阿摩司書 4 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

阿摩司書 4:1-13

1住在撒瑪利亞山上的巴珊肥母牛啊,

你們要聽!

你們壓榨貧寒人,欺凌窮苦人,

又使喚丈夫倒酒暢飲。

2因此,主耶和華憑祂的聖潔起誓:

「時候快到了,

有人要用魚鉤鉤走你們,一個也不留。

3你們都要從城牆缺口走出來,

被丟到哈門

這是耶和華說的。

4以色列人啊,

你們去伯特利犯罪吧,

吉甲增添罪惡吧!

要每天早晨獻上祭物,

每三天奉上你們的十分之一。

5你們獻上帶酵的餅作感恩祭,

並且到處誇耀你們自願獻的祭。

以色列人啊,這就是你們愛做的事。

這是主耶和華說的。

6「我在各城降下饑荒,

使你們遍地缺糧。

儘管如此,你們仍不歸向我。

這是耶和華說的。

7「我在收割前三個月停止降雨。

我在一座城降雨,

在另一座城不降雨;

我使一塊田有雨水的滋潤,

另一塊田因無雨而乾裂。

8兩三座城的人都踉踉蹌蹌地湧到一座城找水喝,

水卻不夠喝。

儘管如此,你們仍不歸向我。

這是耶和華說的。

9「我用熱風和黴災擊打你們,

叫蝗蟲吞噬你們田園中的菜蔬、葡萄樹、無花果樹和橄欖樹。

儘管如此,你們仍不歸向我。

這是耶和華說的。

10「我在你們中間降下瘟疫,

如從前降在埃及一樣。

我殺戮你們的青年,

擄掠你們的戰馬,

使你們軍營中的死屍臭味撲鼻。

儘管如此,你們仍不歸向我。

這是耶和華說的。

11「我在你們中間施行毀滅,

如從前毀滅所多瑪蛾摩拉一樣,

使你們像從火裡抽出的一根柴。

儘管如此,你們仍不歸向我。

這是耶和華說的。

12以色列人啊,

我要這樣懲罰你們。

以色列人啊,

準備迎見你們的上帝吧!

因為我要這樣懲罰你們。」

13看啊,那位造山又造風,

向人顯明祂的心意,

將黎明變為黑暗,

將群山踩在腳下的——

祂的名字是萬軍之上帝耶和華。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Amosi 4:1-13

Israeli Hajarudi Kwa Mungu

14:1 Za 22:12; Isa 58:6; Eze 39:18; 18:12; Amo 3:9; 2:8; 8:6; Yer 44:19Sikilizeni neno hili, ninyi ngʼombe wa Bashani

mlioko juu ya Mlima Samaria,

ninyi wanawake mnaowaonea maskini,

na kuwagandamiza wahitaji,

na kuwaambia wanaume wenu,

“Tuleteeni vinywaji!”

24:2 Amo 6:8; Isa 19:8; Yer 31:31; 2Fal 19:28; 2Nya 33:11Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake:

“Hakika wakati utakuja

mtakapochukuliwa na kulabu,

na wanaosalia kwa ndoana za samaki.

34:3 Eze 12:5Nanyi mtakwenda moja kwa moja

kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta,

nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,”

asema Bwana.

44:4 Hos 4:15; Hes 28:3, 4; 28:3; Eze 20:39; Kum 14:28; Yos 7:2; Amo 5:21, 22“Nendeni Betheli mkatende dhambi;

nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi.

Leteni dhabihu zenu kila asubuhi,

zaka zenu kila mwaka wa tatu.

5Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani,

jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari:

jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli,

kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,”

asema Bwana Mwenyezi.

64:6 Isa 9:13; 1Fal 17:1; Hag 2:17; Yer 5:3; Hos 5:15“Niliwapa njaa kwenye kila mji,

na ukosefu wa chakula katika kila mji,

hata hivyo bado hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

74:7 Kum 11:17; Isa 5:6; Zek 14:17; Kut 9:4, 26; 2Nya 7:13“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu

kabla ya kufikia mavuno.

Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,

lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.

Shamba moja lilipata mvua,

na lingine halikupata, nalo likakauka.

84:8 Eze 4:16-17; Ay 36:31; Yer 14:4; 2:7; Hag 1:6Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji,

lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

94:9 Kum 28:22; Isa 9:13; Hag 2:17; Yer 3:10; Yoe 1:7; 2:25; Kut 10:13“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu,

niliyapiga kwa kutu na ukungu.

Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

104:10 Kut 9:3; 11:5; Kum 28:27; Isa 9:13, 17“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu

kama nilivyofanya kule Misri.

Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga,

niliwachukua farasi wenu.

Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

114:11 Mwa 19:29; Yer 23:14; Isa 7:4; 13:19; Zek 3:2; Yud 23; Ay 36:13“Niliwaangamiza baadhi yenu kama

nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.

Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni,

hata hivyo hamjanirudia,”

asema Bwana.

12“Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli,

na kwa sababu nitawafanyia hili,

jiandaeni kukutana na Mungu wenu, ee Israeli.”

134:13 Dan 2:28; Za 65:6; 135:7; Yn 2:25; Amo 9:6; 5:8, 27; Isa 47:4Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo,

na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu,

yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza,

na kukanyaga mahali pa juu pa nchi:

Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.