馬可福音 11 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬可福音 11:1-33

騎驢進耶路撒冷

1耶穌和門徒將近耶路撒冷,快到橄欖山附近的伯法其伯大尼兩個村莊時,祂派了兩個門徒, 2對他們說:「你們去前面的村莊,一進村就會看見一頭從來沒有人騎過的驢駒拴在那裡,你們把牠解開牽來。 3若有人問你們為什麼這樣做,就說,『主要用牠,很快會把牠送回來。』」 4他們進了村子,果然看見有一頭驢駒拴在街道旁一戶人家的門外,就上前解開牠。 5旁邊站著的幾個人就問他們:「你們為什麼要解開這頭驢駒?」

6門徒依照耶穌的吩咐回答,那些人就讓他們牽走了。 7他們把驢駒牽到耶穌面前,將自己的外衣搭在驢背上,耶穌就騎了上去。 8很多人把衣服鋪在路上,有人將田間的樹枝砍下來鋪在路上。 9大家前呼後擁,高聲歡呼:

「和散那11·9 和散那」原意是「拯救我們」,此處有「讚美」的意思。

奉主名來的當受稱頌!

10那將要來臨的我祖大衛的國度當受稱頌!

和散那歸於至高之處的上帝!」

11耶穌進了耶路撒冷,來到聖殿,巡視各處。那時天色已晚,耶穌便和十二門徒出城前往伯大尼

咒詛無花果樹

12第二天,他們離開伯大尼後,耶穌餓了。 13祂遠遠看見有一棵枝葉茂盛的無花果樹,就走過去找果子吃。到了樹下,卻什麼也找不到,只有滿樹的葉子,因為當時不是收無花果的季節。 14祂對那棵樹說:「願無人再吃你的果子!」祂的門徒都聽見了這句話。

潔淨聖殿

15他們來到耶路撒冷後,耶穌進入聖殿,趕走了裡面做買賣的人,推翻了兌換錢幣之人的桌子和賣鴿子之人的凳子, 16不准人抬著貨物穿過聖殿。 17祂教導他們說:「聖經上不是記載『我的殿必稱為萬民禱告的殿』嗎?你們竟把它變成了賊窩。」

18祭司長和律法教師聽到這番話後,就策劃如何殺害耶穌,只是有些怕祂,因為百姓都對祂的教導感到驚奇。 19到了傍晚,耶穌和門徒去了城外。

無花果樹的教訓

20早上,他們又經過那棵無花果樹,看見它連根都枯了。 21彼得想起昨天發生的事,就對耶穌說:「老師,你看!昨天你咒詛的無花果樹已經枯了。」

22耶穌說:「要對上帝有信心。 23我實在告訴你們,不論何人,只要有信心,毫不疑惑,就是對這座山說,『從這裡挪開,投進大海裡!』也必定為他成就。 24所以我告訴你們,你們禱告時無論求什麼,只要相信已經得到了,就必得到。 25你們站著禱告的時候,若想起有人得罪了你們,就要饒恕他。這樣,你們天上的父也會饒恕你們的過犯。 26你們如果不饒恕別人,你們天上的父也不會饒恕你們的過犯。11·26 有些古卷無此節。

質問耶穌的權柄

27他們再次回到耶路撒冷。耶穌在聖殿裡行走的時候,祭司長、律法教師和長老上前質問祂: 28「你憑什麼權柄做這些事?誰授權給你了?」

29耶穌說:「我也要問你們一個問題,你們回答了,我就告訴你們我憑什麼權柄做這些事。 30約翰的洗禮是從天上來的還是從人來的?請回答我!」

31他們彼此議論說:「如果我們說『是從天上來的』,祂一定會問,『那你們為什麼不信他?』 32如果我們說『是從人來的』,又怕觸怒百姓,因為他們都相信約翰真的是先知。」 33於是,他們回答說:「我們不知道。」耶穌說:「我也不告訴你們我憑什麼權柄做這些事。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 11:1-33

Yesu Aingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Mathayo 21:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

111:1 Mt 21:17; 21:1Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni. Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake, 211:2 Hes 19:2; 1Sam 6:7akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. 311:3 Mk 14:14Kama mtu yeyote akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa baada ya muda mfupi.’ ”

411:4 Mk 14:16Wakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa kando ya barabara, karibu na mlango wa nyumba. 5Walipokuwa wanamfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakawauliza, “Mna maana gani mnapomfungua huyo mwana-punda?” 6Wakawajibu kama vile Yesu alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu. 7Kisha wakamleta huyo mwana-punda kwa Yesu na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda. 811:8 Mt 21:8Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani. 911:9 Za 118:25-26; Mt 23:39Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema,

“Hosana!”11:9 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

1011:10 Lk 2:14“Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!”

“Hosana kwake yeye aliye juu!”

1111:11 Mt 21:12-17Yesu akaingia Yerusalemu na kwenda Hekaluni. Akaangalia kila kitu kilichokuwamo, lakini kwa kuwa ilishakuwa jioni, akaenda zake Bethania pamoja na wale kumi na wawili.

Yesu Alaani Mtini Usiozaa

(Mathayo 21:18-19)

1211:12 Mt 21:18Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 1411:14 Mk 11:20Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Yesu Atakasa Hekalu

(Mathayo 21:12-17; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)

1511:15 Mt 21:12; Lk 19:45; Yn 2:14Walipofika Yerusalemu, Yesu akaingia katika eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakinunua na kuuza humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, 16wala hakumruhusu mtu yeyote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu. 1711:17 Isa 56:7; Yer 7:11Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa:

“ ‘Nyumba yangu itaitwa

nyumba ya sala kwa mataifa yote’?

Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’ ”

1811:18 Mt 21:46; Lk 20:19; Mt 7:28Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote ulikuwa unashangazwa na mafundisho yake.

1911:19 Lk 21:37Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji.

Mtini Ulionyauka

(Mathayo 21:20-22)

2011:20 Mt 21:19; Mk 11:14Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 2111:21 Mt 23:7Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”

2211:22 Yn 14:1Yesu akawajibu, “Mwaminini Mungu. 2311:23 Mt 21:21Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ngʼoka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. 2411:24 Mt 7:7Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu. 2511:25 Mt 6:14Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [ 2611:26 Mt 18:35; 6:4, 15Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]”

Swali Kuhusu Mamlaka Ya Yesu

(Mathayo 21:23-27; Luka 20:1-8)

2711:27 Mt 21:23; Lk 20:1Wakafika tena Yerusalemu, na Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wa watu wakamjia. 28Wakamuuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka ya kufanya hayo?”

29Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 30Niambieni, je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

31Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 3211:32 Mt 11:9Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’…” (Waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana alikuwa nabii wa kweli.)

33Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatujui.”

Naye Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”