耶利米書 48 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 48:1-47

關於摩押的預言

1論到摩押以色列的上帝——萬軍之耶和華說:

尼波大禍臨頭了!

它必被毀滅;

基列亭必蒙羞淪陷,

堡壘必蒙羞被毀。

2摩押不再受稱讚,

敵人在希實本圖謀害她,說,

『來吧!我們剷除這個國家。』

瑪得緬啊,你也將被敵人追殺,

變得死寂無聲。

3「從何羅念傳來呼喊聲,

『荒涼了!毀滅了!』

4摩押滅亡了,

她的孩童放聲哀哭。

5摩押人痛哭著走上魯希坡,

他們在何羅念的山坡下聽見悲慘的哀號。

6逃命吧!藏到曠野去吧!

7摩押啊,你要被攻佔,

因為你倚仗自己的成就和財富。

你的神明基抹及供奉它的祭司和官長都要被擄去。

8所有的城邑必被毀滅,

無一倖免;

山谷遭踐踏,

平原被蹂躪。

這是耶和華說的。

9「給摩押翅膀讓她飛走吧48·9 給摩押翅膀讓她飛走吧,」或譯作「給摩押豎起墓碑吧,因為她將被毀滅」或「在摩押撒鹽吧,因為她將被毀滅」。

因為她的城邑將淪為廢墟,

杳無人跡。

10不殷勤地為耶和華做工,

不揮刀斬殺摩押人的必受咒詛。

11摩押自幼常享安逸,

從未被擄到別處,

好像沉澱的酒沒有被從這缸倒到那缸,

味道依舊,香氣未變。

12「不過,看啊,時候將到,我要派倒酒的人去把她倒出來,倒空酒缸,把缸打碎。這是耶和華說的。 13摩押人必因他們的神明基抹而羞愧,就像以色列人因信靠伯特利的神像而羞愧一樣。

14摩押人啊,

你們怎能自稱為驍勇善戰的英雄呢?

15摩押要滅亡了,

她的城邑要被摧毀,

她最勇敢的青年將被殺戮。

這是名叫萬軍之耶和華的君王說的。

16摩押快要被毀滅了,

災難就要來臨。

17她的近鄰和知道她名望的人啊,

你們都要為她哀悼,

『那強大、輝煌的權勢竟然崩潰了!』

18底本的居民啊,

你們要從榮耀的位子上下來,

坐在乾旱的地上,

因為毀滅摩押的要來攻擊你們,

摧毀你們的堡壘。

19亞羅珥的居民啊!

你們要站在路旁觀望,

詢問逃難的男女究竟發生了什麼事。

20你們會得知摩押淪陷了,

她羞愧難當。

你們哀傷痛哭吧!

你們要在亞嫩河邊宣告,

摩押滅亡了!』

21「審判降臨在平原上的何倫雅雜米法押22底本尼波伯·低比拉太音23基列亭伯·迦末伯·米恩24加略波斯拉摩押各地的城邑。 25摩押的權勢被粉碎了,她的力量被摧毀了。這是耶和華說的。

26「你們要灌醉她,因為她藐視耶和華。她必在自己的嘔吐物中打滾,被人恥笑。 27摩押啊,你不是曾經嘲笑以色列嗎?以色列難道是強盜嗎?你每次談到她總是不屑地搖頭。

28摩押人啊,

你們要離開城邑,住到岩洞裡,

像鴿子在岩縫裡築巢一樣。

29我們聽說摩押人傲氣沖天,

他們狂妄自大、心中高傲。

30我知道狂傲的摩押不過是外強中乾,

她的誇耀不過是虛張聲勢。

這是耶和華說的。

31因此,我要為她哀號,

摩押人痛哭,

吉珥·哈列設人悲傷。

32西比瑪的葡萄樹啊,

我為你們比為雅謝人哭得更悲痛!

你們的枝條雖然延伸到大海,

一直到雅謝

但毀滅者已在蹂躪你們夏日的果子了!

33摩押的沃土上再沒有歡喜快樂的聲音。

我使榨酒池不出酒,

再沒有踩踏葡萄的歡呼聲,

歡呼被呐喊取代。

34「哀哭聲從希實本傳到以利亞利雅雜,又從瑣珥傳到何羅念伊基拉·施利施亞,因為連寧林的水也乾涸了。」 35耶和華說:「我要滅絕摩押那些在邱壇獻祭和向假神燒香的人。 36我的心為摩押悲鳴,好像淒涼的簫聲;我的心為吉珥·哈列設人悲鳴,他們的一切財富都消失了。 37他們都悲哀地剃去髮鬚,割傷雙手,腰束麻布。 38摩押境內的屋頂和街頭巷尾,哀聲處處可聞,因為我已把摩押打得粉碎,好像打碎沒人要的器皿。這是耶和華說的。 39摩押破碎不堪!她嚎啕痛哭,羞愧難當,令四圍的人嗤笑、驚懼。」

40耶和華說:

「看啊,敵人必像展翅疾飛的大鷹一樣來攻擊摩押

41他們要攻取城池,佔領堡壘。

那時,摩押的勇士像臨盆的婦人一樣心驚膽戰。

42摩押必被摧毀,徹底滅亡,

因為她藐視耶和華。

43摩押人啊!

你們要充滿恐懼,

陷入深坑和網羅。

這是耶和華說的。

44逃過驚恐的必落入深坑,

爬出深坑的必陷入網羅,

因為我懲罰摩押的時候到了。

這是耶和華說的。

45「逃難的人來到希實本

無助地站著,

因為希實本烈焰熊熊,

西宏的城火光沖天,

燒毀了摩押和其中的叛逆之人。

46基抹神明的摩押人啊,

你們有禍了!

你們滅亡了!

你們的兒女都被擄去了。

47但將來,我要使你們重整家園。

這是耶和華說的。」

摩押的審判到此為止。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 48:1-47

Ujumbe Kuhusu Moabu

148:1 Hes 32:37; Yos 13:19; Mwa 19:37; Kum 23:6Kuhusu Moabu:

Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

“Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.

Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;

Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.

248:2 Hes 21:25; Isa 16:14; Yos 23:16Moabu haitasifiwa tena;

huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:

‘Njooni na tuangamize taifa lile.’

Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;

upanga utakufuatia.

3Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,

kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.

4Moabu utavunjwa,

wadogo wake watapiga kelele.

548:5 Isa 15:5Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,

wakilia kwa uchungu wanapotembea,

kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,

kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.

648:6 Yer 17:6; Mwa 19:17Kimbieni! Okoeni maisha yenu,

kuweni kama kichaka jangwani.

748:7 Hes 21:29; Isa 46:1-2; Yer 49:3; 9:23; Za 49:6; Mk 11:28; Amo 2:3Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu,

ninyi pia mtachukuliwa mateka,

naye Kemoshi48:7 Kemoshi alikuwa mungu wa Wamoabu. atakwenda uhamishoni,

pamoja na makuhani wake na maafisa wake.

848:8 Kut 12:23; Yer 4:7; Yos 13:9Mharabu atakuja dhidi ya kila mji,

wala hakuna mji utakaookoka.

Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa,

kwa sababu Bwana amesema.

948:9 Amu 9:45; Yer 51:29Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,

kwa kuwa ataangamizwa;

miji yake itakuwa ukiwa,

pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

1048:10 Yer 47:6; 1Fal 20:42; 1Sam 15:3, 11; 2Fal 13:15-19“Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila!

Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!

1148:11 Zek 1:15; Sef 1:12“Moabu amestarehe tangu ujana wake,

kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,

haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,

hajaenda uhamishoni.

Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,

nayo harufu yake haijabadilika.

12Lakini siku zinakuja,”

asema Bwana,

“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,

nao watamimina;

wataacha magudulia yake yakiwa matupu

na kuvunja mitungi yake.

1348:13 Hos 10:6; Amu 11:24; Yos 7:2Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,

kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu

walipotegemea mungu wa Betheli.48:13 Betheli ina maana ya Nyumba ya Mungu; lakini pia ni mahali ambapo Mfalme Yeroboamu alisimamisha moja ya sanamu za ndama ili kuabudiwa; nyingine aliiweka huko Dani (1Fal 12:29-33).

1448:14 Mhu 9:11; Za 33:16“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,

watu jasiri katika vita’?

1548:15 Yer 50:27; 51:40, 57; 46:18; Isa 9:17Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,

vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”

asema Mfalme, ambaye jina lake

ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

16“Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,

janga kubwa litamjia kwa haraka.

1748:17 Za 110:2; 2Fal 3:4-5Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,

ninyi nyote mnaojua sifa zake,

semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,

tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’

1848:18 Isa 47:1; Hes 21:30; Yos 13:9“Shuka kutoka fahari yako

na uketi katika ardhi iliyokauka,

enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,

kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako,

na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma.

1948:19 Hes 32:34; Kum 2:36Simama kando ya barabara na utazame,

wewe unayeishi Aroeri.

Muulize mwanaume anayekimbia

na mwanamke anayetoroka,

waulize, ‘Kumetokea nini?’

2048:20 Isa 16:7; Hes 21:13Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa.

Lieni kwa huzuni na kupiga kelele!

Tangazeni kando ya Arnoni

kwamba Moabu ameangamizwa.

2148:21 Hes 21:23; Isa 15:4; Yos 13:18; 15:51; 13:9, 21Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu:

katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,

2248:22 Hes 21:30; Yos 13:9, 17; Hes 32:38katika Diboni, Nebo

na Beth-Diblathaimu,

2348:23 Hes 32:38; Yos 13:17-19katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli

na Beth-Meoni,

2448:24 Amo 2:2; Yer 49:13; Isa 15:1katika Keriothi na Bosra;

kwa miji yote ya Moabu,

iliyoko mbali na karibu.

2548:25 Za 75:10; Eze 30:21; Za 37:17Pembe48:25 Pembe hapa ni ishara ya nguvu. ya Moabu imekatwa,

mkono wake umevunjwa,”

asema Bwana.

2648:26 Yer 25:16, 27; 51:39; Isa 28:8; 1Sam 17:26“Mlevye,

kwa kuwa amemdharau Bwana.

Moabu na agaegae katika matapishi yake,

yeye na awe kitu cha dhihaka.

2748:27 Mit 24:17; Yer 2:26; Ay 16:4; Za 44:14; Mik 7:8-10; Kum 7:8-10; Sef 2:8Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?

Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,

kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau

kila mara unapozungumza juu yake?

2848:28 Za 55:6-7; Wim 1:15; Amu 6:2; Wim 2:14; Mwa 8; 8Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,

enyi mnaoishi Moabu.

Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake

kwenye mdomo wa pango.

2948:29 Law 26:19; Isa 16:6; Ay 40:12; Mit 10:5; 16:18“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:

kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,

kiburi chake na ufidhuli wake,

na kujivuna kwa moyo wake.

30Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”

asema Bwana,

“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote.

3148:31 Isa 15:5-6; 2Fal 3:25Kwa hiyo namlilia Moabu,

kwa ajili ya Moabu yote ninalia,

ninaomboleza kwa ajili

ya watu wa Kir-Haresethi.

3248:32 Hes 32:3; 21:13; Isa 16:8-9; Yos 13:25Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo,

enyi mizabibu ya Sibma.

Matawi yako yameenea hadi baharini;

yamefika hadi bahari ya Yazeri.

Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva

na mizabibu yako iliyoiva.

3348:33 Isa 16:10; 24:7; Amo 5:17; Yoe 1:12Shangwe na furaha vimetoweka

kutoka bustani na mashamba ya Moabu.

Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo;

hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe.

Ingawa kuna kelele,

sio kelele za shangwe.

3448:34 Isa 15:4-6; Hes 32:3; 21:23; Mwa 13:10; Yos 13:26; Hes 21:25“Sauti ya kilio chao inapanda

kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi,

kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya,

kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka.

3548:35 Isa 15:2; 16:12; Yer 11:13Nitakomesha wale wote katika Moabu

watoao sadaka mahali pa juu,

na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”

asema Bwana.

3648:36 Isa 16:11; 15:7; Mit 11:4; 2Fal 3:25“Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;

unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.

Utajiri waliojipatia umetoweka.

3748:37 Isa 15:2; Eze 29:18; Isa 3:24; Amo 8:10; Eze 27:31; 2Sam 10:4Kila kichwa kimenyolewa

na kila mwenye ndevu zimekatwa;

kila mkono umekatwa

na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.

3848:38 Yer 22:28; Isa 15:3Juu ya mapaa yote katika Moabu

na katika viwanja

hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo,

kwa kuwa nimemvunja Moabu

kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,”

asema Bwana.

39“Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!

Jinsi wanavyolia kwa huzuni!

Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!

Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,

kitu cha kutisha kwa wale wote

wanaomzunguka.”

4048:40 Kum 28:29; Hab 1:8; Isa 8:8; Yer 49:22Hili ndilo asemalo Bwana:

“Tazama! Tai anashuka chini,

akitanda mabawa yake juu ya Moabu.

4148:41 Isa 21:3; Mik 4:9; Amo 2:16; Isa 15:1Miji itatekwa na ngome zake

zitatwaliwa.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu

itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

4248:42 Za 83:4; Isa 16:14; Mit 16:18Moabu ataangamizwa kama taifa

kwa sababu amemdharau Bwana.

4348:43 Isa 24:17, 18; Yer 49:5Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea,

enyi watu wa Moabu,”

asema Bwana.

4448:44 1Fal 19:17; Ay 20:24; Yer 11:23; 23:12; Isa 24:18“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu

ataanguka ndani ya shimo,

yeyote atakayepanda kutoka shimoni,

atanaswa katika mtego,

kwa sababu nitaletea Moabu

mwaka wa adhabu yake,”

asema Bwana.

4548:45 Hes 21:21, 26-28; Yos 12:2; Hes 24:17“Katika kivuli cha Heshboni,

wakimbizi wamesimama pasipo msaada,

kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,

mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;

unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,

mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.

4648:46 Hes 21:29; Amu 11:24Ole wako, ee Moabu!

Watu wa Kemoshi wameangamizwa;

wana wako wamepelekwa uhamishoni

na binti zako wamechukuliwa mateka.

4748:47 Za 14:7; Dan 11:41; Yer 49:6; Isa 11:1; Yer 12:15; Eze 16:53“Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,

katika siku zijazo,”

asema Bwana.

Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.