耶利米書 37 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 37:1-21

西底迦求耶利米代禱

1巴比倫尼布甲尼撒約西亞的兒子西底迦代替約雅敬的兒子哥尼雅做猶大王。 2西底迦和他的臣僕及人民卻沒有聽從耶和華藉耶利米先知說的話。 3西底迦王派示利米雅的兒子猶甲瑪西雅的兒子祭司西番雅來對耶利米先知說:「求你為我們向我們的上帝耶和華禱告。」 4當時,耶利米還可以自由來往,沒有被他們囚在獄中。 5那時,法老的軍隊已從埃及出發,正在圍攻耶路撒冷迦勒底人聽見消息就退兵了。

6耶和華對耶利米先知說: 7「這是以色列的上帝耶和華的話,『猶大王派你們來求問我,你們告訴他,前來支援你們的法老軍隊必中途返回埃及8迦勒底人必捲土重來,攻佔這城,將它付之一炬。 9耶和華說,你們不要自欺,以為迦勒底人必撤軍。其實他們不會撤軍。 10即使你們能打敗迦勒底全軍,他們營中受傷的殘兵也必起來燒毀這城。』」

11迦勒底人因害怕法老的軍隊而撤軍的時候, 12耶利米起身離開耶路撒冷,前往便雅憫境內去接收他在同族中應得的地業。 13耶利米先知來到便雅憫門時,哈拿尼亞的孫子、示利米雅的兒子守門官伊利雅逮捕了他,說:「你想去投奔迦勒底人!」 14耶利米說:「不,我不是去投奔迦勒底人。」但伊利雅不信,把他押到眾官長那裡。 15官長們大怒,命人鞭打耶利米,把他囚禁在書記約拿單的房子裡,因為他們已把這房子改作監牢。 16耶利米被囚禁在地牢中許多天。

17後來,西底迦王派人把他帶到自己的宮中,私下問他:「耶和華有什麼話給你嗎?」耶利米說:「有,你要被交在巴比倫王手中。」 18耶利米又問他:「我在什麼事上得罪了你、你的臣僕或人民,以致你們把我囚在監牢中? 19那些曾向你們預言『巴比倫王絕不會來這裡攻打你們』的先知如今在哪裡呢? 20現在,我主我王啊,請聽我說!求你不要把我送回書記約拿單的房子,免得我死在那裡。」

21於是,西底迦王下令把耶利米囚在護衛兵的院子裡,派人每天從餅鋪取一個餅給他,直到城中絕糧。耶利米就這樣住在護衛兵的院子裡。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 37:1-21

Yeremia Gerezani

137:1 2Fal 14:17; 1Nya 3:16; Eze 17:13; 2Nya 36:10; 24:8, 12; Yer 22:24Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini37:1 Yehoyakini ni jina jingine la Yekonia au Konia. mwana wa Yehoyakimu. 237:2 2Fal 24:19; 2Nya 36:12-14; Mit 29:12Lakini sio Sedekia, wala watumishi wake, wala watu wa nchi walisikiliza maneno ya Bwana aliyonena kupitia kwa nabii Yeremia.

337:3 2Fal 25:18; Yer 52:24; Hes 21:7; 1Sam 12:19; Yer 38:14; Kut 8:28; 1Fal 13:6Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa Bwana, Mungu wetu.”

437:4 Yer 32:2Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. 537:5 Mwa 15; 18; Yer 34:21; 31:1; Isa 30:5; 2Fal 24:7; Eze 17:15Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu.

6Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema: 737:7 Mwa 25:22; 2Fal 22:18; 18:21; Yer 2:12; 36; Mao 4:17“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri. 837:8 Yer 21:10; 39; 8; Mit 21:30; Yer 38:3, 8Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’

937:9 Yer 29:8; Mk 13:5“Hili ndilo Bwana asemalo: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha! 1037:10 Law 26:36-38; Isa 30:17; Yer 21:4-5, 10Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.”

11Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao, 1237:12 Yer 32:9Yeremia akaanza kuondoka mjini ili kwenda nchi ya Benyamini ili akapate sehemu yake ya milki miongoni mwa watu huko. 1337:13 Yer 20:2; 21:9Lakini alipofika kwenye Lango la Benyamini, mkuu wa walinzi, ambaye jina lake lilikuwa Iriya mwana wa Shelemia mwana wa Hanania, akamkamata Yeremia na kusema, “Wewe unakwenda kujiunga na Wakaldayo!”

1437:14 Isa 58:6; Yer 40:4Yeremia akasema, “Hiyo si kweli, mimi sijiungi na Wakaldayo.” Lakini Iriya hakumsikiliza; badala yake, akamkamata Yeremia na kumpeleka kwa maafisa. 1537:15 Yer 20:2; 38:26; Ebr 11:36; Mdo 5:40; 12:6; 1Fal 22:27Wakamkasirikia Yeremia, wakaamuru apigwe, na akafungwa katika nyumba ya Yonathani mwandishi waliyokuwa wameifanya gereza.

16Yeremia akawekwa kwenye chumba kilichofukuliwa chini, kilichojengwa kwa zege ndani ya gereza chini ya ngome, akakaa huko kwa muda mrefu. 1737:17 Yer 15:11; 38:16; 21:7; Mwa 25:22Kisha Mfalme Sedekia akatumana aletwe katika jumba la kifalme, mahali alipomuuliza kwa siri, “Je, kuna neno lolote kutoka kwa Bwana?”

Yeremia akajibu, “Ndiyo, utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli.”

1837:18 1Sam 16:18; Yn 10:32; Mdo 25:8Kisha Yeremia akamwambia Mfalme Sedekia, “Nimefanya kosa gani dhidi yako na maafisa wako au watu hawa, hata ukanitia gerezani? 1937:19 Yer 14:13; Eze 13:2Wako wapi manabii wako waliokutabiria wakisema, ‘Mfalme wa Babeli hatakushambulia wewe wala nchi hii?’ 20Lakini sasa, bwana wangu mfalme, tafadhali sikiliza. Niruhusu nilete maombi yangu mbele yako, usinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, nisije nikafia humo.”

2137:21 Law 26:26; 2Kor 4; 6; Isa 33:16; 2Fal 25:3; Yer 52:6; 39:13-14Ndipo Mfalme Sedekia akatoa maagizo Yeremia awekwe katika ua wa walinzi, na apewe mkate kutoka mitaa ya waokaji kila siku mpaka mikate yote katika mji itakapokwisha. Kwa hiyo Yeremia akabaki katika ua wa walinzi.