הבשורה על-פי מתי 19 – HHH & NEN

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי מתי 19:1-30

1כשסיים ישוע את דבריו, עזב את הגליל וחזר ליהודה דרך עבר הירדן. 2קהל גדול הלך בעקבותיו, והוא ריפא את החולים שביניהם. 3פרושים אחדים שבאו לנסותו שאלו: ”האם מותר לאיש להתגרש מאשתו על כל דבר?“ 4ישוע הגיב: ”האם אינכם קוראים את כתבי־הקודש? הלא כתוב שאלוהים ברא איש ואישה מבראשית, 5ושעל האיש לעזוב את אביו ואמו, ולהתאחד עם אשתו.19‏.5 יט 5 כלשונו: ”על כן יעזוב איש את אביו ואת אמו ודבק באשתו והיו לבשר אחד.“ (בראשית ב 24) 6לפיכך הם כבר לא שניים אלא אחד! וכך אסור לאיש להפריד את מה שאלוהים איחד.“

7”אם כך,“ המשיכו הפרושים, ”מדוע משה אמר שאיש יכול לכתוב לה ספר כריתות (מכתב גירושין), וזה כל מה שנדרש ממנו?“

8ישוע הסביר: ”משה הרשה לכם להתגרש מנשותיכם רק משום שלקח בחשבון את האופי העקשני שלכם. אולם לא זאת הייתה כוונתו המקורית של אלוהים. 9אני אומר לכם: כל איש המגרש את אשתו, מלבד במקרה שבגדה בו, ונושא אחרת לאישה – הוא נואף!“

10”אם כך הדבר,“ אמרו תלמידיו של ישוע, ”הרי מוטב לא להינשא כלל!“ 11”לא כל אחד יכול לקבל עמדה זאת“, אמר ישוע. ”רק אלה שה׳ עוזר להם בכך יכולים לקבל אותה. 12אחדים נולדים סריסים ואינם יכולים להינשא, אחרים מסורסים על־ידי אדם, ויש המסרבים להינשא למען מלכות השמים. מי שיכול – שיקבל זאת על עצמו.“

13ילדים קטנים הובאו אל ישוע כדי שיניח את ידיו עליהם ויתפלל. אולם התלמידים גערו באמהות שהביאו את הילדים: ”אל תטרידו אותו!“

14ישוע שמע ואמר: ”תנו לילדים לבוא אלי ואל תמנעו מהם, כי לכאלה שייכת מלכות השמים!“ 15לפני שהלך משם הוא הניח את ידיו על ראשי הילדים וברך אותם.

16יום אחד בא איש אל ישוע ושאל: ”רבי, אילו דברים טובים עלי לעשות כדי לזכות בחיי נצח?“

17”מדוע אתה שואל אותי בנוגע לטוב? רק אלוהים טוב באמת!“ השיב לו ישוע. ”אולם בתשובה לשאלתך: אם תשמור את המצוות תזכה בחיי נצח.“

18”איזה?“ שאל האיש.

”לא תרצח, לא תנאף, לא תגנוב, לא תענה עד שקר, 19כבד את אביך ואת אמך, ואהבת לרעך כמוך!“ השיב ישוע.

20”תמיד שמרתי את כל המצוות האלה. מה עוד עלי לעשות?“

21”אם ברצונך להיות שלם,“ ענה ישוע, ”מכור את כל רכושך וחלק את הכסף לעניים, כדי שאוצרך יהיה בשמים, ולאחר מכן לך אחרי.“

22לשמע דברים אלה התעצב האיש והלך לדרכו, כי היה עשיר מאוד.

23ישוע פנה לתלמידיו ואמר: ”לאדם עשיר קשה מאוד להיכנס למלכות השמים. 24דעו לכם שקל יותר לגמל לעבור דרך חור המחט, מאשר לאיש עשיר להיכנס למלכות האלוהים.“

25הערה זאת הביכה את התלמידים. ”מי, אם כן, יוכל להיוושע?“ שאלו.

26ישוע הביט בהם ואמר: ”למעשה, אף אחד, אולם עם אלוהים הכול אפשרי!“

27”אנחנו עזבנו הכול כדי ללכת אחריך“, אמר פטרוס. ”מה נקבל בתמורה?“

28”כשבן־האדם יישב במלכות על כסא כבודו המפואר,“ השיב ישוע, ”אתם, תלמידי, תשבו על שנים־עשר כסאות ותשפטו את שנים־עשר שבטי ישראל. 29כל מי שוויתר למעני על ביתו, אחיו, אחיותיו, אביו, אמו, אשתו, ילדיו או רכושו – יקבל בתמורה פי מאה ויזכה בחיי נצח. 30אולם רבים מאלה שהם ראשונים עתה יהיו אז אחרונים, ואחדים מהאחרונים עתה יהיו אז ראשונים.“

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 19:1-30

Yesu Afundisha Kuhusu Talaka

(Marko 10:1-12)

119:1 Mt 7:28Yesu alipomaliza kusema maneno haya, aliondoka Galilaya, akaenda sehemu za Uyahudi, ngʼambo ya Mto Yordani. 219:2 Mt 4:23Umati mkubwa wa watu ukamfuata, naye akawaponya huko.

319:3 Mt 5:31Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?”

419:4 Mwa 1:27; 5:2Akawajibu, “Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, 519:5 Mwa 2:24; Efe 5:31naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? 619:6 1Kor 7:10, 11Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

719:7 Kum 24:1-4; Mt 5:31-32Wakamuuliza, “Kwa nini basi Mose aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?”

8Yesu akawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. 919:9 Lk 16:18Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.”

1019:10 Mit 21:19Wanafunzi wake wakamwambia, “Kama hali ndiyo hii kati ya mume na mke, ni afadhali mtu asioe!”

1119:11 Mit 13:11; 1Kor 7:7-9, 17Yesu akawaambia, “Si watu wote wanaoweza kupokea neno hili, isipokuwa wale tu waliojaliwa na Mungu. 1219:12 1Kor 7:12, 14; 9:5, 15Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

(Marko 10:13-16; Luka 18:15-17)

1319:13 Mk 5:23Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta.

1419:14 Mt 23:34; 18:3; 1Pet 2:2Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa.” 15Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko.

Kijana Tajiri

(Marko 10:17-31; Luka 18:18-30)

1619:16 Mt 25:46; Lk 10:25Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

1719:17 Law 18:5Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”

1819:18 Yak 2:11Yule mtu akamuuliza, “Amri zipi?”

Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 1919:19 Kut 20:12-16; Kum 5:16-20; Law 19:18; Mt 5:43waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.”

20Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?”

2119:21 Mt 5:48; Lk 12:33; Mdo 4:34-35; Mt 6:20Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

2219:22 Za 62:10Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Hatari Za Utajiri

2319:23 Mt 13:22; 1Tim 6:9-10Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Amin, nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. 24Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

25Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

2619:26 Zek 8:6; Rum 4:21; Lk 18:28; Kum 33:9; Mt 4:20; Lk 5:11Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”

2719:27 Mt 4:19Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata! Tutapata nini basi?”

2819:28 Mt 20:21; 25:31; Lk 22:28-30; Ufu 3:21; Lk 22:28, 29, 30; 1Kor 6:2, 3; Ufu 2:26Yesu akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. 2919:29 Mt 6:33; 25:46; Mk 10:29, 30; Lk 18:29, 30Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele. 3019:30 Mk 10:33; Lk 10:30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.