路加福音 14 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

路加福音 14:1-35

論安息日治病

1有個安息日,耶穌到一位法利賽人的首領家裡作客,人們密切地監視祂。 2當時有一個患水腫病的人在耶穌面前, 3耶穌問法利賽人和律法教師:「在安息日可以醫病嗎?」

4他們都閉口不言。耶穌便扶著那人把他醫好,叫他走了, 5然後又問他們:「如果你們有驢14·5 」另有抄本作「兒子」。或牛在安息日掉進井裡,難道你們不會立刻把牠拉上來嗎?」 6他們都啞口無言。

論謙卑

7耶穌在宴席中看見賓客們都爭著坐首位,就用比喻對他們說: 8「參加婚宴的時候,不要坐在首位,因為或許有更尊貴的賓客來赴宴, 9主人會把他帶到你面前,說,『請你把首位讓給他吧!』你就要滿面羞愧地退到末位去了。 10你去赴宴時,應該先坐在末位,這樣主人會對你說,『朋友,請上坐!』那時,你在賓客面前就有光彩了。 11因為自高的人必遭貶抑,謙卑的人必得尊榮。」

論待客之道

12耶穌又對主人說:「擺設午宴、晚宴時,不要邀請你的朋友、弟兄、親戚或有錢的鄰居,免得他們回請你,你便得到報答了。 13相反,你設宴時,要邀請貧窮的、殘疾的、瘸腿的、瞎眼的, 14這樣你就有福了,因為他們都沒有能力回報你,到了義人復活那天,上帝一定會賞賜你。」

大宴席的比喻

15同席的一個客人聽了這番話,就對耶穌說:「能夠在上帝的國坐席的人多麼有福啊!」

16於是,耶穌對他說:「有一個人大擺宴席,邀請了許多客人。 17要開席的時候,主人就派奴僕去對客人說,『一切都準備好了,來赴宴吧!』 18可是,他們都找藉口推辭。頭一個說,『我剛買了一塊田,必須去看一看,請恕我不能參加。』 19另一個說,『我新買了五對牛,要去試一試,請恕我不能參加。』 20還有一個說,『我剛結了婚,所以不能去。』 21奴僕回來將這些話告訴主人,主人非常生氣,於是對奴僕說,『快出去到城裡的大街小巷把貧窮的、殘疾的、瘸腿的、瞎眼的都請來。』 22奴僕說,『主人啊,我照你的吩咐辦了,可是還有空位。』 23主人又說,『出去到大路上、籬笆旁硬把人拉來,讓我家裡座無虛席。 24我告訴你們,原來邀請的那些人沒有一個能嚐到我的宴席!』」

做門徒的代價

25有一大群人跟著耶穌,祂轉身對他們說: 26「若有人要跟從我,就要愛我勝過愛他的父母、妻子、兒女、弟兄、姊妹,甚至自己的生命,否則就不能作我的門徒。 27若不背起自己的十字架跟從我,就不能作我的門徒。

28「哪有人建樓房不事先坐下來計算成本,看能否建成? 29否則,打好了地基卻不能完工,徒惹別人嘲笑, 30『這個人開了工,卻不能完工!』

31「哪有王要跟另一個王打仗時,不先坐下來酌量一下自己的一萬人是否敵得過對方的兩萬人? 32如果自知不敵,一定趁敵人還遠的時候,就差使者去求和。

33「同樣,你們若不撇下一切,就不能作我的門徒。 34鹽本來是好的,但如果鹽失去了鹹味,怎能使它再變鹹呢? 35沒有味的鹽,既不利於土壤,也不適宜作肥料,只好丟掉。有耳可聽的,就應當聽。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 14:1-35

Yesu Nyumbani Mwa Farisayo

114:1 Lk 7:36; 11:37; Mt 12:10Ikawa siku moja Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo siku ya Sabato, watu walikuwa wakimchunguza kwa bidii. 2Papo hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. 314:3 Mt 22:25; 12:10Yesu akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa sheria, “Je, ni halali kuponya watu siku ya Sabato au la?” 4Wakakaa kimya. Hivyo Yesu akamshika yule mgonjwa mkono na kumponya, akamruhusu aende zake.

514:5 Lk 13:15Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ngʼombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” 6Nao hawakuwa na la kusema.

Unyenyekevu Na Ukarimu

714:7 Lk 11:43Alipoona jinsi wageni walivyokuwa wanachagua mahali pa heshima wakati wa kula, akawaambia mfano huu: 814:8 Mit 25:6“Mtu akikualika arusini, usikae mahali pa mgeni wa heshima kwa kuwa inawezekana amealikwa mtu mheshimiwa kuliko wewe. 9Kama mkifanya hivyo yule aliyewaalika ninyi wawili atakuja na kukuambia, ‘Mpishe huyu mtu kiti chako.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kukaa katika nafasi ya chini kabisa. 1014:10 Mit 25:6, 7Badala yake, unapoalikwa, chagua nafasi ya chini, ili yule mwenyeji wako atakapokuona atakuja na kukuambia, ‘Rafiki yangu, nenda kwenye nafasi iliyo bora zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wenzako wote. 1114:11 Mt 23:12; Lk 18:14Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”

12Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, wao nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umelipwa kile ulichofanya na kupata thawabu yako. 1314:13 Neh 8:10, 12; Kum 14:29Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu, 1414:14 Mdo 24:15; Yn 5:29nawe utabarikiwa kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa. Mungu atakulipa wakati wa ufufuo wa wenye haki.”

Mfano Wa Karamu Kuu

(Mathayo 22:1-10)

1514:15 Isa 25:6; Ufu 19:9; Mt 3:2Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Yesu, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya Ufalme wa Mungu!”

1614:16 Mt 22:2Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 1714:17 Mit 9:2, 3Wakati wa karamu ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaambie wale walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ki tayari sasa.’

18“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’

19“Mwingine akasema, ‘Ndipo tu nimenunua jozi tano za ngʼombe wa kulimia, nami ninakwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 2014:20 1Kor 7:33Naye mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

2114:21 Lk 14:13“Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake, akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’

22“Yule mtumishi akamwambia, ‘Bwana, yale uliyoniagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’

23“Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na vijia vilivyoko nje ya mji na uwalazimishe watu waingie ili nyumba yangu ipate kujaa. 2414:24 Mt 21:43; Mdo 13:46Kwa maana nawaambia, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeionja karamu yangu.’ ”

Gharama Ya Kuwa Mwanafunzi

(Mathayo 10:37-38)

25Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukisafiri pamoja na Yesu, naye akageuka, akawaambia, 2614:26 Mt 10:37; Yn 12:25“Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. 2714:27 Mt 10:38; Lk 9:23Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

2814:28 Mit 24:27“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? 29La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, 30wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’

31“Au ni mfalme gani atokaye kwenda kupigana vita na mfalme mwingine, ambaye hakai chini kwanza na kufikiri iwapo akiwa na jeshi la watu 10,000 ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu 20,000? 32Kama hawezi, basi wakati yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma ujumbe wa watu na kuomba masharti ya amani. 3314:33 Flp 3:7-8Vivyo hivyo, yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Chumvi Isiyofaa

(Mathayo 5:13; Marko 9:50)

3414:34 Mk 9:50“Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itafanywaje ili iweze kukolea tena? 3514:35 Mt 5:13; 11:15Haifai ardhi wala kwa lundo la mbolea, bali hutupwa nje.

“Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”