Nymphas, and the church which is in his house. 16And when this epistle is read among you, cause that it be read also in the church of the Laodiceans; and that ye likewise read the epistle from Laodicea. 17And say to Archippus, Take heed to the ministry which thou hast received in the Lord, that thou fulfil it. 18The salutation by the hand of me Paul. Remember my bonds. Grace be with you. Amen.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wakolosai 4:1-18

14:1 Law 25:43, 53Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.

Maagizo Zaidi

24:2 Lk 18:1; 1The 5:17; Efe 6:18; Flp 4:6Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. 34:3 Mdo 14:27; Efe 6:19-20; Rum 15:30; 1Kor 16:9Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa. 44:4 Efe 6:20Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena. 54:5 Efe 5:15; Mk 4:11; Efe 5:16Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 64:6 Efe 4:29; Mk 9:50; 1Pet 3:15Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.

Salamu Za Mwisho

74:7 Mdo 20:4; Efe 6:21-22Tikiko atawaambia habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mtendakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana. 84:8 Efe 6:22; 6:21Nimemtuma kwenu kwa madhumuni haya ili mpate kufahamu hali yetu, na pia awatie moyo. 94:9 Flp 1:10; Flm 10; Kol 4:12Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mmoja wenu. Watawaambia mambo yote yanayotendeka hapa kwetu.

104:10 Mdo 19:21; 4:36Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.) 114:11 Flp 2:25Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu. 124:12 Kol 1:7; Flp 1:23; Rum 15:30; 1Kor 2:6Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti. 134:13 Kol 2:1Ninashuhudia kumhusu kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na wale wa Hierapoli. 144:14 2Tim 4:11; Flp 1:24; 2Tim 4:10Rafiki yetu mpenzi Luka yule tabibu, pamoja na Dema, wanawasalimu. 154:15 Rum 16:5Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia, na pia Nimfa, pamoja na kanisa linalokutana katika nyumba yake.

164:16 2The 3:14Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kanisa la Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia.

174:17 Flp 1:2; 2Tim 4:5Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma uliyopokea katika Bwana.”

184:18 1Kor 16:21; Ebr 13:3Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen.