耶利米書 52 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 52:1-34

猶大的滅亡

1西底迦二十一歲登基,在耶路撒冷執政十一年。他母親叫哈慕她,是立拿耶利米的女兒。 2西底迦約雅敬一樣做耶和華視為惡的事。 3因此,耶和華向耶路撒冷猶大的人發怒,把他們從祂面前趕走。

後來,西底迦背叛了巴比倫王。 4在他執政第九年十月十日,巴比倫尼布甲尼撒率領全軍攻打耶路撒冷,在城外紮營,修築圍城的高臺。 5城一直被圍困到西底迦執政第十一年。 6那年四月九日,城裡饑荒非常嚴重,百姓無糧可吃。 7城被攻破,西底迦和士兵便在夜間穿過御花園,從兩城牆中間的門逃往亞拉巴。當時迦勒底人仍四面包圍著城。 8迦勒底的軍隊追趕西底迦,在耶利哥平原追上了他。他的軍隊都四散而逃。 9迦勒底人擒住西底迦,把他押到哈馬利比拉去見巴比倫王。巴比倫王在那裡審判他, 10當著他的面殺了他的眾子和猶大所有的首領, 11又剜去他的雙眼,用銅鏈鎖著他押往巴比倫,將他終生囚在牢裡。

12巴比倫尼布甲尼撒執政第十九年五月十日,他的臣僕——護衛長尼布撒拉旦進入耶路撒冷13放火焚燒耶和華的殿、王宮及城內所有的房屋。他燒毀了所有重要建築。 14他率領的迦勒底的軍隊拆毀了耶路撒冷四圍的城牆。 15護衛長尼布撒拉旦擄去最貧窮的人、城中的餘民、投降的人和剩下的技工, 16只留下一些最貧窮的人,讓他們照料葡萄園、耕種田地。

17迦勒底人打碎耶和華殿中的銅柱、銅底座和銅海,把銅運往巴比倫18並帶走了盆、鏟、蠟剪、碗、碟及一切獻祭用的銅器。 19護衛長還帶走了杯、火鼎、碗、盆、燈臺、碟和奠酒的杯等所有金銀器皿。 20所羅門王為耶和華的殿所造的兩根銅柱、一個銅海、銅海下面的十二頭銅牛,以及一些銅底座,用的銅多得無法計算。 21兩根銅柱中空,高八米,周長五點三米,銅壁厚四指。 22銅柱有柱冠,柱冠高二點三米,周圍裝飾著銅網和銅石榴。兩根柱子都一樣。 23每根銅柱周圍裝飾著九十六個石榴,網子四周共有一百個石榴。

24護衛長擄走祭司長西萊雅、副祭司長西番亞、三名殿門守衛, 25又從城中擄走一名將領、王的七個親信、一名負責招兵的書記和六十名平民, 26把他們帶到利比拉去見巴比倫王。 27巴比倫王在那裡處死了他們。猶大人就這樣被擄去,離開了家園。

28以下是尼布甲尼撒擄去的人數:他執政第七年擄去三千零二十三名猶大人; 29執政第十八年,從耶路撒冷擄去八百三十二人; 30執政第二十三年,他的護衛長尼布撒拉旦擄去七百四十五名猶大人。總共四千六百人。

31猶大約雅斤被擄後第三十七年,即巴比倫以未·米羅達元年十二月二十五日,巴比倫王恩待約雅斤,釋放了他, 32並好言相待,使他的地位高過被擄到巴比倫的其他各王。 33約雅斤脫去了囚服,終生與巴比倫王一起吃飯。 34在他有生之年,巴比倫王供應他每天的需用,直到他去世。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 52:1-34

Anguko La Yerusalemu

(2 Wafalme 24:18–25:30)

152:1 2Fal 24:17-18; Yos 10:29; Hes 33:20; 2Fal 8:22Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna. 252:2 Yer 36:30Alifanya maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Yehoyakimu. 352:3 Eze 17:12-16; Kut 33:15; Mwa 4:14Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya Bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake.

Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

452:4 Zek 8:19; 2Fal 25:1-7; Yer 34:1; Eze 24:1-2; Kum 28:52-57Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Wakapiga kambi nje ya mji na kuuzunguka mji pande zote. 5Mji ulizungukwa na jeshi mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia.

652:6 Law 26:26; Mao 1:11; Eze 4:16Ilipowadia siku ya tisa ya mwezi wa nne, njaa ikazidi kuwa kali sana ndani ya mji, hadi hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu. 752:7 Mao 4:19Kisha ukuta wa mji ukavunjwa na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba. 8Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia Mfalme Sedekia na kumpata katika sehemu tambarare za Yeriko. Askari wake wote wakatengwa naye na kutawanyika, 952:9 Yer 21:7; 32:4; Hes 34:11; 13:21naye akakamatwa.

Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mahali ambapo alimtangazia hukumu. 1052:10 Yer 22:30; 39:6-7Huko Ribla mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake. Pia akawaua maafisa wote wa Yuda. 1152:11 Eze 12:13; 17:16; Yer 34:4Kisha akayangʼoa macho ya Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli, alipomweka gerezani mpaka siku ya kifo chake.

1252:12 Zek 8:19; Yer 39:9; Zek 7:5Mnamo siku ya kumi ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme, aliyemtumikia mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu. 1352:13 2Nya 36:19; Kum 29:24; Mik 3:12; Za 74:8; Yer 19:13; Kum 13:16; Mao 2:6Alichoma moto Hekalu la Bwana, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Aliteketeza kila jengo muhimu. 14Jeshi lote la Wakaldayo chini ya jemadari wa askari walinzi wa mfalme walivunja kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu. 1552:15 2Fal 24:1; Yer 38:19; 1:3Nebuzaradani, jemadari wa askari walinzi, akawapeleka uhamishoni baadhi ya watu maskini sana na wale waliobaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli. 16Lakini Nebuzaradani akawaacha mabaki ya wale watu maskini kabisa ili watunze mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.

1752:17 1Fal 7:15, 27-37; Yer 27:19-22Wakaldayo walivunja vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Bwana. Hivyo wakaichukua hiyo shaba yote na kuipeleka Babeli. 1852:18 Kut 27:3; 1Fal 7:45; Hes 4:14Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika katika huduma ya Hekalu. 1952:19 Law 10:1; 1Fal 7:50; Hes 3:31; Kut 25:29; Hes 4:7; Dan 5:2; Ezr 1:7Jemadari wa askari walinzi wa mfalme akachukua yale masinia, vile vyetezo, yale mabakuli ya kunyunyizia, zile sufuria, vile vinara vya taa, zile sahani na yale mabakuli yaliyotumika kwa sadaka za vinywaji, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha.

2052:20 1Fal 7:25, 47Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na wale mafahali kumi na mawili wa shaba waliokuwa chini yake, pamoja na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Mfalme Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika. 21Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane, kimo chake na mzunguko dhiraa kumi na mbili, na unene wa nyanda nne, na zote zilikuwa wazi ndani. 2252:22 1Fal 7:15-16, 20, 47; Kut 28:33Sehemu ya shaba juu ya ile nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tano, na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na makomamanga yake ilifanana na hiyo ya kwanza. 23Kulikuwa na makomamanga tisini na sita pembeni; jumla ya makomamanga juu ya wavu uliokuwa umezunguka yalikuwa mia moja.

2452:24 2Fal 25:18; Yer 37:3; 21:1; 2Fal 12:9Yule jemadari wa askari walinzi akawachukua kama wafungwa Seraya kuhani mkuu, kuhani Sefania aliyefuata kwa cheo, na mabawabu watatu. 2552:25 Yer 36:10Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri saba wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji. 26Nebuzaradani jemadari akawachukua hao wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. 2752:27 Yer 20:4; Law 26:33; Hes 34:11Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe.

Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao. 2852:28 2Fal 24:14-16; Neh 1:2; 2Nya 36:20; Kum 28:36Hii ndiyo hesabu ya watu ambao Nebukadneza aliwachukua kwenda uhamishoni:

katika mwaka wa saba,

Wayahudi 3,023;

29katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza,

watu 832 kutoka Yerusalemu;

3052:30 Yer 43:3; 13:19katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake,

Wayahudi 745 walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme.

Jumla ya watu wote walikuwa 4,600.

Yehoyakini Anaachiwa Huru

3152:31 2Fal 25:27-30; Mwa 40:13-20Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki52:31 Pia aliitwa Ameli-Mariduki. alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini mfalme wa Yuda, na kumfungua kutoka gerezani siku ya ishirini na tano ya mwezi wa kumi na mbili. 32Alizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima zaidi kuliko wale wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli. 3352:33 2Sam 9:7, 13Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya mfungwa, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme. 3452:34 2Sam 9:10Siku kwa siku mfalme wa Babeli alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake, hadi siku ya kifo chake.